Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa

ukitaka kutafuta uwiano juu ya hilo, usitazame kina dangote, angalia matajiri wa kawaida, maana ndio wengi, japo hata dangote hana darasa, kwa sababu hata cv yake ni businiss student, sasa hiyo ni elimu gani?
Dangote kamaliza chuo bachelor degree, pia elimu ya chuo kikuu usaidia mtu kufanikiwa maana tafiti zinaonyesha matajiri wengi duniani level yao ya elimu ni kuanzia bachelor degree
 
mhm , mafanikio ni nyota ya mtu ndugu, na wala hayana formula, pamoja na porojo zoote sijui vitabu , mafunzo ya ujasilia mali, huyo huyo anayecht unaweza kukuta huko face book akapata mchongo akauajiri na wewe
Mkuu nyota gani ? Unaamini karika ushirikina? Duniani hakuna bahati inayokuja bila kuitengenezea mazingira
 
Unachokisema kinaweza kuwa na mahusiano kwa kiasi flani ila mafinikio hayana mpango maalumu unaweza ukawa umesoma vyuo vyote na mavyeti kibao lakini usiwe na mafanikio yoyote lakini unaweza mkuta tajiri mkubwa ameishia la saba tu au hata kujua kusoma alikuwa hajui ila amejifundisha kusoma baada ya kuwa tajiri
Mkuu mbona unaongelea matajiri wapi, wa kwenye forbes list?, au ukimuona tu mtu anamiliki gari na nyumba basi ni tajiri?
 
1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi, ana pesa za kununua nguo lakini hana pesa za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia movie, kusoma magazeti na kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana muda wa kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku zote hujiona anajua kuliko mtu yeyote yule na hapendi kujifunza kwa wengine. Huongea sana kuliko kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo.
Mafanikio huja tu hata kama unahayo mambo
 
Mafanikio kila mtu anayapima kwa upande wake mkuu,kuna mtu akinunua nguo na kujaza makabati na mabegi kwake ni mafanikio

2.Kuna mtu yeye akimiliki nyumba lakini analala njaa hayo kwake ni mafanikio.

3.Kuna mtu akinunua gari huku akiwa amepanga yeye kwake ni mafanikio.

4.Kuna mtu kuhama chumba kimoja na kupanga vyumba viwili kwake ni mafanikio.

5.Kuna mtu mwingine akiuza gari ya milioni 20 akanunua uwanja wa milioni 5 na zinazobaki akapiga starehe mpak zikaisha kwake ni mafanikio.

6.Kuna mtu akiwa na demu geto huku ana TV ,Sub woofer,piki piki,Dstv na chenji za kubadilisha mboga kwake ni mafanikio

Hivyo basi kila mtu anayo mafanikio yake,tahadhari ni kwamba usije kuwa kile ambacho wewe unacho basi kila mtu awe nacho ndo uone amefanikiwa...

Mafanikio ni yale matakwa ya mtu husika akiyakamilisha ndo kwake huita mafanikio,hivyo kama kuna watu wanaweka mabando kwenye simu zao walizonunua kwa pesa zao wenyewe na kukesha kuchati hakuna ubaya wowote labda kwake ndo mafanikio.

KILA MTU HUYAPIMA MAFANIKIO KWA KUTIMIZA MALENGO ALIYOJIWEKEA,ASIJE AKAKUDANGANYA MTU KWAMBA KUSOMA VITABU NDO KUFANIKIWA,HAO PIA HUPIGIA PROMO VITABU VYAO ILIWAUZE WAPATE MAFANIKIO

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..
 
1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi, ana pesa za kununua nguo lakini hana pesa za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia movie, kusoma magazeti na kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana muda wa kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku zote hujiona anajua kuliko mtu yeyote yule na hapendi kujifunza kwa wengine. Huongea sana kuliko kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo.
Kuna watu wana hizi tabia ila wamefanikiwa, mimi binafsi nineshuhudia wasiofanikiwa ni wale ambao hawapendi ushirikiano na wanaokaa kusema ya watu.
 
Kinachofurahisha zaidi, ukisoma comments za watu unaanza kuona baadhi ya mambo ambayo mleta uzi ameyataja.

Watu ambao watachelewa kufanikipiwa ni pamoja na wale wasiopenda kukosolewa, ama kusikia/kuambiwa tofauti na mambo yanayoyaamini wao kuwa ndio sahihi. They are not "open minded".
 
Tena siku hizi za karantini hiyo mitandao ndo inafnya kazi kuliko siku nyingine zozote zile
 
Back
Top Bottom