Taarifa ikufikie kwamba mabasi hayo yatakapoanza daladala zote zitatoka na alielithibitisha hilo March 29 2016 ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) David Mziray wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukosekana vituo kwenye barabara ya Morogoro.
>>>’huu mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapoanza mabasi ya daladala yote yatatoka, ndio maana utaona mabasi mengi yanayotumia barabara hizi za mchanganganyiko kwa maana magari ya kawaida na mabasi, hakuna vituo vya daladala kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito, yakishaanza haya mabasi ya mwendo wa haraka, huduma hizi za mabasi ya kawaida zitasimama’
NB: Naombeni ufafanuzi,
1. Huu mradi wa DART kuna kipindi tulisikia kuna majadiliano kati ya uongozi na madereva wa DSM, je wamejumuishwa katika umiliki?
2. Mradi unamilikiwa na serikali kwa asilimia ngapi?
3. Ina maana vipato vyote vya wananchi wamiliki wa dala dala vinahamia kwa mtu(kampuni) mmoja?kama sivyo je hawa wadau serikali ina mpango gani nao?