Tanzania kuuza dagaa nje ya nchi
Dagaa waliokuwa wakidhaniwa kuwa ni chakula cha watu maskini, sasa wameboreshwa na kupata sokoDar es Salaam. Dagaa waliokuwa wakidhaniwa kuwa ni chakula cha watu maskini, sasa wameboreshwa na kupata soko nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua mashindano ya wachakataji dagaa yalioanzishwa na Jumuiya ya Ulaya (EU), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Yohana Budeba, alisema dagaa hao watauzwa katika nchi za Ulaya, Zambia, Namibia, Malawi, Uganda na Zimbabwe.
Alisema vikundi vinavyoshiriki mashindano hayo ni 20 kutoka mikoa ya Mwanza, Kigoma, Geita, Mara na Kagera na kwamba Serikali imejipanga kutoa elimu ya kutosha kwa wachakataji na wavuvi.
Budeba alisema watazunguka katika mikoa hiyo kuwahamasisha wavuvi kutumia nyavu sahihi za uvuvi ili kuwalinda dagaa wasiishe kama ilivyokuwa kwa samaki aina ya Kamba.
Chanzo: Mwananchi