CRDB muwe makini kwenye mikopo

Hizi bank kwani zimebadili taratibu ya mikopo ya kiofisi?

Hii ngumu sana kutokea maelezo yako yanatia shaka kwa zaidi ya asilimia zote
 
Ahsante mkuu. Kama ni mtumishi was umma au binafsi, CRDB hawatoi mkopo bila kuja kwa immediate supervisor wa muomba mkopo kuthibitisha picha ya muomba mkopo, majina yake na jina na shahihi ya aliyemsainia kama immediate supervisor. Na wanakuja kwenye kituo cha kazi. Huyo jamaa yako afuatilia kama hayo yote yalifanyika.
I concur with you. CRDB wako makini. Kuna shida kidogo NMB.
 
Sio kweli!
Zile fomu kuna sehemu ambayo lazima watie sahihi waweka sahihi (signatories) wa taasisi husika.
Kama mleta uzi ni mume wako amekudanganya kuwa amelizwa.
Atakuwa amemkopea bi mdogo wanataka kujenga.
Hakuna kitu kama hicho.
Pia lazima kuwe na barua ya mwajiri ya kuthibitisha kuhusu mwombaji
 
Sio kweli!
Zile fomu kuna sehemu ambayo lazima watie sahihi waweka sahihi (signatories) wa taasisi husika.
Kama mleta uzi ni mume wako amekudanganya kuwa amelizwa.
Atakuwa amemkopea bi mdogo wanataka kujenga.
Hakuna kitu kama hicho.
Pia lazima kuwe na barua ya mwajiri ya kuthibitisha kuhusu mwombaji
 
Mleta Uzi ni mke wa mdanganyaji. Mme kapata mkopo wooote kapeleka anakokujua au kaonga au kanywa pombe alafu masikini kaenda kumdanganya mke wake! Mke shtuka! Mmeo kakudanganya mabenki yako makini sana hayawezi kumpa mkopo mtu ambaye siyo!
 
Ni kuweka mdani kuanzia aliyepeleka hizo form kwa ajili ya makato

Afisa utumishi akipitisha makato nae anachakujibu

Afisa mikopo aliyepitisha kwa kuweka sahihi yake nae sukuma ndani


Baada ya hapo mnakaa na meneja wa benki kupitia cctv footage kujua kilichojiri kwenye tarehe husika huo mchezo mchafu ulipofanyika
Umetisha jombaa...
 
Kikawaida, benki hazifanyi kazi na HR yeyote ili mradi yupo ofisini. Benki zina deal na HR aliye certified kuhudumia specific bank. Ikitokea ukasainiwa na HR ambaye hatambuliki na benki husika, hupewi mkopo. Kwahiyo sasa, huyo HR mkuu anamjua ni HR gani aliyepitisha huo mkopo. Aanzie hapo kumsaidia huyo jamaa yake wa stuli ndefu. Akimuona ana complicate ajue hilo deal analijua na walipanga "kumpiga".
Nina wasi wasi na huyu mwamba(Hr) anataka kumpiga huyo jamaa yake.ki kawaida haiwezekani.
 
Maofisa wa benk walivyomakini kukagua viambatanishi wakati wa kuomba mkopo sidhani kama wanaweza kufanya uzembe huo. Hata benki statement nayo alifoji? Mleta uzi usituletee masihala! Mimi nilishawahi kukopa karibu benki zoote najua wanavyokagua na kujihakikishia tena kupitia maofisa zaidi ya mmoja hawawezi kukosea!
Bank statement inahitajika endapo mshahara wa mwombaji hupitii benk anayokopea.
 
Katika kutoa mikopo ya watumishi
kwenye mabenki..

Pesa haitaweza kuwekwa kwenye akaunti ya mteja mpaka makato yapitishwe na afisa utumishi..

Na kupitishwa kwa makato na afisa utumishi ni lazima ajiridhishe kwamba muhusika ni yeye na documents zote zipo ok..

Nakushangaa ukisema pesa kapata bila afisa utumishi kuingiza makato kwenye 'LAWSON'


Kuna walakini hapa
huko sawa kabisa mpaka HR apitie lawson ndio asaini mkopo
 
Ndugu yangu walitaka kumpiga hela ndefu. Mida ya saa 9 alasiri ya leo huyu jamaa yangu alipigiwa simu na afisa utumishi (HR) wake kuwa afike ofisini haraka,kuna dharura inayomhusu.

Aliyoyakuta alitaka kuzimia,hasa kipindi hiki cha Magu. Kuna mtu amechukua mkopo CRDB,tsh 15,000,000/_ kwa jina lake. Copy ya salary slip na barua ya uthibitisho kazini ni ya kwake.

Ila kitambulisho cha kazi ina jina lake,(lakini sio halisi), kadi ya kura ni ya majina yake ila picha sio yake(hajajiandikisha kupiga kura,anatumia national ID kwa mambo yake) na picha iliyoko kwenye fomu si yake.

HR alimwambia huyu mtu ameshachukua hizo fedha,na benki wameleta hizo fomu ili aanze kukatwa/marejesho yaanze mwezi huu.

Hapa jamaa yangu amelala baada kunywa dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa na kushusha BP. Hali ni tete. Ila HR amemhakikishia kuwa hajapitisha makato hayo.

Kwangu ni mara ya kwanza kukumbana na tukio hii. Wenye kujua haya mambo karibuni kutoa elimu.
Kwanini awe mwoga kwa jambo asilohusika sanasana yeye alitakiwa kuwafungulia kesi benki kwa utapeli na kuwadai fidia
 
Back
Top Bottom