Baada ya kuchagua camera kwa matumizi na budget yako (episode I), sasa tuanze
kurecord. Tuta-assume accessories chache sana tunazihitaji kutokana na budget yetu.
Tufanye sisi ni content creator tunaoongelea mambo ya
mapishi. Sasa tuanze kuset mazingira yetu ya kurecord.
Tutaweka story katika sehemu/mazingira ya aina tatu:
1. Unavyowakaribisha watazamaji wako. Na kuwaambia leo tunapika nini, mahitaji ni yepi, itachukua muda gani etc.
2. Tunavyoandaa mahitaji ya kupika na vifaa vya kupikia, na shughuli yenyewe ya upishi.
3. Tunavyoset vyakula mezani baada ya kupika na kuwaaga watazamaji wetu.
Hii ni storyline ambayo mimi nineona inaweza kufaa, unaweza ukaja na yako kwa kuongeza au kupunguza.
Sasa setting yangu ya light na camera nataka iwe ivi.
Mazingira ya Kwanza
Mpishi wetu atakaa mbele ya camera. Tutakua na background ya jiko maua na tutakua na source tatu za mwanga.
Source ya kwanza: Key light (main source), hii inakua na mwanga mkali, na inakaa nyuzi 45 na camera yako na kidogo ikae juu ya utosi wako.
Ya pili: Fill light, kidogo mwanga mdogo, inakaa opposite na main light.
Ya tatu: Background light (mbwembwe light) hii unaiweka nyuma yako. Mwanga mdogo sana. Unaweza kutumia table lamp au ata mwanga wa LED tubes zile.
Katika hii story, mpishi anaongea direct na camera kwahiyo Mic ni accessory nyingine ya muhimu sana.
Mazingira ya Pili:
Mpishi hataonekana, itakua inaonekana mikono inavyofanya kazi, na vyombo vinavyoangaika na vitu vinavyopikika.
Camera nitaset nyuzi 45 hadi 90 kutoka kwenye meza yangu.
Hii shot commonly tunaiita over the head shot au top shot, wewe tu.
Sasa mwanga nitaweka taa za aina mbili, main light (key light) na itasaidiwa na second light (fill) kupunguza glare na vivuli.
Hapa Mic sio issue, kwasababu kutakua na kukata kata sana vipande, mpishi anaweza akawa haongei tutaweka sauti baadae wakati wa post-edit.
Sishauri sana kutumia ring light, ila kama upo na tight budget unaweza kutumia source moja tu.
Mazingira ya Tatu:
Hii itakua mixer ya setting ya kwanza na ya pili.
Mfano anavyowaaga watazamaji wake atakua anatumia setting ya kwanza ya kukaa mbele ya camera na anavyoandaa vitu mezani atatumia setting ya pili ya over the head shot.
Mnaonaje hapa wakuu.