Felix Mwakyembe
Member
- Feb 13, 2017
- 9
- 16
Pamoja nauwepo maji ya kutosha lakini watuwanakosa maji safi na salama ya kutumia
Hivi karibuni, katika Jiji la Nairobi nchini Kenya, ilizinduliwa Taarifa kuhusu Hali ya Mazingira ya Afrika kwa mwaka 2024, ikiangazia zaidi suala la upatikanaji maji salama barani humu.
Kikubwa katika uzinduzi huo ilikuwa changamoto ya usalama wa maji inalikabili Bara la Afrika, ikielezwa kuugua ugonjwa unaofahamika kwa lugha ya Kiingereza kama “Congo syndrome,” kwa tafsiri isiyo rasmi ni ugonjwa wa Kongo.
Kwa kifupi, ugonjwa wa Kongo, unaelezwa kuwa ni ile hali ya kujaaliwa maji mengi lakini watu wakikosa maji safi na salama ya kutumia, huizoea hali hiyo na kuifanya kuwa sehemu ya maisha yao, hivyo kutokujali tena, kwamba kunakuwa namaji kila mahali, lakini kukikosekana hata tone kwa ajili ya kunywa.
Hali hiyo inatambulika hivyo kutokana nan chi hiyo ya Kongo kuwa na utajiri mkubwa wa maji lakini wtu wake wakikabiliwa na uhaba wa maji kwa ajili ya matumizi yao.
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) inaielezea DRC kuwa nchi yenye utajiri mkubwa zaidi wa maji katika Bara la Afrika, huku mito na maziwa nchini humo ikikadiriwa kuwa na kilometa 86,080 za maji na ni kwa ukweli huu ndipo hali ya uwepo wa maji ya kutosha lakini watu wakikabiliwa na uhaba wa maji kwa ajili ya matumizi, hivyo kutambulika kwa “Congo syndrome.”
Ni katika mukhtadha huu, ambapo kitendo cha watu barani Afrika kukabiliwa na uhaba wa maji safi na salama wakati bara hilo likijaaliwa rasilimali maji ya kutosha, imesababisha na ugonjwa huo wa Kongo na hapa Mkurugenzi Mkuu wa CSE, Sunita Narain anasema,
“Uwepo wa maji ya kutosha haina maana ya usalama wa maji, na mabadiliko ya tabianchi sio sababu ya ukame, mafuriko na madhara mengine, bali ni usimamizi.”
Taarifa hiyo iliyozinduliwa na Kituo cha Sayansi na Mazingira (CSE) cha New Delhi nchini India kwa kushirikiana na Taasisi ya Mazingira, Sayansi, Afya na Kilimo (MESHA) ya nchini Kenya inabainisha kuwa uhaba wa upatikanaji maji salama na usafi wa mazingira unasababisha kiwango cha matukio ya maradhi ya kuambukiza kwa njia ya maji kuwa juu hivyo kuathiri uhai na tija katika shughuli za kiuchumi barani humo.
Tafiti zinabainisha kuwa mambo haya mawili, umasikini na magonjwa yametengeza mnyororo ambapo hivi sasa nusu ya kazi za uzalishaji wafanyazo wakulima wadogo wenye kuandamwa na maradhi barani Afrika huishia kulisha minyoo inayowasababishia kuungua.
“Nusu ya kazi inayofanywa na mkulima mdogo mgonjwa huenda kulisha minyoo inayowafanya waugue,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo, tafsiri ni yangu.
Dira ya maji Afrika, 2025 inabainisha uwepo wa uhusiano baina ya maji na umasikini, na ni kutokana na uhusiano huo, kiwango cha upatikanaji maji na usafi wa mazingira katika bara hili kimethibitishwa kuwa chini.
Hata hivyo wakati wakazi wengi wa Bara la Afrika wakikabiliwa na uhaba wa maji salama, tafiti zinaonyesha bara hilo kuwa na utajiri wa vyanzo vya maji, ikiwemo mito mikubwa zaidi ya 17, zaidi ya maziwa 160, na eneo kubwa la ardhioevu.
Vyanzo vingine vya maji barani humo ni pamoja na Chemi chemi zenye kilometa za mraba 0.66 za maji, kiwango hiki kinaelezwa kuwa zaidi ya mara 100 ya maji safi yote yapatikanayo kwa mwaka kutoka kwenye mito na mabwawa barani humo.
Takwimu zaidi zilizotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, zinaonyesha kuwepo kwa vyanzo vya rasilimali maji (Africa renewable water resource) vyenye wastani wa kilometa za mraba 3,930, kiwango ambacho ni chini ya asilimia tisa ya jumla ya vyanzo vyote duniani.
UNEP, kama lilivyonukuliwa kwenye taarifa ya Kituo cha Sayansi na Mazingira, linaonyesha kuwa takribani asilimia moja ya eneo la Afrika ni ardhioevu, huku maji yaliyopo aridhini yakikadiriwa kuwa kilometa za mraba 660,000.
“Bara la Afrika limejaliwa kuwa na rasilimali maji ya kutosha, ikiwemo Mto Nile unaotambulika kuwa ndio mto mrefu zaidi duniani, japo makadirio mengine yanauonyesha Mto Amazon kuwa ndio mrefu zaidi, Ziwa Viktoria ni la pili kwa ukubwa duniani,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo ikionyesha utajiri wa rasilimali maji kwa Bara la Afrika.
Hali ya maji ikiwa hivi kwa Bara zima la Afrika, Benki ya Dunia (WB), inaikadiria Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pekee kuwa na nusu ya maji yote yapatikanayo kwenye uso wa bara hili.
Katikati ya kadhia hii ya maji, wadau wa mazingira wanabainisha kuwa jambo hilo lina uhusiano wa moja kwa moja na utawala bora katika usimamizi wa rasilimali maji na uboreshaji wa eneo hilo ndilo suluhisho la uwepo wa usalama wa maji barani humo.
Vipo vikwazo viwili vinavyobainishwa katika taarifa hiyo ya mazingira ya mwaka 2024 ambavyo bara hilo linapaswa kuvikabili, ikiwemo kile cha serikali kuwa ndio msambazaji mkuu wa maji, ikichukua nafasi ya familia na jamii kama ngazi ya msingi katika upatikanaji na usimamizi wa maji.
Pili ni utegemezi kwa maji yaliyopo juu na chini ya ardhi, huku utegemezi kwa maji ya mvua na mafuriko ukiporomoka pamoja na maji hayo kuwepo kwa wingi kuliko yale ya mito au chini ya ardhi.
Hivyo, uvunaji maji ya mvua unatajwa na taarifa hiyo kuwa moja ya suluhisho la usalama wa maji barani humo, kwani sio tu kuwa chanzo kitakachoongeza kiwango cha upatikanaji maji safi na salama bali pia ushirikishwaji jamii kwa kuweka usimamizi wa rasilimali hiyo kuwa suala la kila mmoja.
Uvunaji maji ya mvua sio jambo jipya kwa jamii za Kiafrika, lilikuwepo, hivyo itapunguza utegemezi kwa taasisi za serikali kukidhi mahitaji ya maji na kupunguza ruzuku ya serikali kutokana na ushiriki wa kila mwana jamii katika kugharamia mahitaji yake ya maji.
Hatua hiyo itahamasisha jamii kuhimili mahitaji yao ya maji, na ieleweke pia kwamba uvunaji maji itakuwa sehemu ya mpango wa pamoja wa maendeleo endelevu ya ardhi na vyanzo vya maji kwa maeneo ya vijijini.