Vituo vya CNN, ABC, CBS na NBC wagoma kurusha tangazo la kuisifia serikali ya Rais Trump kwa matokeo chanya ya siku 100 ya awali madarakani
Tangazo hilo lililotolewa tarehe 1 May 2017 lilikataliwa na vituo vikubwa vya televisheni nchini Marekani bila maelezo.
Lara Trump, mke wa mtoto wake Rais Trump, na ambaye ni mshauri wa
kikundi maalum cha Donald J. Trump For President Inc. kinachoandaa kampeni ya Rais Trump 2020, ameeleza hatua hii kama kuingilia uhuru wa kujieleza na kuita hatua hii ya vituo hivi kama ukiukwaji wa Katiba.
Lara Trump amesisitiza kuwa tangazo hili linaweka ukweli wa mafanikio ya Rais Trump na serikali yake ndani ya siku 100 za awali madarakani na si vinginevyo.
https://www.donaldjtrump.com/media/...ck-paid-campaign-ad-setting-a-chilling-preced
Tangazo hili linaonekana kuwabeza vyombo vikubwa vya habari (mainstream media) na kuwaita waongo yaani fake news.
Vituo hivi vya televisheni mpaka sasa havijatoa maelezo yoyote kuhusiana na sakata hili.