Ndani ya US kuna US intelligence community zilikuwa 16 ila kwa sasa zipo 17 lakini zote zinafanya kazi kwa kutegemeana na kuna zingine hata ukzisema hakuna mtu anayezigua ila kuna zle zinajulikana kama "Big Five" (+1) kutokana na ukubwa wa majukumu yao na utendaji wao wa kazi kulinganisha na vyombo vingine lakini vyote 17 zinasimamiwa na DNI taasisi hii imeanzishwa April 22,2005 kwa sheria ya National security act ya mwaka 1947 na madhumuni yake yalikuwa kufanya kazi chini ya CIA ktk mambo ya kudeal na ugaidi na office zake zilikuwa Fairfax, Virginia, United States yalipo makao ya CIA
July ,30,2008 rais George W. Bush kwa kutumia Executive order number 13470 akifanya amendments Executive order yake ya April 22,2005 Executive order number 12333 iliyotumika kuanzisha DNI ambayo ilikuja kusainiwa na rais Obama october 22 na kuipatia mamlaka DNI kuchukua overall responsbility ya kusimamia all intelligence community na kuziamisha office zao kutoka Fairfax, Virginia, United States mpaka Washington Fort Meade, Maryland , U.S. yalipo makao makuu ya NSA
Sasa kwa vile umeomba ujua kuhusu CIA,NSA na FBI sasa tujikite kwenye maombi yako ya kujua juu ya taasisi hz
NSA (National Security Agency) taasisi hii kubwa naweza kusema inawezekana ikawa ni kubwa kwa majukumu kwa sababu taasisi zote zinaitegemea taasisi hii kwa njia moja ama nyingine pia ndio taasisi ya intelligence ndani ya US yenye bajeti kubwa na wafanyakazi wengi kuliko taasisi zote za intelligence ndani ya US makao yake makuu yakiwa Fort Meade, Maryland inakadiliwa kuwa na wafanyakazi 30,000 mapaka 50,000 wakiwa wanafanya kazi ndani ya jengo moja so ni kama kijiji waliofika Fort Meade, Maryland watakuwa mashaidi kwa hili kutokana na ukubwa wa jengo na eneo kazi yao kubwa ni (MCP) yani Monitoring,Collecting na Processing information na data duniani kwa maslai mapana ya US ikiwa na wakalimani wa lugha na mabingwa wa kucrack codes zaid ya 3500 so information yeyote hata uongee kizigua ,kimakonde watajua tu ulikuwa unasema nn taasisi hii iliyoanziswa mwaka 1952 baada ya kuonekana kama human espionage kama vile inazidiwa nguvu kutokana na matumizi na uvumbuzi mkubwa wa technology na ilikuja kuonekena umuhimu wake zaid mwaka 1980 kwani hii iliundwa zaid kusaidiana na CIA kwa maana CIA wanatumia human espionage kuliko technology espionage katk kazi zao
Pia majukumu yao mengine ni kulinda viongozi na intellgence zote ndani ya US ktk swala la cyber security ikiwa na wataalamu kutoka kila pande ndani ya dunia yapo mengi sana ya kuelezea juu ya NSA lakini kwa ufupi sana ni hayo tu
CIA ( Central Intelligence Agency) moja ya taasisi pendwa duniani kutokana na weledi wao juu ya maswala ya intellgence pia kuhakikisha 50 US states zinakuwa safe dhidi ya threat kutoka sehemu mbalimbali duniani kwani kwa record zilizopo ni kuwa US ndo nchi inayopendwa sana duniani kutokana na raia wa nchi mbalimbali kutamani kuishi au kutembelea US pia ndio nchi yenye maadui wengi kuliko nchi yeyote duniani kwani wanasema kiwango kilekile unachopendwa ndio kiwango kilekile unachochukiwa
CIA ndio taasisi namba mbili duniani ya Intelligence Agency kwa ubora baada ya inter - service intelligence (ISI) ya Pakistan ikiwa na wafanyakazi wanaokadiliwa 21,642 duniani kumbuka mambo ya ujasusi ni siri so kuna watu wengine ni undercover agents so inakuwa ni ngumu kwa nchi kusema ina wafanyakazi wangapi ktk idara fulani CIA ilianziswa mwaka 1947 na makao yake makuu yakiwa Langley, Virginia, U.S. na kazi yao ni (CP) collecting na processing information so ukiangalia NSA na CIA wamezidiana vitu viliwi ambavyo ni Monitoring , Data kwani CIA yy anacollect na kuprocess information tu
CIA wanatumia humani kama kitendea kazi chao kikubwa wakati NSA anatumia Technology kama kitendea kazi chake kikubwa lakni mpaka leo mabingwa na makingpin wa ujasusi wanakubaliana kuwa human intellgence ndo inaleta matokeo chanya zaidi ya Tech intellgence mfano ukitumia mtu unahukakika wa kupata taarifa sahihi na zenye uhakika zaid kuliko ukitumia tech ndo maana kuna mahusiano ya karibu sana kati ya Langley, Virginia, U.S. na Fort Meade, Maryland kwani tech inaweza kuwa hacked na kukuletea majibu ya uongo lakini huwezi kumuhack binadamu sana sana utamkamata tu pia hapo unaweza usipate information yeyote hata kama ukitesa au kumuua ok nadhani niishie hapo juu ya CIA jambo yako mengi sana juu ya taasisi hii pendwa
FBI ( Federal Bureau of Investigation) hii inajulikana kama domestic intelligence and security ilianzishwa mwaka 1908 na ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 35,239 makao makuu yake ni Northwest, Washington, D.C. kazi yake kubwa ni (CCI) counterterrorism , counterintelligence na investgations federal crimes
Ikumbukwe US ni muunganiko wa nchi (states) 50 zote zikiwa na kila kitu chake kuanzia police na sheria zake ndo maana unaweza kukuta kuna sheria hii kwa state fulani ni kosa kwenye states nyingine si kosa so kukiwa na mkanganyiko huu kunaitajika kuwe na taasisi moja yenye mamlaka zaidi ya police wa states husika ndo maana kukaundwa FBI kama ni US states police wenye kudeal na federal case na federal crimes nchi nzima na wanamamlaka juu ya states police zote kama NYPD,LAPD,CHPD na zingine zote pia ktk balozi zote za US dunian FBI wapo kama (ESA) kwani sheria za kimataifa zinatambua kama ubalozi ni sehemu ya nchi inayoumiliki huo ubalozi ndo maana mpaka leo police wa Uingereza wapo nje ya ubalozi wa Ecuador , London wanamsubili Julian Assange mmiliki wa mtandao wa wikileaks kwani wakiingia ndani ya ubalozi itakuwa ni act of war kwani ni sawa na kuivamia nchi nyingine
Sasa kwa concept hyo FBI wakiwa ndani ya ubalozi wa US popote dunian wanahesabiwa kama wako ndani ya US soil
kama mnakumbuka yule msomali aliyeuwawa nadhani ni mwaka jana nchini kenya nje ya ubalozi wa US baada ya kumtishia kisu mlinzi wa ubalozi FBI ndio walikuwa wanaukagua ule mwili naomba niishie hapo hope nimekujibu swali lako
Decentman pia mkuu
comrade igwe ameelezea kwa ufupi hapo juu