Chuo cha mifugo Tengeru, hatarini!

Panthera 1

Member
Dec 30, 2014
50
9
Habari za muda huu watanzania wenzangu,

Napenda kuchukua hatua hii kuelezea hatari iliyopo ndami ya chuo cha mifugo Tengeru ambacho ni moja kati ya vyou vilivyokuwa maarufu hapa Tanzania lakini kwa sasa chuo hakipo katika hali ya ubora.

Mamia ya mifugo ilokuwepo hapa chuoni haipo na sijui kama serikali imefuatilia hilo lengo langu la leo ni kuelezea tatizo la maji lilokikumba chuo hiki kwa muda wa miezi miwili sasa bila upatikanaji wake licha ya kwamba kuna mkusanyiko mkubwa wa wanafunzi na mamia ya wafanya kazi na bado Arusha ipo katika wasiwasi wa mlipuko wa kipindupindu.

Mpaka sasa wanafunzi na wafanya kazi wapo katika hatari kwa kukosekana huduma hiyo muhimu na tayari mpaka sasa kila kaya ndani ya chuo hiki imechangishwa mchango wa elfu thelathini za kitanzania kwa ajili ya kununua mashine ya kuvutia maji kutoka ziwa Duluti haijulikana mpaka sasa ni lini huduma ya naji itarejea na kuwaweka wanafunzi wetu katika ya usalama zaidi.

OMBI.
Waziri wa mifugo karibu chuo cha mifugo Tengeru uje kutazama jinsi mambo yalivyobadilika, mifugo ya leo siyo ya zamani.
 
Vp kuhusu Kinangop wale mbuzi wetuna kondoo wapo? Piggery unit je na Ng'ombe wale wa Shoo 2 farasi je hivi wale kuku zaidi ya 1000 wapo.Niliacha common room inawika haswa je ni vile au wameimaliza? Dah soil napo mkuu tulikuwa tunaamka saa tisa na nusu usiku kwenda kukamua wale Jesse maziwa kibao Siagi ndiyo mpaka basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…