Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 866
Upo mjadala mpana sana na bishaniwa kuhusu chimbuko la tattoo Duniani, mpaka kufika mwaka 2015 wanasayansi wengi wa kihistoria walikubaliana kwamba chimbuko la tattoo ni ulaya ya kati yani huko Oztal Alps.
Walihitimisha uchunguzi wao kurejelea mwili wa kale uliopatikana huko Oztal Alps ulioitwa "Ötzi", jina hilo linamanisha "Mtu wa barafu aliyekaushwa kwa asili kutokana na kufunikwa na barafu miaka mingi".
Mtu huyo alikutwa na tattoos 61, alikutwa amefunikwa na barafu (glacial ice) katika mlima wa Alps, na anatajwa kuwa aliishi miaka 3250 BCE. Utafiti huo uliofanywa huko chuo cha Zurich, kinacho juhusisha na Studies in Archaeology, kilihitimisha utafiti wake mwaka 2013.
Utafiti huo ni ule unaofahamika kama, Deter-Wolf, Aaron (2013). "The Material Culture and Middle Stone Age Origins of Ancient Tattooing". Tattoos and Body Modifications in Antiquity: Proceedings of the sessions at the EAA annual meetings in The Hague and Oslo, 2010/11. Zurich Studies in Archaeology. Vol. 9. Chronos Verlag. pp. 15–26.
Lakini mwaka 2018 mambo yalibadirika tena pale utafiti mwingine ulipo ishangaza Dunia hasa pale ulipo patikana mwili wa mtu mwingine aliyekutwa na tattoos nyingi huko Egypt.
Mwelekeo wa historia ya utafiti wa tattoos ukarudi Afrika, Hii ndio ikawa tattoos kongwe zaidi ulimwenguni kugunduliwa mpaka sasa.
Tattoo hii iligunduliwa kwenye maiti mbili tofauti kutoka Misri ambazo ni za miaka kati ya 3351 na 3017 BCE.
Hivyo ulimwengu wa utafiti ukahitimisha rasmi mwaka 2020 kuwa historia ya tattoos duniani imetokea Misri yani Africa.
Ikumbukwe kuwa tattoos ilikuwa ni sehemu ya urembo kwa tamaduni nyingi Afrika, toka huko mpaka sasa tattoos imechukua mabadiriko mengi kutoka kuwa utamaduni wa urembo Katika kutambulisha mila na tamaduni za makabila mbalimbali mpaka kuwa sehemu ya utamaduni wa kishenzi.
Tattoo zilibadili sura ya mitazamo mwanzoni mwa miaka ya 1920, pale zilipoanza kutumiwa na magenge mengi ya wauza madawa ya kurevya, wauuza unga walitumia tattoo katika utambulisho wao katika sehemu tofauti katika kutambuana, Ntaeleza hili kwa ufasaha Zaidi kwenye Uzi unaofuata.
Magenge ya uharifu na ya wauza unga yalifanya utamaduni wa tattoos uonekane ni uhuni na ushenzi, hii ni kuwa wengi wa wauza unga tattoos zilitumika kama "code of identity" kwenye magenge yao, nimesema hili ntalieleza kwenye Uzi mwingine sio huu.
Ok, basi tuendelee...
Mpaka kufikia miaka ya 1950 duniani kote katika majeshi mbalimbali yalidhibiti utamaduni wa tattoos katika majeshi na askali wao.
Tattoo imewekewa udhibiti chini ya sera kadhaa na nchi nyingi zimepigwa marufuku kabisa uwepo wa tattoos au askali wao kuchora tattoos, ni nchi chache zilizo ruhusu tattoo kwa askali wao.
Kuendana na kanuni na sheria za nchi nyingi tattoo zimerusiwa maeneo baadhi katika mwili hasa sehemu zilizofunikwa za mwili.
Picha ni mama mwenye tattoo za utamaduni wa Afrika, samahani iwapo picha hii italeta taharuki yoyote.
Ndimi Comred Mbwana Allyamtu CMCA