Chenji kurudishwa Ikulu; Mfumo wa fedha za serikali umebadilishwa lini?

Miaka yangu michache ya utumishi wa umma (miaka nane) nilikuwa nikishuhudia ofisi za serikali ifikapo June mwishoni huwa zinarejesha pesa iliyobaki hazina. Yaani kama hazikutumika kwa sababu yoyote ile. Niliona ipo maantiki kuzirejesha hazina maana ndipo zilipotokea.

Sasa naona kumezuka mtindo wa baadhi ya ofisi za umma (so far ni bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,NEC) kurejesha fedha Ikulu pesa iliyobaki hata kabla ya mwaka wa fedha hujaisha i.e 31/6/2016.

Hapa sipingi "chenji" kurejeshwa, bali nashangaa ni vipi zinarejeshwa Ikulu. Sijaona waraka wa hazina unaoelezea haya mabadiliko.

Naomba mwenye kujua anijuze juu ya haya mabadiliko kama yapo.
Mkuu ni kuonyesha solidairty tu kwa Rais katika harakati zake za kubana matumizi kuwa anaungwa mkono. Vinginevyo Ikulu hakuna akaunti ya serikali, si unajua fadha za serikali zinakokaa!!?
 
Watendaji wameingiwa hofu hawajiamini tena, inabidi wakurupuke huko waliko ili kutafuta hisani kwa mfalme.
 
Mimi mwenyewe nashangaa sana,ilikuwa zikirudishwa hazina sasa unafikir kutokuwa na misusuru ya upigaji picha kurudisha chenji,hayo yalikuwapo tangu mwanzo lakin fedha ilikuwa inarudishwa HAZINA,hata ukaguzi wa mahesabu wanakubali,sasa wakaguz wakija wataoba chenji nimeenda kwa rais,mambo ya ajabu tunashuhudia.
 
Kati ya hizo hela na zile chenji za rada zipi nyingi?

Na za rada zilirudishwa ikulu?
 
Jamani haya maigizo jaribuni kuzoea jamani,mbona ya Wema mmeshazoea???
 
Hao wanajipendekeza tu kwa baba jesca wakat zilipaswa kurudishwa hazina fedha zote
 
Miezi 12 ijayo hakutakuwa na mtu mwenye hamu na huyu Raisi. Style yake ya uongozi inatia shaka sana.

Watanzania tunataka kuona madawati shuleni, dawa hospitalini, barabara nzuri na vitu vinashuka bei madukani. Mbwembwe na nani karudisha nini miaka minne na nusu kabla ya uchaguzi hazileti kiki yoyote zaidi ya kupoteza muda. Muda huo angeutumia kuchagua nani anafaa kuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Back
Top Bottom