Chenge,Werema: Tume imedanganya kiasi kilichopo kwenye mchanga, wajivua lawama

Hii ngoma sio nyepesi kama akina Polepole na Shaka Hamidu Shaka wanavyotaka umma uamini. Hii huenda ikawa ni kashfa mbaya kuliko zote katika nchi hii itakayoharibu kabisa image ya nchi, Serikali, academia, etc. Italigharimu taifa kwelikweli.

Tume iliyofanya uchunguzi wa jambo zito kama lile in less than 3 months hawawezi kuja na reliable findings. Mkulu naye alifanya haraka mno; angetulia akaweka jicho la tatu kujadili findings za Tume kwa kina na umakini wa hali ya juu kabla ya kufikia maamuzi. Tumeingia cha kike watanzania; tutalipa na tutalipa gharama kwelikweli. Mwenye ufahamu na atafakari.
 
Rais kakurupuka au wewe ndo unakurupuka?
Rais ndo katoa report au tume?
Tume iliyoundwa haikuwa na uwezo wa kupata taarifa sahihi?
Mkuu tuvumiliane tu,na tuheshimu mawazo ya kila mtu.
Lakini chenge anajua alichofanya akiwa waziri
Kwanza makontena yaliyofanyiwa uchunguzi ni yale 200 na kitu yeye chenge amejuaje kwamba hakuna madini ya kiwango kilichotajwa na tume?
TUME IDANGANYE KWA LIPI?
 
Jamani nisameheni, naombeni kujua professional ya change,

Tafiti hupingwa Kwa Tafiti sasa yeye kafanya tafiti gani hadi aje apinge hiyo tafiti? Naona Kuna watu wanamsapot chenge duuh watanzania wengine sijui vichwani mwao kuna vitu gan
Halafu ni chadema eti wanampongeza chenge , mbowe awe anaangalia gazeti lake la TANZANIA DAIMA litakosa soko kwa kushabikia mrema na chenge
 
Watanzania tuwe macho na huyu BABA BASHITE tutalipishwa tena kodi zetu kama tulivyolpishwa samaki.huyu jamaa sio mzima ni bora sasa watanzania tuchukue maamuzi magumu au tuangalie upande wa pili.


Swissme
Kumbuka hii tume ilikuwa kuona kuna nini. Tume ya pili inaangalia masuala ya kisheria nakadhalika. Haraka ya nini? Kwani wewe ni geologist au chenge hata werema. Acheni hizo tuache kurukia vitu kabla ya wakati!
 
Back
Top Bottom