Lengo la mtunzi ni kutaka ujumbe wa neno la Mungu uwafikie watu kwa njia ya muziki na kwa aina ya muziki inayopendwa na watu wengi zaidi. Dhamira yake kuu ujumbe uwafikie watu wengi zaidi na wa matabaka yote kama vile watu wa bar, kwenye madisko, vilabu vya pombe n.k
Kosa lake ni kwamba aliangalia tu suala la coverage (wingi wa watu watakaousikiliza) na kusahau sualala la MAADILI ya wimbo wa dini.
Kuwaonesha watu wamevaa nguo zinazochora maungo ya miili yao siyo sahihi, vile vile kuonesha vitovu nje siyo suala la kimaadili kwani ni kweli mtu anaweza akavutiwa na wimbo lakini tayari wimbo ukamvuta na kumpelekea kwenye mawazo ya uzinzi!