Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,463
Je, COVID-19 ni nini?
COVID-19 ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya Corona, virusi hivi ni sawa sawa na vile vinavyosababisha mafua ya kawaida tofauti na mafua, virusi vya corona vinaweza kuambukiza mwingine kabla hata ya huyo mtu hajaanza kuonesha dalili. Tofauti ni kwamba, watu wenye matatizo mengine ya kiafya kama matatizo ya mapafu au ugonjwa wa kisukari, wamo katika hatari kubwa ya kuhisi kuhisi matatizo makali ya mapafu.
Watu walio na virusi vya COVID-19 kwa kawaida wataonyesha dalili zifuatazo: homa kali na kikohozi au kuhisi kuishiwa na pumzi. Athari zikizidi, wanaweza kuwa na matatizo makubwa ya kupumua na watahitaji kulazwa hospitalini au katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi wengine hupoteza maisha.
Je, COVID-19 inaenezwa vipi?
Virusi vya COVID-19 huenezwa hasa kwa kutangamana na mtu ambaye aliyeambukizwa na kuathirika au kuguza vifaa ambavyo viliguzwa au kupigiwa chafya na mgonjwa aliye na COVID-19. Virusi hivi hupatikana kwenye chembechembe za mate au makamasi. Vinaingia mwilini kwa kuguza au kupitia kwa kinywa, Pua au macho.
Jinsi ya kujizuia kupata ugonjwa wa COVID-19
Kunawa mikono kwa sabuni yako na kuepuka kugusa uso wako kwa mikono yako ni njia bora zaidi za kuepuka kupata magonjwa. Kujitenga kijamii (kudumisha angalau umbali wa mita 2 au futi 6 mbali na wengine) na kukaa nyumbani kama vile iwezekanavyo pia ni njia nzuri ya kuzuia kupata huu ugonjwa. Ili kuzuia kuambukiza virusi hivi kwa wengine, watu wanapaswa kukohoa au kupiga chafya huku wakifunika mdomo wao kwa sehemu ya ndani ya visugudi na sio kwa viganja zao na kuvaa Barakoa
COVID-19 ilianza lini?
Virusi vya Corona vimeingia Afrika Mashariki baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini Kenya tarehe 13 Mar 2020 na 16 Machi 2020 Mgonjwa wa Kwanza akagundulika Nchini Tanzania. Mlipuko wa Virusi vya Korona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ulibainika rasmi tarehe za katikati za mwezi Desemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan huko Nchini China.
Hadi sasa, zaidi ya Watu Milioni 3.81 wamepoteza Maisha kutokana na Ugonjwa wa COVID-19 Huku Watu zaidi ya Milioni 176 Wakiwa Wameambukizwa Duniani Marekani, India na Brazili zikiwa zinaongoza. WHO Coronavirus (COVID-19) Dashboard
NINI MCHANGO WA WANASAYANSI KATIKA KUPAMBANA NA COVID-19?
Kutokana na kuenea kwa kazi kwa ugonjwa wa COVID 19 ambao hadi sasa bado dawa yake haijapatikana, Watafiti wanaendelea kufanya Jitihada Pamoja na kutafuta Chanjo ya Ugonjwa.
Baadhi ya Chanjo za COVID-19 zimeonesha ubora katika kupambana na Maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19
CHANJO YA COVID-19
Nchi nyingi sasa zinatoa Chanjo za COVID-19 bure ili kujilinda na Maambukizi.
Kutokana na Chanjo ya COVID-19 kuonesha ubora wa kupamba na COVID-19 Baadhi ya Chini sasa ni lazima kuchoma sindano ya Chanjo ili uweze kuingia Nchi hizo.
Baadhi ya Mataifa ya Afrika yanayotoa chanjo na chanjo wanazotumia ni:
Morocco (AstraZeneca na Sinopharm)
Algeria (Sputnik V)
Misri (Sinopharm)
Kusini mwa jangwa la Sahara, mataifa yanayotoa chanjo ni:
Afrika ya kati(Johnson & Johnson)
Ushelisheli (Sinopharm na AstraZeneca)
Rwanda (taarifa zinasema wanatumia Pfizer na Moderna)
Mauritius (AstraZeneca)
Zimbabwe (Sinopharm)
Mataifa mengine kama vile Senegal na Guinea ya Ikweta yamepokea chanjo za Sinopharm lakini bado hazijaanza kutoa chanjo kwa umma.
Guinea ilitoa chanjo 60 za Sputnik V kutoka Urusi kwa watu kwa majaribio.
JE, KUNA UMUHIMU WA TANZANIA KUKUBALI KULETEWA CHANJO? MTIZAMO WAKO NI UPI?
Hivi karibuni Kamati maalum ya wanasayansi iliyoundwa na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa thathmini kuhusu hali ya ugonjwa Corona nchini, imeonya kuwa nchi ipo katika hatari ya kukabiliwa na wimbi la tatu iwapo hatua hazitochukuliwa.
Ripoti ya Kamati hiyo, ilitaka Serikali kuanza kuchukua hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo, kuanza kutangaza watu walioambukizwa virusi vya corona, na kuagiza chanjo. Kamati hiyo ilishauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa COVAX ulio chini ya mwamvuli wa GAVI. Mpango wa COVAX unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi.
Wakati hayo yakiendelea, Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, amewataka Wananchi wanaotaka kwenda Kuhijji, Wajiandae kuchanjwa kwani huwezi kuingia Maka Saudi Arabia bila kuchanjwa.
Hivi Sasa Serikali imeanzisha utaratibu wa kupima COVID -19 tena mara msafiri anapowasili kutokana na kuwepo vyeti vya COVID-19 vya kughushi huku wengine wakipata maambukizi wakiwa safarini na kuingiza Ugonjwa nchini.
“Kipimo tunachotumia sasa kinaonyesha majibu kwa muda mfupi na hata kama Mtu amepata maambukizi ndani ya saa mbili au tatu zilizopita tunambaini. Hii ndiyo namna ya kudhibiti maambukizi yasiingie nchini,”alisema Mkurugenzi wa huduma za kinga, Dk. Leonard Subi.
GHARAMA ZA KUPIMA UNAPOWASILI UWANJA WA NDEGE
Kwa mujibu wa utaratibu wa sasa msafiri yeyote anatakiwa kujaza fomu ya kuomba kupima Corona mtandaoni, kisha kwenda kwenye hospitali au kituo husika na kupima.
Gharama za malipo ni Dola za Marekani 100 (sawa na Sh. 230,000 ), Sh. 10,000 ya Hospitali au kituo ulichopimiwa na siku ya kurudi au kuingia nchini unatakiwa kulipa Dola 25 (sawa na Sh. 57,750)
MAMBO UNAYOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU CHANJO YA COVID-19
Usalama wa chanjo za COVID-19 ni kipaumbele cha juu. Chanjo ya COVID-19 imethibitishwa kuwa salama na yenye ufanisi.
Nchini Marekani, hatua nyingi zimewekwa ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama na zenye ufanisi. Hatua hizi zinajumuisha waliojitolea kutoka makundi mbalimbali ya rangi, kabila na umri wanaoshiriki katika majaribio ya kitabibu ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama kwa jamii mbalimbali. Taarifa na takwimu kutoka kwenye majaribio zinakaguliwa kwa kujitegemea na wanasayansi, wataalamu wa tiba, na wataalam wa afya ya umma kabla ya wewe kupewa chanjo.
Vituo vya Kudhibiti Magonjwa (CDC) vimeunda zana mpya ya kugundua haraka maswala yoyote ya usalama kuhusiana na chanjo za COVID-19. "V-safe" ni zana mpya inayotumika kwenye simu mahiri, ya kukagua afya baada ya chanjo. Itatolewa kwa watu wakati watakapokuwa wanapokea chanjo ya COVID-19.
Chanjo ya COVID 19 itakusaidia kujikinga kutokana na kupata COVID-19. Dozi mbili zinahitajika
Unahitaji dozi 2 za chanjo ya sasa ya COVID-19 ili kupata kinga kubwa zaidi dhidi ya ugonjwa huu mbaya.
Hivi sasa kuna usambazaji mdogo wa chanjo ya COVID-19 nchini Marekani, lakini usambazaji utaongezeka katika wiki na miezi ijayo
Kila mtu ataweza kupata chanjo dhidi ya COVID-19 mara tu idadi kubwa ya kutosha ya chanjo itakapopatikana. Chanjo ikishapatikana kwa wingi, kutakuwa na watoaji wa chanjo maelfu kadhaa.
Mnamo tarehe 13 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-Biotech ili kuzuia COVID-19.
Mnamo tarehe 20 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Moderna ili kuzuia COVID-19.
Ukosefu wa fedha za kulipa, hali ya uhamiaji, au ukosefu wa bima havitakuzuia kupata chanjo dhidi ya COVID-19
Dozi za chanjo zitatolewa kwa watu bila malipo bila kujali hali ya uhamiaji au ikiwa wana bima au la. Watoaji wa chanjo wanaweza kutoza ada za usimamizi wa kutoa chanjo. Watoaji wa chanjo wanaweza kulipwa ada hii na kampuni ya bima ya umma au ya binafsi ya anayepokea chanjo.
Baada ya chanjo ya COVID-19, unaweza kupatwa na athari za kawaida. Hii ni ishara kwamba mwili wako unajenga kinga
Athari ni dalili kwamba chanjo inafanya kazi, athari zinaweza kuwa kama homa na zinaweza hata kuathiri uwezo wako wa kufanya shughuli za kila siku, lakini zinapaswa kuondoka baada ya siku chache.
Kama Mwananchi, upi mtizamo wako juu ya Chanjo ya Corona na njia zinazotumika kupambana na Covid - 19 hapa nchini Tanzania?
Pia, soma:
1). Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
2). Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga