Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,054
- 4,499
Awamu ya baba wa taifa na ile ya mzee ruhusa hakukuwa na changamoto la katika katika kwa umeme maeneo ambayo huduma hii ilikuwa imeyafikia. Ni kweli kwamba maeneo hayo yalikuwa hasa kwenye miji mikubwa ya nchi. Shughuli za kiuchumi wa viwanda hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa ambapo tumesambaza huduma hii ya umeme hadi kwenye karibu kila kijiji.
Jinsi uchumi wa viwanda ulivyozidi kukua na idadi ya watu kuongezeka, ndivyo changamoto ya umeme ilivyojitokeza na kukua kila kukicha. Zilianza hasa katika kipindi cha awamu ya tatu ya Mzee Mkapa ambaye suluhisho lake lilikuwa ni kuwapa kampuni ya makaburu wa South Africa kutuendeshea Tanesco yetu. Matokeo yake hatutayasahau. Tulipigwa tukapigika.
Ikaja awamu ya nne ya Mzee Kikwete. Wao wakaona suluhisho lake ni kukodi majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka makampuni ya nje ya nchi kama yale ya Richmond, Dowans, Symbion na IPTL. Tukapigwa na kupigika hadi Waziri mkuu akatimuliwa na bunge la Mzee Sitta.
Ikaja awamu ya tano ya Mzee Magufuli. Nayo ikahangaika kwa kubana mafisadi na kuanzisha mahakama ya mafisadi kama suluhisho la changamoto hili la umeme. Kwa kiasi fulani kukawa na ahueni ya kuonesha kuwa ile ndoto ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025 labda ingaliweza kutimia.
Sasa imekuja awamu ya sita ya Mama yetu Mzee Salmia inayopenda kushirikisha wananchi wote kupata suluhisho la changamoto mbali mbali ya wananchi kidemokrasia. Kwa kuwa umeme wa bei rahisi kuliko wote ni ule unaotokana na maji. Na kwa kuwa nchi yetu imejariwa mito mingi na kuzungukwa na maziwa makubwa makubwa mengi: kwa nini maji ya ziwa kama lile la Victoria yasipekwe kwa mabomba huko kwenye bwawa la Mtera na lile la Nyerere ili wakati wa ukame kwenye mabwawa hayo, yakafunguliwa kuyajaza? Ethiopia wanatumia maji ya ziwa Victoria kupitia mto Nile kuzalisha maelfu ya maelfu ya MW za umeme hadi kuwauzia Wakenya.
Kwanini sisi tusitumie Ziwa hili ambalo liko kwetu? Kwani ni shilingi ngapi kupeleka maji ya ziwa letu huko? Kama hatuna hizo hela, tutafute pa kukopa kwani manufaa ya mkopo huu ni mkubwa sana. Hili litakuwa ni suluhisho la once and for all ya changamoto hili la umeme.
Tutaweza hata kuuza umeme nje ya nchi na kuachana na kuuza mahindi na mchele nje ya nchi wakati tukiwa tuna njaa. Tutaweza kupunguza sana bei ya umeme ili wananchi wote waweze kuitumia kama nishati rahisi ya kupikia na hivyo kuachana na ukataji wa miti wakitafuta kuni na mkaa. Mwananchi ataweza kutumia shilingi zisizozidi elfu tano tu kwa mwezi kwa nishati ya kupikia ya umeme.
Tanesco nao wataweza kukusanya matrilioni ya pesa kwani kila mwananchi atakuwa mteja wao. Viwanda vingi vitajengwa na kuzalisha bidhaa nyingi kwa bei nafuu. Kwa muda mfupi nchi yetu itakuwa upper middle income country chini ya uangalizi wa mama!
NB: Umeme utokanao na gesi mara zote bei yake ni ya juu sana (unaffordable to many of our people) ukilinganishwa na ule unaotokanq na maji. Umeme wa gesi ni kwa wakati wa dharura tu au kwa kuuza nje.