Chama cha Wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Chama cha Wamiliki wa Mabasi(TABOA) kwa kushirikiana na Wamiliki wa Malori na Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima kuanzia siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitishwa siku ya Jumanne wiki ijayo.

Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutao mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi, Malori, Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Bwana. Eneo Mrutu amesema sheria inaloyolenga kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva linasababisha mmiliki kufungwa jela.

Aidha amewaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kutopisha sheria hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.


Chanzo: ITV




 
tuwekee hiyo sheria tuisome nasisi, yaani dereva akiwahepa trafik anakamatwa tajiri, au?
 
TABOA wamwajiri Tindu wakae naye waone sheria ikae vipi na Waziri Mkuu aairishe mswaada huu ili mgomo husiwepo
 
Reactions: SDG
Duh, kosa la dereva mmiliki wa gari anahusishwa je? Yaani dereva akafanye uhuni wake huko then mmiliki akafungwe?

Tanzania sijui tunaenda wapi?
Uwezo wa Watanzania kufikiri ndo umefika hapo
 
magari ya kwao,wao wanajua wapi wapakie abiria wapi wasipakie wao ndio wanapanga...!!!

in anko's voice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…