CHADEMA yapata pigo Bumbuli, BAVICHA kimya chenu kitawaponza

Wanachama 200 wakiwamo viongozi wa Chadema katika Kitongoji cha Kwemghogho wilayani hapa wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM .

Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao jana, mbunge wa Bumbuli, January Makamba alisema uamuzi wao unatokana na CCM kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo.

Makamba alisema CCM imefanya mengi hivyo haoni ajabu kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine vya siasa.

Alisema chama hicho kina kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano na siyo migogoro, fitina na majungu.

Makamba alisema moja ya mambo yanayochangia kurudisha nyuma maendeleo ni baadhi ya watu kukaa vijiweni na kurushiana maneno, lakini kwa wana-CCM muda huo sasa haupo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema aliwahamasisha vijana kujiunga na CCM kwa kuwa ilani yake inatekelezeka kwa wakati


Chanzo: Mwananchi
Hao ni wana CCM wanajitekenya na kucheka wenyewe.
 
Ukiwa ccm lazima unakuwa na matatizo ya fikra,wanasema mkutano wa wabunge,sasa mfano cuf wana wabunge jumla kumi wa bara tu wa majimbo,jumla ya majimbo Tanzania ni Mia 300 ina maana haya majimbo 200 ualiyobaki uruhusiwi kwenda kutafuta wanachama,kufungua ofisi na kuhutubia,mikutano ya ndani mnakutana na viongozi tu sio wanachama hawa wanachama utawapata wapi tofauti na mkutano wa adhara.ccm msifurahie ushindi wakati wenzenu mmewafunga mkono,mguu,mdomo na uchochezi pembeni kesi,policcm,jeshiccm na mahakama ccm a.k Lema na Lijuakali!
 
“Kila chama kinahitaji kijijenge, uchaguzi uliopita hatukushinda sababu ya Lowassa. Uchaguzi huu umedhihirisha hilo sababu alipita katika kata zote lakini hawakushinda. 2015 tulishinda uchaguzi sababu ya nguvu za vyama vyetu,” amesema na kuongeza.

Asante Kambaya kwa kuwaumbua Nyumbu
Huwa tunawaambia kila siku kuwa fisadi hawezi kuwapeleka ikulu lkn wanajifanya kichwa ngumu
 
“Kila chama kinahitaji kijijenge, uchaguzi uliopita hatukushinda sababu ya Lowassa. Uchaguzi huu umedhihirisha hilo sababu alipita katika kata zote lakini hawakushinda. 2015 tulishinda uchaguzi sababu ya nguvu za vyama vyetu,” amesema na kuongeza.

Asante Kambaya kwa kuwaumbua Nyumbu
Huwa tunawaambia kila siku kuwa fisadi hawezi kuwapeleka ikulu lkn wanajifanya kichwa ngumu
Fisadi asiyekamatwa,kaa kimya Lugumi,Escrow,kagoda,kuuza nyumba za serikali na mv bagamoyo iliyopaki ni ccm ufisadi branch haviguswi na mpambanaji wetu
 
Hapo Bumbuli si ndio Watu mpaka wapande kwenye miti ndio wapate mawasiliano ya simu halafu Mbunge wao alikua Naibu Waziri wa Mawasiliano!
 
Kila jambo na wakati wake.

Siasa ikifanywa muda wote kazi zitafanyika muda gani?

Uchaguzi ukifika si kuna muda wa kampeni huwa unatolewa? Au tatizo ni nini?
Ndio sheria ya usajili wa vyama vya siasa inavyoelekeza, siyo? Kwamba vyama vikae tu visubiri wakati wa uchaguzi? Kama msisitizo ni kufanya kazi kwanini mnazuia vyama vingine visifanye kazi yake ya siasa, lakini mnataka mfanye nyie tu mwaka mzima?
 
Fisadi asiyekamatwa,kaa kimya Lugumi,Escrow,kagoda,kuuza nyumba za serikali na mv bagamoyo iliyopaki ni ccm ufisadi branch haviguswi na mpambanaji wetu
Kwa taarifa yako huyo Lugumi ndio mgombea urais wa chadema 2020

Na utakuja kumsafisha hapa
 
Jamani si yupo jimboni kwake na anaongea na wapiga kura wake hafanyi siasa. Kosa ni kwenda kufanya anticlockwise agenda za chama kinachoongoza. Tusubiri 2020
 
nawapongeza ..watu hao kwa kutambua maana ya demokrasia.hawajakosea kuhama na hata wakiludi tena chadem ni haki pia ya kidemokrasia
 
Kama ni habari ya kweli, hadi mwaka 2020 hata TAL atakuwa ameshahamia CCM.
Hongera Magufuli, pole sana FAM.
 
Unafki mtupu MTU wangu, kifungo cha kisiasa, je kimeisha? Au wanamjaribu mh jmp.
 
wabunge wameruhusiwa kutembelea wapiga kura wao.kinachokataliwa,Mnyika kutoka kibamba kwenda kuhutubia Geita,tabu yote ya nini
Eti eeh ila jaffo kwenda handeni na wenyeviti wa ccm wa mkoa mzima wa Tanga ni sawa??? Aseee basi tuna safari ndefu sana
 
Kila jambo na wakati wake.

Siasa ikifanywa muda wote kazi zitafanyika muda gani?

Uchaguzi ukifika si kuna muda wa kampeni huwa unatolewa? Au tatizo ni nini?
Dah mie siwaelewi ujue labda unipe fundisho leo mkuu unaposema tukifanya siasa muda gani tutafanya kazi je hiyo mikutano anayofanyaga magufuli au majaliwa huko mikoani huwa kazi zinafanyika ila akitaka kufanya lowassa ndo kazi hazifanyiki??? Duh

Ni kama bunge eti likiwa live watu hawafanyi kazi ila kipindi cha maswali na majibu kwa mawaziri mnaweka live afu majadiliano ya bunge zima ndio mnazima je ina maana mikutano ya wapinzani na pale wabunge wa upinzani wanapokuwa live ndio muda pekee ambapo watu hawafanyi kazi??? Nasubiri unieleweshe

Pia mmeruhusu wabunge majimboni kwao kufanya mikutano sasa kma unasema kazi hazitofanyika je lema akifanya mkutano arusha mjini ndo kazi zinafanyika ila akija mbowe ndo kazi hazifanyiki??? Haaahahahha anyway nisaidie hapa mkuu maana sielewi bado
 
Mikutano ya ndani ya wanachama haikuzuiliwa ndugu, usitafute visingizio
Kwahiyi mmi nikisajili chama leo ina maana sitopata wafuasi wala kunadi sera zangu za chama kipya hadi kampeni za 2020??
Kwa sheria ipi ya vyama vya siasa?? Kwa kifungu gani cha katiba?? Mnatoa wapi haya mamlaka?? Mlikutana na TCD?? Msajili aliafiki kabla hamjaweka katazo hilo??? Embu nisaidie mkuuu maana niko njiapanda
 
Back
Top Bottom