kabengo Donasian
Member
- Jun 9, 2016
- 73
- 14
Hii
Tayari wameshafungua KesiKahama. Chadema kimesema leo kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza dhidi ya Polisi, kupinga zuio la maandamano mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Akizungumza mjini Kahama jana, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na hawatanyamaza inapozuiwa na mtu, au mamlaka yoyote.
“Tutapambana kwa njia na nguvu zote kulinda demokrasia nchini, hata kama itabidi kufia uwanjani. Ikibidi kwenda mahakamani kudai haki hiyo tutafanya hivyo.” alisema
Hata hivyo, Mbowe hakuwa tayari kuthibitisha taarifa za Chadema kufungua kesi jijini Mwanza, leo.
Mawakili wa Chadema akiwamo Peter Kibatala na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walitarajiwa kuwasili Mwanza jana tayari kutoa ushauri wa kisheria na kufungua kesi.
Kama ile ya Mazishi ya kamanda MawazoMahakama itende haki
Tunaamini itatenda kama ilivyifanya kwa kamandamawazokwa mahakama zetu hakuna kipya, rejea hukumu ya mita 200, mgomo wa walimu
ngoja watafsiri sheria km ccm =policcm....
.....Chadema itashinda tu hiyo kesi hapo ni Shule tu
KILA LA KHERIBREAKING NEWS; viongozi wa Chadema Taifa wakiongozana na mawakili wazoefu wametinga mahakaman kufungua kesi kupinga suala LA polisi kuzuia mikutano ya adhara.habari na Godfrey Aspenance TN
chanzo jukwaa la siasa, whatsapp
Hofu yangu ni uhuru wa mahakamaSasa hizi ndio akili ...safi
Watashindwa kama serikali ikigundua kuna loop holes kwenye kesi ya msingi. Hapo ni vita vya kisheria tu. Mbona marehemu Mtikila amewatoa jasho serikali sana tu!Hofu yangu ni uhuru wa mahakama
Watashindwa kama serikali ikigundua kuna loop holes kwenye kesi ya msingi. Hapo ni vita vya kisheria tu. Mbona marehemu Mtikila amewatoa jasho serikali sana tu!
Tatizo mara nyingi tunakuwa na hukumu zetu kabla ya hukumu halali.
Serikali ikishindwa hiyo kesi utaona tunavyowapamba wanasheria wa UKAWA na kuwaita Makanda hatari, wameigalalaza serikali....hadi tutawaita mawakili wa serikali "******"
Kimbembe UKAWA ushindwe kesi, hapo utasoma kila aina ya laana, mara bilioni kumi na mbili za Magufuli ndio zinafanya kazi,mara mahakama zetu haziko huru, mara majaji wa voda Fasta ....ilimradi kuhalalisha kushindwa kwetu.!
Ngoja tuendelee kusoma sarakasi zao.!