CHADEMA wampokea Lijualikali kutoka gereza la Ukonga, atoa ya moyoni

Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.

Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.

Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa ya faini.

Chanzo: Mwananchi

Rejea kuhusu hukumu yake kutenguliwa =>Mahakama Kuu yatengua Hukumu ya Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali




Kweli CHADEMA kiboko mmemutoa kafara Dr. Elly ili mmutoa Lijuakali gerezani. Anyway pumzika kwa amani Dr.
 
Karibu Uraiani Kamanda,mapambano yanaendelea.
Wabaya wako watakiona mara kumi ya waliyokufanyia.
 
PETER Lijualikali, Mbunge wa Kilombero, (Chadema) amesema akiwa mfugwa kwa yake kwa siku 79 katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, aliteswa na kunyimwa haki zake, anaandika Pendo Omary.


Baada ya kutoka gereza la Ukonga amesema “kuishi gerezani unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye busara. Kuna mateso ya kikatili ambayo ambayo wafugwa wanafanyiwa. Kuna wakati niliumwa maralia, daktari akashauri nipumzike. Lakini nilifanyishwa kazi ngumu na kuhatarisha afya yangu.”


“Askari Magereza saikolojia yao bado ipo kikoloni. Nimeshuhudia mtu anapigwa hadi anatambaa. Kuna harassment ambazo nilikuwa nafanyiwa. Nilipigwa sana.


“Gerazani kuna madaraja matatu, daraja la kwanza, la kati na la tatu. Kwa nafasi yangu ya ubunge nilipaswa kuwekwa daraja la kwanza. Ningekufa taifa lingepata hasara kubwa. Lingepoteza zaidi ya bilioni tano kurudia uchaguzi.


“Wakati haya yanafanywa kwa wafugwa wa kawaida, wezi wa meno ya tembo wakiwemo raia wa China wenyewe wanapewa huduma maalum ambazo ni nzuri, tena daraja la kwanza,” amesema Lijualikali.


Lijualikali amesema: “Uhusiano wangu na jeshi kama taasisi ulikuwa mbovu. Lakini uhusiano wangu na askari (mtu mmoja mmoja) haukuwa mbaya sana. Wengine walikuwa wananiambia walitumwa kunifanyia mateso na viongozi wao.”
 
Ashkuru mungu hawamkulawiti maana magereza wanyama sana. Wamewalawiti wale mashekh wa uamsho wallah hawa watu ni majuha sana
 
Tunako elekea ni Kubaya sana,tunafanyiana unyama wenyewe kwa wenyewe,ktk nchi yetu sote.
 
wakati Lijuakali yuko gerezani CHADEMA walimtelekeza hawakuwa na habari nae......habari muhimu kwao ilikuwa ni Makonda
 
hii ni hatari sizonje 2020 yeye Na bashite watakuwa jela upibzanu utakapochukua nch rasmi. what goes around come around
 
Ccm dhambi waliyo ifanya kwa juakali kali wataivuna.

Na juakali asilipize kisasi mungu pekee ndio atakaye mlipa.
 
.....
.....Naamini huko Bungeni na Jimboni utakuwa Mtetezi na Mkomavu na Front line katika kutetea HAKI your are very young HAKI na UKWELI vitakupeleka mbali....

MUNGU ibariki CHADEMA
 
wakati Lijuakali yuko gerezani CHADEMA walimtelekeza hawakuwa na habari nae......habari muhimu kwao ilikuwa ni Makonda
Hapa hujanena vyema jirani! Aliyefanikisha kutoka kwa Peter gerezani ni LISSU wa CHADEMA. MACCM yalimpania vilivyo!
 
Huyu Lijualikali kata very brief .... ngoja nimsaidie

1.Kuna wale wachina wa meno ya tembo waliofungwa miami 30 (majina yao ni Shi ,Yubo na mwingine babu hivi) hao wanakaa PC( Private Cells) hawafanyi kazi yoyote kama ilivyo kwa wafungwa wengine ...Wao sana kazi ya kula mikate tu ya wagonjwa na maziwa na kula wali wa wagonjwa wakati sio wagonjwa... Yaani kwa kifupi ni wafungwa lacinié wanaishi kama wako nyumbani

2.Kuna wafungwa watatu kati ya watano wa ile kesi ya money laundering ya TTCL( majina yao ni Justice Katiti,Mbetwa robert na Gideon Oturo) hawa toka wameingia Jan 2017 gerezani kama wafungwa bwana jela wa Ukonga Ndugu Mwaisabila kawaweka PC(Private Cell) hawafanyi kazi yoyote wao ni kukaa tu na kucheza draft kuanzia asubui mpaka jioni. Ikumbukwe hawa ni wafungwa lakini wanapewa treatment ya ki VIP kuliko hata watu wanavyoweza kudhania...Kuanzia chai ,chakula cha mchana na kadhalika wanaletewa toka nyumbani na wameweka utaratibu chakula kinapokelewa na mahabusu amabao wanaruhusiwa kuletewa chakula toka nyumbani(tena kwa majina wanaopokea chaula cha wafungwa has ni Mohamed Ngumbe na kaka yake na Abdurahman na Ally Mzee).. Tena hawa wajanja sana ,wameamua kujifanya kutoa msaada wa printers kwa ofisi za Magereza Ukonga kama rushwa na mbinu ya kuwalegeza tao watawala wa gereza hilo..kama hamuamini nendeni Ukonga mtakuta hayo ninayoyaandika ambayo Lijualikali kasahau kuyasema.

3.Kuna unyanyasaji mkubwa sana unafanywa na mkuu wa gereza msaidizi Ndugu Haule - yaani huyu ni bora ukutane na shetani kuliko huyu mzee..ana lugha za matusi sana kwa wafungwa ,hana staha kabisa anatukana mpaka ndugu wa wafungwa wanapokuja kuwatembelea siku za weekend..Matusi anayowatolea watu hayaandikiki....ni ya kutisha sanaaaa katika uso wa dunia

4. Kuna vijana askari Magereza wanajiita KM yaani hao kazi yao ni kupiga watu tu ...na matukio Shayo yanapata baraka za mkuu wa gereza na msaidizi wake ...Sawa watu hawa ni wafungwa alakini wana haki zao za msingi sio wanyama wa kupigwa pigwa kama punching bag.. Hata Lijualikali alipigwa sana mitama na hawa KM

Engine yatafuata baadaye -lakini kwa kifupi uongozi wa gereza la Ukonga una upendeleo sana kwa wafungwa wake-kuna watu wanaishi kama wako peponi hawafanyi kazi wakati ni wafungwa na majizi ya kutisha

5.Suala la simu- Kule PC wanakokaa wateule wa Mkuu wa gereza ndio kichaka cha kupigisha simu na ni maaskari hao hao wanaingiza simu hizo gerezani na bina jela anayajua haya yote..hata hivi sasa pale PC wakivamiwa usiku huu zitaokotwa simu hata zaidi ya 15-sasa hili ni gereza au watu wako picnic
 
Kweli CHADEMA kiboko mmemutoa kafara Dr. Elly ili mmutoa Lijuakali gerezani. Anyway pumzika kwa amani Dr.
Mpumbavu kama huyu naye ni mtanzania, acha tutawaliwe na wanyarwanda maana akili zetu hazututoshi.
 
Mpumbavu kama huyu naye ni mtanzania, acha tutawaliwe na wanyarwanda maana akili zetu hazututoshi.
Bilabila ninaoushahidi unaoonyesha kuwa wewe ulishangilia kifo cha Kepteni Komba, kumb mkuki kwa nguruwe
 
Bilabila ninaoushahidi unaoonyesha kuwa wewe ulishangilia kifo cha Kepteni Komba, kumb mkuki kwa nguruwe
Mh! Hili jipya sasa. Ukileta ushahidi wa hili ulilosema kwa kutoa angalau post yangu moja nikishabikia, nalog out jf. Binafsi huwa nahuzunika hata kuku akifa sembuse binadamu mwenzangu???
 
Mh! Hili jipya sasa. Ukileta ushahidi wa hili ulilosema kwa kutoa angalau post yangu moja nikishabikia, nalog out jf. Binafsi huwa nahuzunika hata kuku akifa sembuse binadamu mwenzangu???
Bilabila hivi kwa siasa hizi za kijinga nchini kwetu unadhani watu hawaomeani mabaya- kama Lema kwa hizo alizoita ndoto hukuota k... cha Magu na unajua mara nyingi ndoto ni muendelezo wa mawazo na matamanio ya mchana?
 
JUA.jpg


Mbunge huyo amepokelewa na Viongozi na wanachama wa Chadema wakiongozwa na Frederick Sumaye Pichani


Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.
Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.
Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa masharti ya faini.

Lijualikali atoa ya moyoni
Mshahara wa dhambi ni mauti
 
Back
Top Bottom