CHADEMA Tarime yazidi kubomoka. Wanachama wake mashuhuri wahamia CCM leo, wapokelewa na mwenyekiti wa UVCCM taifa, ndugu Kheri James

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
CHADEMA leo tena imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na wanachama wake mashuhuri ambao walikuwa chachu na nguzo za chama hicho katika wilaya ya Tarime.

Wanachama hao zaidi ya 20 waliongozwa na Leornad Nyankanga, ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Tarime, pia na Frank Chacha, ambaye ni mwanachama aliyefanya operation nyingi ndani ya CHADEMA hapa nchini, na mwaka 2015 alikuwa dereva wa mgombea wao wa urais (Mzee Lowassa) mikoa ya kasikazini na mwanamikakati wa mambo ya siri katika kufanikisha ushindi wa chadema katika chaguzi mbalimbali nchini.

Pia ambaye alikuwa diwani wa kata ya sabasaba (Tarime Mjini), 2010-2015, Ndugu Christopher Chomete pia amejiunga na Chama cha Mapinduzi hivi leo. Abdalah Mahindi (Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwangaza)

Wanachama hao wamepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Kheri James, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ziara yake wilayani Tarime.

NB: Majina na picha za wengine nitawaambia kadri nipokeavyo taarifa toka Tarime.
 
Ingekuwa ni watu wamehamia CHADEMA kesho wangeanza kuona joto la polisi.
 
Serikali wasituone wajinga inamaana CCM ni malaika mikutano yao yote haina intelijensia ya vurugu,inakibali na hawana kauli za kichochezi. Ipo siku inakuja tutawaonyesha sisi sio wajinga tunayajua haya yote. Na mtatamani kurekebisha hamtaweza
 
Serikali wasituone wajinga inamaana CCM ni malaika mikutano yao yote haina intelijensia ya vurugu,inakibali na hawana kauli za kichochezi. Ipo siku inakuja tutawaonyesha sisi sio wajinga tunayajua haya yote. Na mtatamani kurekebisha hamtaweza
Lugha kama hizo unazotumia hapo ndio sababu inawafanya mkose maadili ndio maana mnakimbizwa na marungu kauli zenu mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom