CHADEMA ni kisiwa cha maendeleo na mafanikio kwa vijana

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Ni vigumu kuamini lakini ukweli ni kwamba kama wewe ni kijana na ungependa kupata mafanikio basi chama pekee cha kujiunga ni CHADEMA.

Ndani ya CHADEMA kuna vijana kama Halima Mdee, Mwita Waitara, Sugu, Profesa J, John Heche, Peter Mnyika, Lijuakali, Easter Matiku na wengineo wengi bila kumsahau Zitto aliyewahi kulelewa na CHADEMA.

Sio hivo hata kwa wasanii ambao wana ndoto ya kutimiza malengo yao iwe kisiasa basi ukijiunga na CHADEMA ni lazima ufanikiwe tu kwa namna yoyote.

Lakini baada ya hao wote napenda kumpongeza msanii Wema Sepetu ambae ni moja kati ya wasanii aliyejitoa CCM na kujiunga na CHADEMA akiwa kama kijana lakini nawahakikishieni 2020 Wema ataingia mjengoni akiwa kama mbunge.

Kipindi cha nyuma msanii kama Sugu au Profesa J kipindi wanajiunga na CHADEMA wasanii wengi na watu wengi waliwaponda, mimi nakumbuka hata kuna kituo flani cha redio Sugu alivyochukua fomu ya ubunge waliwahi kumponda. Sio hivo tu bali hata kikundi fulani cha vichekesho kabla hajawa mbunge walishawahi kumuigiza amefulia lakini CHADEMA walimpigania hadi akawa mbunge.

Hivo hivo kwa Wema Sepetu najua kuna watu wengine wasanii sasa hivi wanamponda lakini siku atakapoingia mjengoni na kuitwa mheshimiwa atakuwa sio tena level na hii ndio maana halisia ya maisha.

Kuna kipindi flani msanii kama Masanja Mkandamizaji alishauriwa kujiunga CHADEMA agombee ubunge huko kwao lakini kilichomkuta kura za maoni CCM alipigwa chini. Sio yeye hata Nakaaya sasa hivi angekuwa mbunge ijui ilikuwaje akajitoa CHADEMA lakini leo hii angekuwa mbunge.

Ukweli ni kwamba leo hii CHADEMA imekuwa chama kikubwa mtaani yaani imefikia hatua ukiwa MwanaCHADEMA mtaani na unafahamika au ni kiongozi kuna utawakuta wapo tayari hata kukusomesha yaani ukipata shida CHADEMA hawawezi kukuacha na kukupigania.

Hivo ukweli ni kama wewe ni kijana CHADEMA ndio kisiwa pekee cha mafanikio.

Huu ni ushauri.
 
hayo yote nayatambua ila nilichokuwa najaribu kudadavua kwamba chadema ni chama bora kwa vijanaaa
Nakubali ni chama Bora kwa vijana wenye majina na Umaarufu wao kama Wema na wasanii wengine, wasomi vijana waliokuwa viongozi mavyuoni... na kadhalika,lakini kwa wale makapuku wanzangu na mie.... hao ni madekio bora hata ya wale wanaompiga deki Fulani
 
Reactions: jyn
hahaa unataka niambia umaruufu,elimu, usomi ndio unaweza kukubeba chadema
 
hahaa unataka niambia umaruufu,elimu, usomi ndio unaweza kukubeba chadema
Hoja hapa ni Umaarufu wako tuu.... iwe imeupata kwenye Sanaa, taaluma, uchumi,siasa au kijamii
Chadema kama chama hatua kilipofikia, bado nikutafuta watu wenye msaada kwa Chama, maana bado kiko chini na wanaamini nguvu itapatikana kwa kuwaleta watu wanaoonekana wanaushawishi ktk Jamii, yaani MAARUFU. Ndio sababu MTU mmoja maarufu akihamia CDM ni Habari kubwa na ataenziwa sana. Makapuku hawana chao kabisa wao nafasi yao ni kupiga deki na kuandamana.
Hebu linganisha kupokelewa kwa kina Lowasa, Kingunge, Sumaye, Wema n.k. Usisahau hata mifano iliyotolewa na mleta mada ni majina ya Vijana waliosumbuka kutengeneza majina yao Wenyewe binafsi kisha Chadema ndio ukawapa fursa kisiasa.
So... kama umejipanga nenda Chadema vinginevyo Fanya harakati ila uwe na sifa za ziada kumzidi Mukya
 
ila lakini mkuu unajua kuna watu walijiunga na chadema kama kina mnyika,nassari,lijukali, zitto walijiunga chadema wakiwa makapuku leo lakini huoni kama leo hii ni wabunge
 
Chadema ni chama cha maendeleo na demokrasia japo hakina maendeleo yoyote mwaka wa 26 huu bado kimepanga, pia hakina demokrasia yoyote ndani ya chama kwanini mwanachama yoyote anahaki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama, lakini kwa chadema utaonekana msariti na kufukuzwa kama Zitto kama siyo kutangulia mbele ya haki (r.i.p. Chacha Wangwe)
Isitoshe huwezi kutubutu kuhoji chochote ndani ya chama kinachofanywa na viongozi au matumizi za fedha za chama.
Mbaya zaidi mwenyekiti anaweza kujiamulia maamuzi makubwa ndani ya chama na kutangulia bila idhini ya mikutano mkuu.
ukiwa kiongozi wa chama usijisahau kwani ulipata matatizo japo uko kwenye majukumu ya chama hutapata msaada wowote na train haitakusubiri itaendelea na safari yake.
Haya ni mchache tu ya chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA
 
mkuu hayo yote ni maneno hapa tunakizungumzia ni mafanikio ambayo kijana atayapata baada ya kujiunga na chademaa
 
Duuuh endelea kuota mafanikio Chadema utaishia kusubiria Meri airport,

Wanasiasa ni wanafiki sana kisichompa tija yeye kwako haina masilah kwamwe hutakuja waona wakishikamana kujadili mambo ya msingi ya mafanikio ya wengine na umma kwa ujumla.

Ukitaka fahamu hayo kaulizie matumizi ya ruzuku chadema ama mapato ya chama na matumizi yake ndo utagundua hayo mafanikio unayo yaota.

Ivi Ben Saanane Leo hawaonesh uthubutu kumtafta wapo kimya utadhan amepotea nobody kwenye chama kweli??

Kamanda mawazo alivyo vunjika Mguu kwenye operation sangara huko kanda ya ziwa wakamchunia kimyaaa kateseka kujitibu alone alipofariki wakaenda na v8 zao wakijua watapata kiki,
Mhere mpaka kathubutu kuuza kiwanja chake kwa mahtaji ya mil3 kweli??

Kaa usubirie mafanikio Chadema
 
Nakumbuka Nakaaya Sumari alisema kosa kubwa ambalo amelifanya na analijutia na atalijutia maisha yake yote ni kitendo cha kuondoka Chadema na kuingia CCM.

Saa hii angekuwa mbali sana kisiasa, aling'aa sana Nakaaya. Naamini angekuwa tayari mbunge by now. Kujitoa Chadema na kwenda CCM au vyama vingine ni kujichimbia kaburi kisiasa. Wengi waliofanya hivyo wapo kwenye majuto makubwa.
 
Ni kweli kabisa, kwani no chama cha kutetea wapigaji, wala rushwa na hata wauzaji, wasambajazi na walaji wa ule unga. Shime jiungeni vijana!
 

sosopi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…