CHADEMA mrudisheni Dr.Slaa kundini mtengamae

Naomba nikuulize, hivi ingetokea slaa amefariki ungetoa huu ushauri? Nimekuuliza hivyo ili ujue tunahitaji kujiondoa ktk misingi ya kutegemea umaarufu wa watu kwani hufa na kupotea!!

CCM Leo akina Nyerere hawapo lkn kila siku wanazaliwa watu wapya!!

CDM nayo inaelekea huko... Wengine watakufa wengine watazaliwa huo ndio msingi imara wa chama komavu!!
Angekufaa bado tungemkubuka kwa ideas zake,ingawa asingekuwa msaada kwenye battle ground,....ila unaposema misingi ya umaarufu inategemea umaarufu gani,maana hata huyo aliyekuwa upande wa pili umaarufu wake ndo uliomfanya asimamishwe kuwa mgombea huku kwetu,mkuu mbali na mikiki ya uchaguzi iliyopita challenge gani huyu wa UKAWA tuliyemsimamisha akaleta kwa sasa?maana hata uzito wake umepungua kwenye media?unakumbuka maandamano aliyofanya Dr ?kilichomwokoa mkwere ni scandal ya mzee wa loliondo
 
Nikiingia kwenye details baada ya kuainisha unafiki wako,moja ya badiliko kubwa ambalo nchi hii inalihitaji ni kumkomboa mtanzania kifikra na kufanya reform kubwa kwenye mfumo wetu wa elimu ili profesa asiwe anafikiria kama mtoto wa darasa la pili.
pili,kupunguza ukubwa wa serikali na matumizi yasiyo lazima.Hapa ni kufutilia mbali wakuu wa wilaya ambao kimsingi majukumu yao yanaweza kuhamishiwa kwa mkurugenzi wa halmashauri.Kufuta mbio za mwenge.Pamoja na kubana matumizi anakotuonesha Magu,bajeti ya mwaka huu inaonesha mapato yote ya ndani hayafikii matumizi ya kawaida ya serikali.Ina maana shughuli za maendeleo zitaendeshwa kwa mikopo na misaada.
Tatu,katiba ya wananchi itakayoweka misingi ya uongozi.
nne;Reform ya jeshi na usalama baada ya kuonekana kupwaya na kutowajibika
tano;Huduma kwa jamii pamoja na miundombinu imara zaidi

Mambo ni mengi,sio kutumbua majipu peke yake.
Mkuu hayo mabadiliko unayahitaji chini ya Magufuli au UKAWA ?
 
...mimi nakushauri tu uwe unajipanga vizuri kabla ya kuleta uzi hapa,sio kila wazo la kukurupuka,ni lakuanzishia mada,umeulizwa maswali unashindwa kujibu,na wewe unajibu kwa kuuliza swali,bwege kweli!
 
Nakubaliana na ulichokisema mkuu .
CDM ya sasa sio ile ya mwaka juzi.
Huyu katibu mkuu mpya sijui anafanya nini ??
Yuko kimya mno .
 
Hii nchi ina safari ndefu sana kufikia mafanikio kamwe anayoyafanya Magufuli hayatufikishi upi mkakati wake juu ya madini,maliasili,Miundombinu (reli) nini hatima ya elimu na afya Magufuli atuonyeshe upi mpango kazi wake juu ya mambo muhimu kwa taifa. Kuhusu CHADEMA sidhani kama wanatishwa na Kinachoendelea naamini bado ni wa pinzani wa kweli nangoja kushuhudia wakiibana serikali.....Udhaifu wa Mrisho unamfanya John aonekane Mwamba..
 
...source ya huu uzi ni uzi mwingine uliopoko huku wa Dr Slaa sijui kanasa nyaraka,ndio kichwa maji akakurupuka kuja kuanzisha huu uzi wake.
Taasisi imara siku zote hujengwa kwa misingi,haijengwi kwa nyaraka za kupewa,wala haijengwi kwa kuuza sura kila siku kwenye tv,siku ikikosa hizo nyaraka taasisi yako itakufa!
 
kifo cha slaa,mwanzo wa shujaa mpya.amefanya kwa kipindi chake inatosha wengine wataendeleza.hakuna marefu yasiyokuwa ncha
 
Huyu jamaa kaisha MWENZIE LIPUMBA kaamua kufanya utafiti aliwekeza fedha alizo jipatia yy alizani lie ni SADAKA ataendelea kukinga kumbe ONE MOMENT GAME sasa wife anachukua MIKOPO na BENK WANAUZA NYUMBA no woman no cry
Ila na CCM nadhani WAMRUDISHE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU
 
Huyu jamaa kaisha MWENZIE LIPUMBA kaamua kufanya utafiti aliwekeza fedha alizo jipatia yy alizani lie ni SADAKA ataendelea kukinga kumbe ONE MOMENT GAME sasa wife anachukua MIKOPO na BENK WANAUZA NYUMBA no woman no cry
Ila na CCM nadhani WAMRUDISHE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU
Mkuu sadaka inahusiana nini na hoja?we unajua account yake ya bank?we ukienda kanisani au msikitini hutoi sadaka?jikite kwenye hoja!hayo mengine ni kuonyesha ufinyu wa mawazo au kuonyesha akili yako ilipogota
 
Hii nchi ina safari ndefu sana kufikia mafanikio kamwe anayoyafanya Magufuli hayatufikishi upi mkakati wake juu ya madini,maliasili,Miundombinu (reli) nini hatima ya elimu na afya Magufuli atuonyeshe upi mpango kazi wake juu ya mambo muhimu kwa taifa. Kuhusu CHADEMA sidhani kama wanatishwa na Kinachoendelea naamini bado ni wa pinzani wa kweli nangoja kushuhudia wakiibana serikali.....Udhaifu wa Mrisho unamfanya John aonekane Mwamba..
Mkuu CHADEMA ni wapinzani sikatai,wanakauli za kuishawishi serikali ya Magufuli kuondoa ufisadi?CHADEMA ni smart ila sungura mjanja kanasa tundu mbovu,wafuasi wa CHADEMA wanajua Dr Slaa alikuwa mpambanaji,CHADEMA walisemama kwa kauli moja kumpinga Lowasa Leo Slaa kukataa unafki akajitoa CHADEMA halafu MTU CHADEMA walikuwa wanamponda ndo akagombea urais kwamba ndo bora,?

je kama Lowasa hakuwa mchafu CHADEMA data zao na facts walikuwa wanazitoa wapi?

C.c
Mzee Mwanakijiji
 
Ni vigumu sana kuiuza CCM,si unaona mpaka wewe unasahau unatumia magufuli badala ya ccm.Ndipo tatizo lilipo,mfumo wa ccm umeoza na hatutafika kokote kwa kumtegemea Magufuli tu.
CCM inajulikana,je Magufuli anaangalia maslahi ya chama au nchi?
 
CCM inajulikana,je Magufuli anaangalia maslahi ya chama au nchi?

ccm inajulikanaje?Unaweza ukawa unaangalia maslahi ya nchi lakini kwa namna ambayo si efficient,unazungukwa na wezi ambao sasa wameinamisha vichwa chini kukutii kwasababu wanaujua msimamo wako,ukiwapa mgongo wakapata mwanya wanapiga deal.Hapo ndio kwenye tatizo,maendeleo yataendelea kuwa ya kuchechemea.Magufuli amezungukwa na wezi na matapeli waliokubuhu ambao wanajifanya wameamka na kuacha.Anayofanya magufuli ni mazuri lakini ni sehemu ndogo sana ya mabadiliko tuliyotarajia.
 
Back
Top Bottom