CCM yawageukia Chenge, mawaziri yawataka watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wote waliotajwa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini, kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola vitakavyowahoji.



Waliotajwa katika ripoti ya pili ni aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Profesa Sospeter Muhongo na na Nazir Karamagi.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi) katika ofisi za Lumumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema ili vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa haraka na ufanisi, waliotajwa wanapaswa kutoa ushirikiano.

Polepole amesema chama hicho chenye Serikali kinaviagiza vyombo vya dola kuwahoji waliohusika kwa haraka ili Watanzania wajue ukweli wa yaliyotokea.

Amempongeza Rais John Magufuli kwa kuthubutu kudai rasilimali ambazo zimekuwa zikiibiwa.

Pia, amewataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anayoifanya badala ya kugawanyika.

Chanzo: Mwananchi
 
Natamani siku nishuhudie mpambano wa chenge na masaju pale kisutu!
Ila najua tu kuna mmoja kati yao hata tukimbebea mtutu wa bunduki hatakubali.....
 
So muwavue uanachama kwanza ili vyombo vya dola viwashughulikie kwa Uhuru zaidi!
 
Hivi katika kujumuisha majina hayo ya viongozi wa serikali kwenye taarifa ya pili ya makinikia, mwenyekiti wa kamati hiyo, Prof. Ossoro hakushauriana kweli na mhe. Rais Dr Magufuli? Halafu hiyo kinga ya kikatiba ikiondolewa nafikiri mkuu wa nchi atakuwa makini zaidi na more rational katika maamuzi na masual yote ya nchi kwa maslahi ya wenyenchi.
 
Mbuzi wa BWANA HERI amekula mahindi ya BWANA HERI,, Halafu hili jukwaa huwa nashangaa sana ni tofauti sana na majukwaa mengine kwa nini watu wengi huwa wanaandika point sana lakini huwa hamuwapatii hata like?? Maana yake ni nini?? Badilikeni hili Jukwaa
 
waende tu maana majibu watakayojibu ni rahisi
wote watajibu walitekeleza maamuzi ya mabosi wao
wakienda kwa mabosi wameshaambiwa wasiguswe waachwe walale usingizi na biashara inaishia hapo hapo
 
Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu
 
my foot!
watafanya usanii kama ule walioufanya kwa Mramba na Yona.
jamaa walikuwa saa zote wapo kitaa wanakula bata eti tunadanganywa wako Segerea!
 
Bosi mwenyewe kampokea mtuhumiwa pale magogoni, cha ajabu badala ya kumkamata, akamkorogea kahawa, kajibaraguza kwa kiingereza cha Ras Simba, kamfungulia geti, pua ndefu (mtuhumiwa) kapiga moto jet huyoooo kasepa! Ninyi huku nyuma maneno kibao kama viwete! Wenye akili tumejua hili limeshapita!
 
Nasikia huko nyumbani Chenge kashaunguruma,anasema yeye alisaini mikataba kwa maelekezo ya wakubwa,kama vile fulani alivyokubali kuuza nyumba za serikali kwa maagizo ya mkubwa wake,yeye pia alisaini hiyo mikataba kwa maagizo ya mkubwa wake.

Mmoja aliagizwa kutekeleza wajibu wake wa kusaini mikataba ya madini,na mwingine alitekeleza wajibu wa kuuza nyumba za serikali.Andrew hawezi kusaini mikataba mikubwa hivyo bila uhakika wa "Security" ya baadae.

Polepole akumbuke nafasi hiyo ilikuwa kwa Nape,alijikakamua kuwavua "magamba" kina Chenge na Rostam,lakini mambo yalidunda,sijui safari hii yeye ataweza kuileta CCM mpya?Chenge ana mahali kajishikilia,hapo mahali ndio jana Rais JPM kaagiza "pasiguswe" wala pasiandikwe magazetini.
 
Haya wakihojiwa wakasema kila walichofanya kina baraka ya viongozi wao wakuu ama waheshimiwa mtafanyaje?


Sasa si muanze kwa kuwavua uanachama?

Haki ya mama kesi Chenge hamumkamati.. Nimeamini Tanzania kuna ma Godfather kama kina Corleone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…