CCM wilaya ya Musoma Mjini yaagiza kurudishwa kwa Mkurugenzi wa manispaa hiyo Dr. Khalfan Haule

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,633
2,297
CCM wilaya ya Musoma Mjini imeomba Mheshimiwa Rais, amchukulie hatua na kumrudisha mkuu wa wilaya ya sumbawanga Dr. Khalfan haule ambae alikuwa ni mkurugenzi wa manispaa Musoma kwa kuwepo Saccos hewa ya vijana, na mradi mbovu wa barabara ya lami ya km. 2.64 uliogharimu tsh 3.3 billion ambao hukupokelewa kama utekelezaji wa ilani ya CCM
 
Arudishwe kujibu tuhuma zinazomkabili, na achukuliwe hatua za kinidhamu
 
Hebu tulia uandike vizuri Kwani unawahi nini?
 
Hawa ndio wale wateule tuliombiwa mh.alichukua muda mrefu kujiridhisha kama wanafaa.
 
Wamwache apige kazi, make waziri wa ujenzi kipindi hicho ni mkulu wa nchi bado anamwamini.
 
hayo ni miongoni mwa niliyosema kwamba miaka hii mitano itakuwa ya kuona na kusikia mengi ya ajabu
 

Ujambazi ndo kigezo cha promotion CCM
 
Mamlaka yenye uadilifu usio na shaka na yenye kutenda haki kwa 100% ni MWENYEZI MUNGU pekee.
 
Ma CCMijizi bana.
Akili hamna kabisa.
Sasa arudishweje ?,Kwa basi ana kwa Ndege ?
Then akisharudishwa kama CCMijizi Mkoa wa Musoma mtamfanya nini ?
Mkimhoji then what Next ???
Yaan utendaji kazi wa Mkurugenzi taarifa inapelekwa kwa CCMijizi ????
What a shame
 
Hawa ndio wale wateule tuliombiwa mh.alichukua muda mrefu kujiridhisha kama wanafaa.
Jamaa aliteuliwa kwa kulipa fadhira za kufanikisha uingizwaji wa kura feki kwa Musoma mjini, vijijini na Butiama ili kufanikisha ushindi wa Mkulu, wabunge na madiwani.
 
Hivi USALAMA WA Taifa hawakujua ufisadi WA huyu bwana? Au KAZI yako kukamata wanao hoji kama Mimi?
 
Kwa nini kila kitu ni MAGUFURI tu??.
yeye hana wasaidizi?.
Binafsi nimeshaanza kumuonea huruma maana ukimuona ana dhamira ya kweli ya kuwasaidia watanzania ila tatizo ni wasaidizi wake,mf kwa jambo kama hili TAKUKURU,POLISI,TANROAD MKOA NA MKUU WA MKOA hawapo kushughulikia suala kama hili?
 
Nadhani wewe una visa binafsi na Dr. Haule maana kila mara unatafuta jambo baya la kumsema vibaya huyu jamaa sijajua unapata masilahi gani na zaidi sana nakuona kama una tabia za kike vile maana kati ya halmashauri zaidi ya 70 ambazo nimeshafanya kazi mbalimbali za maendeleo Dr. Haule ni mojawapo ya wakurugenzi wastaarabu niliowahi kukutana nao hivyo nakushauri UACHE MAJUNGU NA UMBEYA FANYAKAZI NA UJENGE TAIFA LAKO umemuonea sana huyu jamaa na amekuwa kimya muda wote lakini waungwana lazima tuseme ukweli juu yake.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…