CCM Moshi Vijijini yamlipua Mbatia

charles ndagulla

Senior Member
Feb 18, 2016
168
110
Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Vijijini kimetoa taarifa ndefu kikiishutumu Taasisi ya Vunjo Development Foundation (VDF) ambayo Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Bwana James Mbatia ni mmoja wa viongozi waanzilishi na ndiye Katibu, kwa tuhuma mbalimbali, ikitaka VDF ichunguzwe kama inajihusisha na utakatishaji wa fedha.

Ripoti hiyo imezungumzia tuhuma nyingine mbalimbali. Pamoja na andiko hili, naambatanisha taarifa hiyo ya CCM kwa ajili ya kuibua mjadala.

Naomba kuwasilisha.
......................................................................................................................................................................................................

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI
S.L.P 541, MOSHI – KILIMANJARO

TAARIFA KWA UMMA SIKU YA JUMANNE,
TAREHE 18/12/2018.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mkutano wa hadhara uliofanywa na mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. JAMES FRANSIS MBATIA tarehe 25/11/2018, Kata ya Makuyuni – jimbo la Vunjo.

Ufafanuzi kuhusu upotoshwaji uliofanywa na Asasi isiyo ya Serikali ijulikanyo Vunjo Development Foundation (VDF):

1. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaitaka Asasi hii ijulikanayo Vunjo Development Foundation (VDF) iache kutumika kisiasa hasa kutokana na tabia na mienendo ya shughuli zake za kila siku ambazo ni kinyume na katiba yake.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaitaka Vunjo Development Foundation (VDF) itamke wazi kwa kuzithibitishia mamlaka za serikali na vyombo vyake ilianza na kiasi gani cha fedha katika akaunti yake na bajeti nzima ya mradi wa barabara za moramu kwa Jimbo la Vunjo ni kiasi gani. Pia, VDF itamke ilitarajia wananchi wa jimbo la vunjo wachangie kiasi gani. Kwa kufanya hivyo itaondoa uwezekano mkubwa wa Asasi ya VDF kutumika katika vitendo vya utakatishaji fedha (Money laundering) hasa kutokana na kumekuwapo na vitendo vingi vya taasisi zisizo za kiserikali kujihusisha na kutumika katika vitendo vya utakatishaji wa fedha.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaitaka Serikali kuichunguza taasisi ya VDF katika hili la utakatishaji fedha (MONEY LAUNDERING) ili kuweza kuondoa hisia hasi iliyopo kwa sasa.

2. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kimejiridhisha vya kutosha kuwa Serikali yetu chini ya MHE. Rais DKT. JOHN P. MAGUFULI kupitia Mkuu wa Wilaya ya Moshi haijakataa kushirikiana na Asasi hii ya VDF katika kuleta maendeleo ya kweli katika Jimbo la Vunjo jambo la msingi ni lazima taratibu, kanuni na sheria za nchi zifuatwe na kuheshimika na asasi hiyo.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kina mashaka na taswira ya jinsi asasi hii inavyofanya shughuli zake, kwani asasi hii imekuwa ikifanya shughuli za kukusanya michango kwa wananchi pasipo kupata kibali (uhalali) kutoka serikalini kinyume na sheria.

Asasi hii pia, imekuwa ikifanya uharibifu mkubwa wa mazingira hasa ukataji ovyo wa miti pamoja na kuharibu mali za wananchi. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi kama walivyoeleza kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Moshi Vijijini iliyofanyika kuanzia tarehe 08/02/2018 – 14/07/2018 na pia kwenye ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya iliyofanyika tarehe 08/11/2018 – 03/12/2018. Wananchi wengi wamekuwa hawakubaliani na namna zoezi hili la ukusanyaji fedha linavyoendeshwa na asasi hii ya VDF kwani imekuwa ikifanya vitendo vya kikatili kwa wananchi vya KUWABAMBUA mali zao wananchi ambao wamekuwa wakikataa au kushindwa kuchangia pesa.

Neno “kubambua” ni kitendo cha kuchukua kwa nguvu bila ridhaa ya mwenye mali kama vile mifugo au kitu chochote cha thamani kisha kuuza ili kulipia kiasi kilichowekwa.

3. Kutokana na vitendo vilivyofanywa na asasi hiyo vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupelekea hatari ya uvunjifu wa amani, serikali ya wilaya kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliamua kuingilia kati jambo hilo na kusitisha zoezi la uchangishaji huo wa fedha. Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaipongeza serikali kwa uamuzi huo ambao ulilenga kuirejesha katika meza ya mazungumzo baina ya taasisi hiyo ya VDF na serikali. Tunaamini lengo la Mkuu wa Wilaya ya Moshi / Serikali ni kuweka utulivu na amani kwa wananchi ambao wamekuwa wakiilalamikia serikali kutoingilia kati suala hilo.

4. Asasi hii ya VDF mbali na kutakiwa kufika katika meza ya mazungumzo, haikufanya hivyo badala yake iliamua kumfungulia kesi tatu (03) Mkuu wa Wilaya ya Moshi. Kesi zote zimefunguliwa katika mahakama kuu ya kanda ya Dar es salaam akishtakiwa kama Mkuu wa Wilaya na nyingine ni kutoka kanda ya Moshi akilengwa binafsi kama Kippi Warioba, kwa kuwa tunaamini katika Utawala wa sheria tunaiachia Mahakama jambo hili kwa kuwa hatutalizungumzia kwa kina kuepuka kuingilia kazi ya Mahakama.

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaitaka asasi hii inayojiita VDF ijitathmini kama dhamira yao ni njema katika Wilaya hii ya Moshi hususani Jimbo la Vunjo.

5. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinatoa masikitiko makubwa juu ya upotoshaji uliofanywa na Mh.

Mbunge JAMES F. MBATIA kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika tarehe 25/11/2018 kwenye viwanja vya Makuyuni kwa kudai kuwa asasi hii ya VDF ina wajibu (Majukumu) sawa na TARURA au TANROADS na kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi imechoka na haina uwezo wa kuwatengezea wananchi wake barabara.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinamkumbusha MH. MBUNGE kwamba TANROADS na TARURA hizi ni taasisi za serikali na zimepewa mamlaka kamili ya kikatiba na sheria za nchi na sio VDF juu ya ukarabati na ujenzi wa barabara katika nchi hii. Hivyo basi, shughuli zote zinazofanywa na asasi hii ya VDF si halali kabisa. Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinataka MH. MBUNGE aache kupotosha wananchi katika kuhalalisha asasi yake ya VDF kuwa ina uwezo wa kufanya lolote sawa na TARURA, TANROADS na Serikali yake.

Wananchi wanajua kuwa TARURA ina vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo kutoka kwenye bidhaa au huduma itakayokuwa inatoa, ruzuku ya Serikali, bodi ya barabara , mikopo na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo, Sekta binafsi (PPP), Ushuru wa maegesho, tozo la msafiri, ada ya kutumia hifadhi ya barabara n.k.

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaitaka VDF ijikite kama mdau wa maendeleo. Jambo hili sio geni katika nchi yetu kwani NCHI YETU imekuwa ikipokea misaada mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya huduma za wananchi zikiwemo barabara, afya, elimu n.k.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinahoji nia ya asasi hii ya VDF kukataa kukaa meza moja na Serikali ya eneo husika ikiwa nafasi hiyo wamepewa ?

Mashaka yetu makubwa dhidi ya asasi hii ni uwezekano wa kutumika kisiasa. Ifahamike kuwa Katibu wa VDF ni Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI (T) na Mbunge wa Jimbo la Vunjo (NCCR). Hili linatoa hisia hasi, hasa ikizangatia tamko la asasi hii ya VDF walilolitoa kupitia kwa wakili wa kujitegemea Ndg. HAROLD SUNGUSIA kumfungulia mashitaka Mkuu wa Wilaya ya Moshi MHE. KIPPI WARIOBA lilifanyika katika ofisi ya chama cha siasa cha NCCR Mageuzi jimbo la VUNJO. Uhalali wa asasi hii ya VDF kufanyia shughuli zake katika Ofisi ya Chama cha siasa (NCCR Mageuzi) unatoka wapi?.

Rai ya Chama Cha Mapinduzi kwa Serikali:-

1. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaiomba Serikali kupitia vyombo vyake ichunguze maudhui ya asasi hii uhalali kama ilivyosajiliwa na ichukuliwe hatua za kisheria endapo itabainika kukiuka taratibu na katiba yake.

2. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA VIJIJINI kinaiomba Serikali wakati inaendelea kujiridhisha na uhalali wake na mwenendo wake isitishe utendaji wa shughuli zake zote katika Wilaya hii ya MOSHI mpaka ijiridhishe.

3. Kwa kuwa VDF imekusanya fedha za wananchi pasipokuwa na kibali kutoka Serikalini na kwa kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika kupitia mikutano mbalimbali wakishurutishwa kuchangia hizo fedha na wasipofanya hivyo wanabambuliwa tunaitaka Serikali ichukue hatua za kisheria kuhusu asasi hii ikiwemo pesa zote zilizokusanywa kutoka kwa wananchi kurejeshewa wahusika haraka iwezekanavyo.

4. Kwa kuwa VDF imekuwa ikijihusisha na shughuli za ujenzi wa barabara kama ilivyo kwa makampuni mengine ya ujenzi, tunaitaka serikali kupitia TRA waichunguze asasi hii ya VDF kama wana “TIN NUMBER” na kama wanalipa kodi ya serikali kama makampuni mengine ya ujenzi yanavyofanya.

Kuhusu fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo (CDCF) - Vunjo:
Sheria ya mfuko wa maendeleo ya jimbo (The constituencies Development Catalyst Fund Act. Na. 16 ya mwaka 2009) ilitungwa Julai mwaka 2009 na kusainiwa na MHE. RAIS, August 21 mwaka huo kwa lengo la kuchochea maendeleo jimboni ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo hufanyika kwa juhudi za wananchi wakishirikiana na mbunge wao, pamoja na serikali kuu kama mchochezi mkuu anayetoa pesa.

Ifahamike kuwa kamati ya mgawanyo wa fedha hizi za mfuko wa jimbo, Mbunge ni mwenyekiti na Afisa Mipango wa Halmashauri ni Katibu.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kimejiridhisha vya kutosha kuwa mbunge wa jimbo la vunjo MHE. JAMES MBATIA anatumia fedha za mfuko wa jimbo la vunjo kwa upendeleo kwa maslahi yake binafsi.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinahoji mgawanyo wa fedha za mfuko wa jimbo la Vunjo ambazo ni shilingi milioni 45,908,878/= namna zilivyopangiwa matumizi yake hivi karibuni kwenye vikao halali ambacho Mwenyekiti wake ni mbunge JAMES FRANSIS MBATIA.

Katika mgawanyo huu wa pesa kata ya Marangu Mashariki pekee imetengewa shilingi milion 30 kati ya hizo milion 45, kata ya makuyuni imetengewa milion 5 na shilingi milion 10 bado hazijapangiwa matumizi yoyote.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinamtaka Mh. Mbunge JAMES MBATIA awaeleze wananchi wote wa jimbo la vunjo lenye jumla ya kata 16 ambazo zina haki ya kunufaika na fedha za mfuko wa jimbo, ikizingatiwa kuwa maeneo mengi ya jimbo la Vunjo miradi mingi imesimama kwakukosa fedha ni kigezo gani kilitumika kutoa robo tatu ya pesa zote kutumika sehemu moja kama sio kuwabagua na kuwatenga wananchi wa kata nyingine. Na kwa taaarifa tulizonazo pesa hizo zinatarajiwa kuelekezwa katika asasi yake binafsi ya VUNJO DEVELOPMENT FOUNDATION (VDF).

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinataka wananchi wote wa Jimbo la Vunjo kuhoji fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo la Vunjo matumizi yake na mgawanyo wake katika maeneo yao.

Kuhusu mgogoro wa Shamba la Lokolova:
Mgogoro wa kugombea ardhi ya shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,470 lililopo kata ya Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa. Mgogoro huu unahusisha Chama cha ushirika na jamii ya wafugaji katika eneo hilo.

Mbali na eneo hili kuwa na mgogoro mbunge wa jimbo la Vunjo MHE. JAMES MBATIA kwa kutumia nafasi yake ya ubunge alifanya hila chafu za kujipatia ardhi yenye ukubwa wa ekari 25 ndani ya ekari hizo 2,470 za ardhi ya Lokolova.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinataka wananchi wafahamu suala hilo na wamfahamu aina ya mbunge ambaye wanaye.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini tunaishukuru serikali kwa kuzuia hati ya ardhi ambayo mbunge amekuwa akijaribu kila mbinu za kutaka kupatiwa hati hiyo ya ardhi.

Ufafanuzi kuhusu mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo kutoshiriki mkutano wa hadhara na kuwa sehemu ya kikwazo kwa mbunge katika kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.

Chama Cha Mapinduzi kinapenda ieleweke ya kwamba madai yote aliyoyatoa MH. Mbunge JAMES F. MBATIA dhidi ya Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Himo sio ya kweli. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI katika madai haya yanayotolewa na Mh. Mbunge imejiridhisha yafuatayo:-

1. Kauli za mbunge kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika tarehe 25/11/2018 kata ya makuyuni, zinakiri kwamba mikutano yote ya kimaendeleo aliyowahi kuitisha mbunge, ilihudhuriwa na mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo na aliweza kutoa mawazo mbadala ya kujenga maendeleo katika Jimbo.

2. Hakuna mahali ambapo Mh. Mbunge ameweza kuthibitisha kwa vielelezo kuwa Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo amekuwa ni kikwazo katika maendeleo ya Jimbo la Vunjo kama alivyodai katika mkutano wake wa hadhara aliouitisha.
KUTOKANA NA KUJIRIDHISHA HUKU:

1. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinataka kuwathibitishia wananchi wote wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo na Jimbo la Vunjo kwa ujumla hakuna taarifa yoyote ya mwaliko aliyopewa Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo ya kumjulisha na kumwalika kuhudhuria katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika eneo lake siku ya jumapili tarehe 25/11/2018.

2. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinahoji uhalali wa mbunge JAMES FRANSIS MBATIA kumsema na kumkosoa Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Himo ambaye anatokana na Chama Cha Mapinduzi kuwa ni kikwazo kwa maendeleo kwa sababu tu ya kutohudhuria mkutano wake wa hadhara ambao hakupewa mwaliko?

3. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinamtaka Mh. Mbunge aonyeshe kwa vitendo kama ana dhamira ya kweli ya kutaka kushirikiana na mwenyekiti wetu wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo. Hususani kwa nini Mh. Mbunge amekuwa akikataa kuhudhuria kwa makusudi kabisa vikao mbalimbali vya mamlaka ya mji mdogo wa Himo vinavyohusu maendeleo huku ofisi yake ikiwa inapewa taarifa rasmi na mwaliko kwa mbunge kuhudhuria vikao hivyo?
Ushauri wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kwa Mbunge:

1. Chama Cha Mapinduzi kinamtaka MH. MBUNGE kutimiza wajibu wake kama kiongozi na mbunge kwa mujibu sheria na taratibu zilizopo.
2. Chama Cha Mapinduzi kinamtaka MH. MBUNGE aache kutoa visingizio visivyo na mashiko ili kutaka huruma ya wananchi.
3. Chama Cha Mapinduzi kinamtaka MH. MBUNGE aache mara moja tabia ya kuchonganisha wananchi na viongozi wao kama mtaji wake wa kisiasa.

MWISHO

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaomba wananchi wa Jimbo la Vunjo waendelee kuwa na Imani na Serikali yao inayoongozwa na Mhe John Pombe Magufuli kuwa Serikali hii ambayo mbunge anaituhumu kuwa haina uwezo wa kujenga barabara ndio serikali iliyojenga barabara zote za lami zilizopo katika Jimbo la Vunjo zenye thamani ya mabilioni ya pesa.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinamtaka MH. Mbunge JAMES MBATIA aache kutafuta wa kumlaumu kwani kushindwa kwake kuleta maendeleo katika Jimbo la VUNJO kunatokana na kushindwa kwake kuwa mwakilishi mzuri ndani na nje ya Bunge kwani imekuwa ni desturi kwake kususia bajeti za maendeleo za Serikali ndani ya Bunge. Ni vema Mh. Mbunge akawa na hofu ya Mungu kwa kila jambo analolitenda kwani kwa kufanya hivyo kutamfanya awe mkweli na mpenda maendeleo wa kweli na bila unafiki.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kilitamani leo Mh. Mbunge aje na maelezo ya kina juu kero mbalimbali ambazo kwa mda mrefu sana zimekosa majawabu yake. Awaeleze wananchi wake ni kwa kiasi gani ameweza kushirikiana na Serikali iliyopo madarakani ya CCM katika kuhakikisha huduma mbalimbali zimeboreka mathalani changamoto za afya, mindombinu ya shule, utatuzi wa migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji n.k.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaamini kwamba maendeleo yanapiga kelele sana kuliko maneno. Sio siri kwa kipindi chote cha uongozi wa Mh. Mbunge maendeleo mengi yamesimama hasa kutokana na uwajibikaji mbaya wake. Ni kweli usiopingika Jimbo la Vunjo linapitia wakati mgumu sana kipindi chake. Ni vema wananchi wa Jimbo la Vunjo wakatathmini juu ya mwenendo wa mbunge wao kama kuna haja ya kumpa nafasi tena ya miaka mitano ijayo ya maumivu.
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kimefatilia kwa uzito wake kauli ya Mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. JAMES MBATIA kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika terehe 25/11/2018 siku ya jumapili. MHE. JAMES MBATIA aliwatangazia wananchi wa Jimbo la Vunjo kuwa MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA atakuja Vunjo kwa ajili ya kufungua barabara za moramu. Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini tumeiuliza serikali juu ya kauli hiyo ya Mbunge MHE. JAMES MBATIA kuhusu ujio wa MHE. RAIS ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro, tumejibiwa hakuna taarifa yoyote ile hadi sasa ya ujio wa MHE. RAIS katika Mkoa wa Kilimanjaro hususani jimbo la Vunjo.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kimejiridhisha vya kutosha kuwa MHE. Mbunge JAMES MBATIA anawapotosha wananchi wa Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kwa makusudi kabisa kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaitaka serikali katika Mkoa wetu wa Kilimanjaro imtake Mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. JAMES FRANSIS MBATIA afute kauli yake mara moja kwani yeye si msemaji wa Serikali katika Mkoa wa Kilimanjaro, tofauti na hapo tutapata mashaka sana juu ya kauli zake hizi ambazo zinaingilia moja kwa moja mamlaka ya Serikali katika Mkoa wetu wa Kilimanjaro.

Mwisho kabisa, Tunapoelekea mwisho wa mwaka, Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinawatakia wananchi wote wa Wilaya ya Moshi Vijijini sikukuu njema ya CHRISTMASS na heri ya mwaka mpya 2019, msherehekee kwa amani na upendo.

Imetolewa na:-
Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Moshi Vijijini
 
Attachments

  • TAARIFA RASMI YA CCM.doc
    66.5 KB · Views: 36
Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Vijijini kimetoa taarifa ndefu kikiishutumu Taasisi ya Vunjo Development Foundation (VDF) ambayo Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Bwana James Mbatia ni mmoja wa viongozi waanzilishi na ndiye Katibu, kwa tuhuma mbalimbali, ikitaka VDF ichunguzwe kama inajihusisha na utakatishaji wa fedha. Ripoti hiyo imezungumzia tuhuma nyingine mbalimbali. Pamoja na andiko hili, naambatanisha taarifa hiyo ya CCM kwa ajili ya kuibua mjadala.
Naomba kuwasilisha
Naked 'conspiracy'
 
Tumechoka kusoma taarifa zao uchwara,kama Mbatia anafanya ufisadi kwenye hiyo VDF milango ya mahakama ipo wazi wakafungue shauri,na mkuu wa nchi alishasema ameunda mahakama ya mafisadi.
Mm nawaona wachumia tumbo tu!!
 
M.kiti wa ccm wilaya ya moshi yeye ndie fisadi na tapeli mkubwa! akumbuke alichofanya nasaco? alivyotapeli shamba la kahawa kwa kuwatumia viongozi matapeli wenzie ambao wako ndani hada sasa. Sijui kwanini yeye yupo nje!
 
Ndefu sana
 
Achani uchwarA wenu. Mahakaman kumefungwa?
 
Mashetani ndivyo yalivyo ni kujaribu kuharibu taswira ya watumishi waaminifu!!!!Kwa sababu lichama lenu limejaa wizi mtupu basi mnaamini na wengine wanafanya hvyo
 
Fungueni kesi mahakamani kama kweli mwizi kuliko kulalamika tu. CCM ni chama tawala hawatakiwi kulalamika kama wapinzani
 
Ccm ni kama wachawi sasa hivi. Hakuna anayewapenda kwa dhati ila kwa woga.
hahahaaaaahaha we jidanganye kwa hili..umebaki peke yako hamia airtell mama. hata viongozi wako waliokwisha hama huwaoni au..huna macho..angalia chaguzi zoteeeee mnavyooigwa chini...usiwa underrate watanzania wewe..ukitaka kujua watanzania wana akili wasubiri kwenye sanduku la kura.
 
Fungueni kesi mahakamani kama kweli mwizi kuliko kulalamika tu. CCM ni chama tawala hawatakiwi kulalamika kama wapinzani
kwani waliokuwa kila siku wanatuimbisha nyimbo za mafisadi ni nani kama sio hao hao viongozi wa upinzani.. eti leo ukiwauliza wanasema walikuwa wanatania...pumbaffffff kabisa...wanafanyaje utani na maisha ya watanzania...? na ndio maana watanzania wamestuka...hawadanganyiki tena.hata ufisadi sasa uko kwenye mavyama.yenu hayohayo..unakumbuka kuna kashfa ya ufisadi chademaa iliyoibuliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali..fedha hazijulikani zilipoenda...hahahaha..ukiwauliza wanakupotezea eti defense yao wanarukia tril 1.5..hahahahhahaaa . hivi hawa halaf tuwape nchi hiiii....over my dead bodyyyyyy
 
Sijawahi kusikia kiongozi yeyote wa upinzani anasema alikuwa anatania. Kuna mahakama ya mafisadi iliyoanzishwa na serikali ya CCM. Kuliko kukaa na kulalamika kwa kutoa matamko kuhusu mbatia kwanini wasimfungulie kesi ndio hoja yangu iliposimamia. Tusiwe taifa la kulalamika wapinzani wanalalamika kwakuwa hawana mamlaka je CCM wenye mamlaka wanamlalamikia nani.?

ok kama wapinzani ukuwahi kuwasikia walikuwa wanatania..kwa hiyo hoja yao kwenye list of shame ilikuwa sahihi..kama ni hivyo kwanini waliwapokea haohao mafisadi na wakaamua kuwasafisha kwamba hawana hatia..hata kama wao wenyewe ndio walikuwa waki organize kampeni dhidi ya mafisadi
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Vijijini kimetoa taarifa ndefu kikiishutumu Taasisi ya Vunjo Development Foundation (VDF) ambayo Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Bwana James Mbatia ni mmoja wa viongozi waanzilishi na ndiye Katibu, kwa tuhuma mbalimbali, ikitaka VDF ichunguzwe kama inajihusisha na utakatishaji wa fedha.

Ripoti hiyo imezungumzia tuhuma nyingine mbalimbali. Pamoja na andiko hili, naambatanisha taarifa hiyo ya CCM kwa ajili ya kuibua mjadala.

Naomba kuwasilisha.
......................................................................................................................................................................................................

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI
S.L.P 541, MOSHI – KILIMANJARO

TAARIFA KWA UMMA SIKU YA JUMANNE,
TAREHE 18/12/2018.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mkutano wa hadhara uliofanywa na mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. JAMES FRANSIS MBATIA tarehe 25/11/2018, Kata ya Makuyuni – jimbo la Vunjo.

Ufafanuzi kuhusu upotoshwaji uliofanywa na Asasi isiyo ya Serikali ijulikanyo Vunjo Development Foundation (VDF):

1. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaitaka Asasi hii ijulikanayo Vunjo Development Foundation (VDF) iache kutumika kisiasa hasa kutokana na tabia na mienendo ya shughuli zake za kila siku ambazo ni kinyume na katiba yake.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaitaka Vunjo Development Foundation (VDF) itamke wazi kwa kuzithibitishia mamlaka za serikali na vyombo vyake ilianza na kiasi gani cha fedha katika akaunti yake na bajeti nzima ya mradi wa barabara za moramu kwa Jimbo la Vunjo ni kiasi gani. Pia, VDF itamke ilitarajia wananchi wa jimbo la vunjo wachangie kiasi gani. Kwa kufanya hivyo itaondoa uwezekano mkubwa wa Asasi ya VDF kutumika katika vitendo vya utakatishaji fedha (Money laundering) hasa kutokana na kumekuwapo na vitendo vingi vya taasisi zisizo za kiserikali kujihusisha na kutumika katika vitendo vya utakatishaji wa fedha.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaitaka Serikali kuichunguza taasisi ya VDF katika hili la utakatishaji fedha (MONEY LAUNDERING) ili kuweza kuondoa hisia hasi iliyopo kwa sasa.

2. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kimejiridhisha vya kutosha kuwa Serikali yetu chini ya MHE. Rais DKT. JOHN P. MAGUFULI kupitia Mkuu wa Wilaya ya Moshi haijakataa kushirikiana na Asasi hii ya VDF katika kuleta maendeleo ya kweli katika Jimbo la Vunjo jambo la msingi ni lazima taratibu, kanuni na sheria za nchi zifuatwe na kuheshimika na asasi hiyo.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kina mashaka na taswira ya jinsi asasi hii inavyofanya shughuli zake, kwani asasi hii imekuwa ikifanya shughuli za kukusanya michango kwa wananchi pasipo kupata kibali (uhalali) kutoka serikalini kinyume na sheria.

Asasi hii pia, imekuwa ikifanya uharibifu mkubwa wa mazingira hasa ukataji ovyo wa miti pamoja na kuharibu mali za wananchi. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi kama walivyoeleza kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Moshi Vijijini iliyofanyika kuanzia tarehe 08/02/2018 – 14/07/2018 na pia kwenye ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya iliyofanyika tarehe 08/11/2018 – 03/12/2018. Wananchi wengi wamekuwa hawakubaliani na namna zoezi hili la ukusanyaji fedha linavyoendeshwa na asasi hii ya VDF kwani imekuwa ikifanya vitendo vya kikatili kwa wananchi vya KUWABAMBUA mali zao wananchi ambao wamekuwa wakikataa au kushindwa kuchangia pesa.

Neno “kubambua” ni kitendo cha kuchukua kwa nguvu bila ridhaa ya mwenye mali kama vile mifugo au kitu chochote cha thamani kisha kuuza ili kulipia kiasi kilichowekwa.

3. Kutokana na vitendo vilivyofanywa na asasi hiyo vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupelekea hatari ya uvunjifu wa amani, serikali ya wilaya kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliamua kuingilia kati jambo hilo na kusitisha zoezi la uchangishaji huo wa fedha. Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaipongeza serikali kwa uamuzi huo ambao ulilenga kuirejesha katika meza ya mazungumzo baina ya taasisi hiyo ya VDF na serikali. Tunaamini lengo la Mkuu wa Wilaya ya Moshi / Serikali ni kuweka utulivu na amani kwa wananchi ambao wamekuwa wakiilalamikia serikali kutoingilia kati suala hilo.

4. Asasi hii ya VDF mbali na kutakiwa kufika katika meza ya mazungumzo, haikufanya hivyo badala yake iliamua kumfungulia kesi tatu (03) Mkuu wa Wilaya ya Moshi. Kesi zote zimefunguliwa katika mahakama kuu ya kanda ya Dar es salaam akishtakiwa kama Mkuu wa Wilaya na nyingine ni kutoka kanda ya Moshi akilengwa binafsi kama Kippi Warioba, kwa kuwa tunaamini katika Utawala wa sheria tunaiachia Mahakama jambo hili kwa kuwa hatutalizungumzia kwa kina kuepuka kuingilia kazi ya Mahakama.

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaitaka asasi hii inayojiita VDF ijitathmini kama dhamira yao ni njema katika Wilaya hii ya Moshi hususani Jimbo la Vunjo.

5. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinatoa masikitiko makubwa juu ya upotoshaji uliofanywa na Mh.

Mbunge JAMES F. MBATIA kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika tarehe 25/11/2018 kwenye viwanja vya Makuyuni kwa kudai kuwa asasi hii ya VDF ina wajibu (Majukumu) sawa na TARURA au TANROADS na kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi imechoka na haina uwezo wa kuwatengezea wananchi wake barabara.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinamkumbusha MH. MBUNGE kwamba TANROADS na TARURA hizi ni taasisi za serikali na zimepewa mamlaka kamili ya kikatiba na sheria za nchi na sio VDF juu ya ukarabati na ujenzi wa barabara katika nchi hii. Hivyo basi, shughuli zote zinazofanywa na asasi hii ya VDF si halali kabisa. Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinataka MH. MBUNGE aache kupotosha wananchi katika kuhalalisha asasi yake ya VDF kuwa ina uwezo wa kufanya lolote sawa na TARURA, TANROADS na Serikali yake.

Wananchi wanajua kuwa TARURA ina vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo kutoka kwenye bidhaa au huduma itakayokuwa inatoa, ruzuku ya Serikali, bodi ya barabara , mikopo na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo, Sekta binafsi (PPP), Ushuru wa maegesho, tozo la msafiri, ada ya kutumia hifadhi ya barabara n.k.

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaitaka VDF ijikite kama mdau wa maendeleo. Jambo hili sio geni katika nchi yetu kwani NCHI YETU imekuwa ikipokea misaada mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya huduma za wananchi zikiwemo barabara, afya, elimu n.k.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinahoji nia ya asasi hii ya VDF kukataa kukaa meza moja na Serikali ya eneo husika ikiwa nafasi hiyo wamepewa ?

Mashaka yetu makubwa dhidi ya asasi hii ni uwezekano wa kutumika kisiasa. Ifahamike kuwa Katibu wa VDF ni Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI (T) na Mbunge wa Jimbo la Vunjo (NCCR). Hili linatoa hisia hasi, hasa ikizangatia tamko la asasi hii ya VDF walilolitoa kupitia kwa wakili wa kujitegemea Ndg. HAROLD SUNGUSIA kumfungulia mashitaka Mkuu wa Wilaya ya Moshi MHE. KIPPI WARIOBA lilifanyika katika ofisi ya chama cha siasa cha NCCR Mageuzi jimbo la VUNJO. Uhalali wa asasi hii ya VDF kufanyia shughuli zake katika Ofisi ya Chama cha siasa (NCCR Mageuzi) unatoka wapi?.

Rai ya Chama Cha Mapinduzi kwa Serikali:-

1. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinaiomba Serikali kupitia vyombo vyake ichunguze maudhui ya asasi hii uhalali kama ilivyosajiliwa na ichukuliwe hatua za kisheria endapo itabainika kukiuka taratibu na katiba yake.

2. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA VIJIJINI kinaiomba Serikali wakati inaendelea kujiridhisha na uhalali wake na mwenendo wake isitishe utendaji wa shughuli zake zote katika Wilaya hii ya MOSHI mpaka ijiridhishe.

3. Kwa kuwa VDF imekusanya fedha za wananchi pasipokuwa na kibali kutoka Serikalini na kwa kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika kupitia mikutano mbalimbali wakishurutishwa kuchangia hizo fedha na wasipofanya hivyo wanabambuliwa tunaitaka Serikali ichukue hatua za kisheria kuhusu asasi hii ikiwemo pesa zote zilizokusanywa kutoka kwa wananchi kurejeshewa wahusika haraka iwezekanavyo.

4. Kwa kuwa VDF imekuwa ikijihusisha na shughuli za ujenzi wa barabara kama ilivyo kwa makampuni mengine ya ujenzi, tunaitaka serikali kupitia TRA waichunguze asasi hii ya VDF kama wana “TIN NUMBER” na kama wanalipa kodi ya serikali kama makampuni mengine ya ujenzi yanavyofanya.

Kuhusu fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo (CDCF) - Vunjo:
Sheria ya mfuko wa maendeleo ya jimbo (The constituencies Development Catalyst Fund Act. Na. 16 ya mwaka 2009) ilitungwa Julai mwaka 2009 na kusainiwa na MHE. RAIS, August 21 mwaka huo kwa lengo la kuchochea maendeleo jimboni ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo hufanyika kwa juhudi za wananchi wakishirikiana na mbunge wao, pamoja na serikali kuu kama mchochezi mkuu anayetoa pesa.

Ifahamike kuwa kamati ya mgawanyo wa fedha hizi za mfuko wa jimbo, Mbunge ni mwenyekiti na Afisa Mipango wa Halmashauri ni Katibu.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kimejiridhisha vya kutosha kuwa mbunge wa jimbo la vunjo MHE. JAMES MBATIA anatumia fedha za mfuko wa jimbo la vunjo kwa upendeleo kwa maslahi yake binafsi.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinahoji mgawanyo wa fedha za mfuko wa jimbo la Vunjo ambazo ni shilingi milioni 45,908,878/= namna zilivyopangiwa matumizi yake hivi karibuni kwenye vikao halali ambacho Mwenyekiti wake ni mbunge JAMES FRANSIS MBATIA.

Katika mgawanyo huu wa pesa kata ya Marangu Mashariki pekee imetengewa shilingi milion 30 kati ya hizo milion 45, kata ya makuyuni imetengewa milion 5 na shilingi milion 10 bado hazijapangiwa matumizi yoyote.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinamtaka Mh. Mbunge JAMES MBATIA awaeleze wananchi wote wa jimbo la vunjo lenye jumla ya kata 16 ambazo zina haki ya kunufaika na fedha za mfuko wa jimbo, ikizingatiwa kuwa maeneo mengi ya jimbo la Vunjo miradi mingi imesimama kwakukosa fedha ni kigezo gani kilitumika kutoa robo tatu ya pesa zote kutumika sehemu moja kama sio kuwabagua na kuwatenga wananchi wa kata nyingine. Na kwa taaarifa tulizonazo pesa hizo zinatarajiwa kuelekezwa katika asasi yake binafsi ya VUNJO DEVELOPMENT FOUNDATION (VDF).

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinataka wananchi wote wa Jimbo la Vunjo kuhoji fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo la Vunjo matumizi yake na mgawanyo wake katika maeneo yao.

Kuhusu mgogoro wa Shamba la Lokolova:
Mgogoro wa kugombea ardhi ya shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,470 lililopo kata ya Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa. Mgogoro huu unahusisha Chama cha ushirika na jamii ya wafugaji katika eneo hilo.

Mbali na eneo hili kuwa na mgogoro mbunge wa jimbo la Vunjo MHE. JAMES MBATIA kwa kutumia nafasi yake ya ubunge alifanya hila chafu za kujipatia ardhi yenye ukubwa wa ekari 25 ndani ya ekari hizo 2,470 za ardhi ya Lokolova.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinataka wananchi wafahamu suala hilo na wamfahamu aina ya mbunge ambaye wanaye.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini tunaishukuru serikali kwa kuzuia hati ya ardhi ambayo mbunge amekuwa akijaribu kila mbinu za kutaka kupatiwa hati hiyo ya ardhi.

Ufafanuzi kuhusu mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo kutoshiriki mkutano wa hadhara na kuwa sehemu ya kikwazo kwa mbunge katika kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.

Chama Cha Mapinduzi kinapenda ieleweke ya kwamba madai yote aliyoyatoa MH. Mbunge JAMES F. MBATIA dhidi ya Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Himo sio ya kweli. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI katika madai haya yanayotolewa na Mh. Mbunge imejiridhisha yafuatayo:-

1. Kauli za mbunge kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika tarehe 25/11/2018 kata ya makuyuni, zinakiri kwamba mikutano yote ya kimaendeleo aliyowahi kuitisha mbunge, ilihudhuriwa na mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo na aliweza kutoa mawazo mbadala ya kujenga maendeleo katika Jimbo.

2. Hakuna mahali ambapo Mh. Mbunge ameweza kuthibitisha kwa vielelezo kuwa Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo amekuwa ni kikwazo katika maendeleo ya Jimbo la Vunjo kama alivyodai katika mkutano wake wa hadhara aliouitisha.
KUTOKANA NA KUJIRIDHISHA HUKU:

1. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinataka kuwathibitishia wananchi wote wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo na Jimbo la Vunjo kwa ujumla hakuna taarifa yoyote ya mwaliko aliyopewa Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo ya kumjulisha na kumwalika kuhudhuria katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika eneo lake siku ya jumapili tarehe 25/11/2018.

2. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinahoji uhalali wa mbunge JAMES FRANSIS MBATIA kumsema na kumkosoa Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Himo ambaye anatokana na Chama Cha Mapinduzi kuwa ni kikwazo kwa maendeleo kwa sababu tu ya kutohudhuria mkutano wake wa hadhara ambao hakupewa mwaliko?

3. CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOSHI VIJIJINI kinamtaka Mh. Mbunge aonyeshe kwa vitendo kama ana dhamira ya kweli ya kutaka kushirikiana na mwenyekiti wetu wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo. Hususani kwa nini Mh. Mbunge amekuwa akikataa kuhudhuria kwa makusudi kabisa vikao mbalimbali vya mamlaka ya mji mdogo wa Himo vinavyohusu maendeleo huku ofisi yake ikiwa inapewa taarifa rasmi na mwaliko kwa mbunge kuhudhuria vikao hivyo?
Ushauri wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kwa Mbunge:

1. Chama Cha Mapinduzi kinamtaka MH. MBUNGE kutimiza wajibu wake kama kiongozi na mbunge kwa mujibu sheria na taratibu zilizopo.
2. Chama Cha Mapinduzi kinamtaka MH. MBUNGE aache kutoa visingizio visivyo na mashiko ili kutaka huruma ya wananchi.
3. Chama Cha Mapinduzi kinamtaka MH. MBUNGE aache mara moja tabia ya kuchonganisha wananchi na viongozi wao kama mtaji wake wa kisiasa.

MWISHO

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaomba wananchi wa Jimbo la Vunjo waendelee kuwa na Imani na Serikali yao inayoongozwa na Mhe John Pombe Magufuli kuwa Serikali hii ambayo mbunge anaituhumu kuwa haina uwezo wa kujenga barabara ndio serikali iliyojenga barabara zote za lami zilizopo katika Jimbo la Vunjo zenye thamani ya mabilioni ya pesa.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinamtaka MH. Mbunge JAMES MBATIA aache kutafuta wa kumlaumu kwani kushindwa kwake kuleta maendeleo katika Jimbo la VUNJO kunatokana na kushindwa kwake kuwa mwakilishi mzuri ndani na nje ya Bunge kwani imekuwa ni desturi kwake kususia bajeti za maendeleo za Serikali ndani ya Bunge. Ni vema Mh. Mbunge akawa na hofu ya Mungu kwa kila jambo analolitenda kwani kwa kufanya hivyo kutamfanya awe mkweli na mpenda maendeleo wa kweli na bila unafiki.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kilitamani leo Mh. Mbunge aje na maelezo ya kina juu kero mbalimbali ambazo kwa mda mrefu sana zimekosa majawabu yake. Awaeleze wananchi wake ni kwa kiasi gani ameweza kushirikiana na Serikali iliyopo madarakani ya CCM katika kuhakikisha huduma mbalimbali zimeboreka mathalani changamoto za afya, mindombinu ya shule, utatuzi wa migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji n.k.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaamini kwamba maendeleo yanapiga kelele sana kuliko maneno. Sio siri kwa kipindi chote cha uongozi wa Mh. Mbunge maendeleo mengi yamesimama hasa kutokana na uwajibikaji mbaya wake. Ni kweli usiopingika Jimbo la Vunjo linapitia wakati mgumu sana kipindi chake. Ni vema wananchi wa Jimbo la Vunjo wakatathmini juu ya mwenendo wa mbunge wao kama kuna haja ya kumpa nafasi tena ya miaka mitano ijayo ya maumivu.
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kimefatilia kwa uzito wake kauli ya Mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. JAMES MBATIA kupitia mkutano wake wa hadhara uliofanyika terehe 25/11/2018 siku ya jumapili. MHE. JAMES MBATIA aliwatangazia wananchi wa Jimbo la Vunjo kuwa MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA atakuja Vunjo kwa ajili ya kufungua barabara za moramu. Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini tumeiuliza serikali juu ya kauli hiyo ya Mbunge MHE. JAMES MBATIA kuhusu ujio wa MHE. RAIS ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro, tumejibiwa hakuna taarifa yoyote ile hadi sasa ya ujio wa MHE. RAIS katika Mkoa wa Kilimanjaro hususani jimbo la Vunjo.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kimejiridhisha vya kutosha kuwa MHE. Mbunge JAMES MBATIA anawapotosha wananchi wa Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kwa makusudi kabisa kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinaitaka serikali katika Mkoa wetu wa Kilimanjaro imtake Mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. JAMES FRANSIS MBATIA afute kauli yake mara moja kwani yeye si msemaji wa Serikali katika Mkoa wa Kilimanjaro, tofauti na hapo tutapata mashaka sana juu ya kauli zake hizi ambazo zinaingilia moja kwa moja mamlaka ya Serikali katika Mkoa wetu wa Kilimanjaro.

Mwisho kabisa, Tunapoelekea mwisho wa mwaka, Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kinawatakia wananchi wote wa Wilaya ya Moshi Vijijini sikukuu njema ya CHRISTMASS na heri ya mwaka mpya 2019, msherehekee kwa amani na upendo.

Imetolewa na:-
Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Moshi Vijijini
Chapisho lingependeza iwapo wangeitaka serikali na vyombo vya dola viache kutumika kisiasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom