Kila Taifa duniani lina alama yake ya taifa (Emblem) na kwa tanzania alama yetu ni "mwenge" kama ilivyo kwa taifa la Marekani ambao wenyewe wanatumia Ndege aina ya Tai. Mwenge ni alama muhimu sana kwa Historia ya nchi yetu.
View attachment 501095
Mwenge unabeba falsafa na Imani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhusu taifa alilokuwa anatarajia kulijenga mara baada ya Uhuru wa nchi ya Tanganyika mwaka 1961. Mwalimu alisema
"Sisi watanganyika, tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka ya nchi yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau". Huu ndiyo ulikuwa msimamo na mtizamo wa Mwalimu kuhusu Mwenge wa Taifa.
Kutokana na msimamo na mtizamo huo wa Mwalimu, Mwenge ndiyo umekuwa alama (Symbol) ya Lakiri (Seal) ya taifa letu. Kwenye kila Nembo yoyote ya kitaifa lazima kuna mwenge.
View attachment 501105 View attachment 501101 View attachment 501102 View attachment 501104 View attachment 501133
Kwa vyovyote vile Mwenge ni kitu muhimu sana kwenye utambulisho wa taifa letu. Lakini Chama Chama Mapinduzi wameshusha hadhi ya Mwenge hadi kuufanya upoteze heshima yake kwa jamii. Ni kwenye mbio za Mwenge ndoa za watu zinavunjika, Magonjwa ya Zinaa yanasambazwa, wananchi wanalazimishwa kuchangia mbio hizo na fedha zao zinaliwa, miradi hewa inazinduliwa na zaidi ya yote Mwenge wenyewe haupewi kipaumbela bali maslahi ya CCM.
Hao CCM wanaoshupalia mbio za mwenge wana Upendo kwa watanzania wenzao ambao si wa chama chao, hivi kweli chama hicho kinaleta tumaini pasipo na matumaini, na heshima mahali palipojaa chuki? Mwenge ni kitu adhimu sana kwa taifa letu lakini unadhalilishwa na CCM kwa jinsi mbio zake zinavyoendeshwa.