CAG: Kama tunataka kuongeza kodi tuachane na malipo kwa pesa taslimu, tutumie kadi

Ni wazo lililoenda shule sana, ila shida inabaki kuwa utatumiaje kadi wakati watu asilimia 90 hawana akaunti benki na pia nchi haina hata vitambulisho vya utaifa? Safari bado ni ndefu
Inawezekana mkuu, ninachokiona kwenye mabasi ya mwendo kasi nmegundua watanzania tunatamani sana na tuko tayari kwa mabadiliko ya teknolojia, tatizo wakutupeleka huko wako slow.
 
Mkuu namba 666 haiko kama ambavyo wengi wanafahamu na watu walivyoandika,kama uliambiwa iko kwenye vyakula haimanishi kwenye kibar code kinachoonyesha bei ya kitu.Hii ni roho kamili inatenda kazi,ikiwa juu ya ardhi hata mazao yanayotokana na ardhi hiyo yanakuwa na hiyo namba(ndiyo maana ni muhimu kuitakasa ardhi ya nchi yako),ikiwa juu ya anga pia,maji unayotumia.

Mojawapo ya sababu ya kumwomba Mungu ukiwa umefunga,kuna vitu hutakuwa navyo kwani hukula chakula wala kunywa maji ambavyo vimewekewa hiyo number.Ni kweli no 666 inatenda kazi hata sasa.Mwombe roho mtakatifu akufunulie ujue otherwise utaelewa ndivyo sivyo.Siri za Mungu ni nyingi naamini unajua na anayezifunua ni roho mtakatifu na si waandishi wengine wanatumia elimu za kidunia.

Hii issue ya kutumia card ni issue ya technologia na inaongeza usalama lakini ni sawa unabii unatimia kwamba siku za mwisho maarifa yataongezeka,hivi vitu havikuwepo enzi za mababu zetu.Cha muhimum wewe fahamu wakati tuliopo ni upi katika kalenda ya Mungu.

Nitarefer notice zangu kama kuna kitu cha kuongezea nitaongezea lakini ilivyo si kama wengi walivyofundishwa.
 
Mzunguko wa pesa umekuwa mdogo sana,vitu vimepanda bei sana hata bidhaa muhimu,kila mtu analalamika pesa haitoshi,which means demand inakuwa kubwa,kwa kuwa thamani ya shilingi iko vile vile,hivyo huyu mwananchi wa chini asiyekuwa na pesa nyingi analazimika kuhitaji pesa nyingi yenye thamani ndogo kwa matumizi machache.Uwezo wa manunuzi unakuwa mdogo.Halafu hapo hapo tunazungumzia kumkamua kodi vibaya.
Hivi kodi na principles za money supply,demand,value e.t.c havipaswi kwenda sambamba?
Nisaidieni wataalamu wa uchumi,mie ni k.ilaza tu eneo hili.
Eric Cartman
 
Ni wazo lililoenda shule sana, ila shida inabaki kuwa utatumiaje kadi wakati watu asilimia 90 hawana akaunti benki na pia nchi haina hata vitambulisho vya utaifa? Safari bado ni ndefu
Tatizo la serikali ya awamu hii haifikiri nje ya Dar. Leo CAG anaongelea eletroniki kai wakati baada ya kusema wanakata kodi kwenye ATM hakuna atakaye tumia tena mashine hizo na imeongeza sana matumizi ya hela cash.
 
Inashangaza mno kuona kwamba kila mwenye akaunti benki anapatiwa kadi lakini asilimia kubwa ya hizi kadi hazimpi mmiliki uwezo wa kufanya malipo. Hii cash culture tuliyonayo inaonekana hakuna mwenye uharaka wa kuiondoa; karne ya 21 hatupaswi kushindilia hela kwenye soksi au kubeba mfuko wa hela kwenda kununua gari.
Utabeba sana hela Mkuu. Kama wameweka kodi hadi kwenye ATM unategemea nini? Tunapenda kuwaza mambo makubwa sana halafu mwisho wa siku hatujui hata tufanyeje! Hii serikali inawaza kodi tu hakuna anayeongelea huduma bora.
 
Mawazo ya aina hiyo ndiyo yatakayoivusha nchi kutoka hapa tulipo. Lakini hizi mbinu za kipolisi eti usipodai risiti utapelekwa jela miaka mitatu ni uzembe wa akili tu. Unakusanya kodi kwa kutisha watu!!!???
Hahahaa manual
 
Ni wazo lililoenda shule sana, ila shida inabaki kuwa utatumiaje kadi wakati watu asilimia 90 hawana akaunti benki na pia nchi haina hata vitambulisho vya utaifa? Safari bado ni ndefu

Hili wazo ni zuri, ila mimi nadhani tunaweza tukatumia creativity kulisolve.
Ndio, nearly a large percent ya wananchi hawana bank account ila sasahivi mobile money is everywhere, kwamfano airtel wameintroduce kadi zao za nfc wao wanaziita "tap tap" ambazo zinakuwa linked to your airtel money, hii inamwezesha mtu kufanya malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali kwa kutumia hizo kadi instead of paying by cash or bank card. Therefore huu mfumo wa malipo still tunaweza kuucategorise as cashless.
Sasa mitandao mingine ikija pia na such products nadhani itakuwa tupo in the right direction kuelekea to a cashless society in a few years.
 
Hakuna lisilowezekana kwa Mungu jamani sisi tusikate Tamaa tuzidi kuomba
Mungu tena! Mungu ndiyo ataleta bank na ATM cards! Mambo mengine hayahitaji Mungu zaidi ya kufanya wenyewe tu, Mungu yupo bize kusikiliza maombi ya walio lala njaa unataka uende kuomba online banking na wewe. Kuumbwa kwa mfano wake ni uwezo wa kufikiri, maarifa na kutatua changamoto wenyewe sio sura.
 
Mkaguzi wa mapato na mahesabu ya serikali amesema matumizi ya kadi za kielekroniki kwenye mihamala itazuia ukwepaji kodi na kuongeza mapato kwa kuwa rekodi zinakuwa rahisi kupatikana na kufuatilia.
Amesema ununuzi kwa kutumia pesa taslimu unahamasisha wizi kwa kuwa mtu anaweza kununua nyumba lakini wakakabidhiana pesa bila kulipa kodi

Napata tabu kidogo kuoanisha Mambo ukizingatia elimu yangu ni NGUMBARO..
Kama kutumia kadi kunasaidia kutunza kumbukumbu na kuboresha makusanyo iweje makampuni ya simu bado kodi haiakisi mapato yake
Nafikiri bado kuna tatizo la kiusimamizi na kiuzalendo zaidi kuliko mfumo
 
teknolojia yetu tatizo ipo chini sana mkuu
Mimi nilishawahi kujiunga na mobile banking crdb.. Nikatoa laki tatu.. Nikaambiwa network ipo down.. Badae nikajaribu.. Tha same issue mara mbili hivi... Nikaenda kwenye atm mbali nikatoa pesa.. Kesho yake eti zile failed attempt zikakubali wakahamisha zile pesa kwenye sim yangu..
From that day nikatupa line.. Sitaki tena kusikia mobile banking mavi yao
 
Mawazo ya aina hiyo ndiyo yatakayoivusha nchi kutoka hapa tulipo. Lakini hizi mbinu za kipolisi eti usipodai risiti utapelekwa jela miaka mitatu ni uzembe wa akili tu. Unakusanya kodi kwa kutisha watu!!!???
Kwani ulikuwa haujui Africa ndio dampo LA viongozi walioza?lakini viongozi makini na wenye maono(ukawa) hawana thamani.Tanzania kuwa nchi ya viwanda itakuwa ni ndoto kama tusipokubali changamoto za kisiasa na maendeleo.
 
Utabeba sana hela Mkuu. Kama wameweka kodi hadi kwenye ATM unategemea nini? Tunapenda kuwaza mambo makubwa sana halafu mwisho wa siku hatujui hata tufanyeje! Hii serikali inawaza kodi tu hakuna anayeongelea huduma bora.

Huduma bora itapatikanaje kama ulipi kodi ,responsibility kwa haki baadae
 
Mawazo ya aina hiyo ndiyo yatakayoivusha nchi kutoka hapa tulipo. Lakini hizi mbinu za kipolisi eti usipodai risiti utapelekwa jela miaka mitatu ni uzembe wa akili tu. Unakusanya kodi kwa kutisha watu!!!???
Ww vip kulupa kodi ni wajibu wako acha kelele
 
Back
Top Bottom