Bungeni: Goodluck Mlinga(CCM) atoa mpya... Adai Anatropia(CHADEMA) anamtamani kimapenzi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787

Anasema kuwa wakati yupo Bungeni, mbunge wa CHADEMA Anatropia alimvua kofia aina ya kibagharashia na kutokomea kusikojulikana, na...

- Kumfanya akose sifa ya kuingia bungeni, hivyo wananchi wa Ulanga kukosa mwakilishi kwa muda

- Kumsababishia mtikisiko wa Mawazo kwa kumnyang'anya kofia.

- Kulikosea heshima vazi hilo (Utamaduni wa vazi hilo anayepaswa kumvua ni mkewe)

- Kuingilia Himaya ya Mke wake (Mama Glory) kwasababu yeye siye mkewe.

- Kuvunja Amri ya Tisa inayokataza kutamani mali ya mtu mwingine, hivyo Anatropia amemtamani kimapenzi

- Kuvunja Msimamo wa CHADEMA wa kutojongelea wabunge wa CCM

Ameuliza hivyo vitendo vyote vinaruhusiwa kwenye Bunge Tukufu?
 
Ooh my God hivi wabunge wanalipeleka wapi Bunge? Kweli watu tunakamuliwa kodi ili watu hawa walipwe mamilioni kwenda kufanya mambo haya bungeni?

inabidi ifike sehemu wawakilishwa tupaze sauti zetu kuonesha kutolizishwa na jinsi bunge linavyokwenda kwa sasa.
 
Nafikiri sasa wabunge wawe wanapimwa akili zao kabla hawajaapishwa kuwa wabunge kamili, huyo mbunge wa ulanga nafikiri hayupo sawa kiakili
 
Jimbo la ulanga lipo wazi huyu jamaa sio mzima kichwani mambo gani hayo? Komedi haitakiwi kwenye siasa inafanya watu waitumie kama udhaifu kukumaliza.
Huyu hata hawazii uchaguzi ujao maana ashajiondoa kwenye mashindano
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…