Mimi niko ofisini ila napenda kufuatilia mambo ya bungeni kupitia chanel ya Youtube ya Bunge, kwa kweli sauti iko chini sana, yaani kwa sauti hiyo hiyo ukiweka mziki sauti inakuwa kubwa inasikia vyema ila ukiweka bunge hata sauti ikiwa 100 lazima mtu asichezesha hata miguu ili kusikia vyema. Je huu ni mkakati tusisikie kinachojadiliwa au namna gani?
Bunge jirekebisheni wekeni sauti kubwa tusikilize hoja za hao viumbe huko. Hizi channel nyingine zinachukua kutoka kwenu kwa hiyo sauti ya huko ndio inafanya hata sauti za channel nyingine ziwe chini. Tuongezeeni sauti
Ongezeni sauti
Ongezeni sauti,
Kama hamtaki zimeni bunge lenu fanyeni kwa siri.