Bulembo: Uchaguzi wa marudio Zanzibar utakuwa huru na haki kama ule uliopita

Utakua huru na haki kama uliopita ??? Sasa nini sababu ya kurudia kama uliopita ulikua huru na haki ?
 
kwa sasa CCM imemeguka vipande ndani ya ccm kuna watu hawamtaki hata kumsikia magufuli ndio maana mr zero bulembo kachukua usukani na media inapenda kuongea na zero wakimlinganisha na yule aliyechukua madaraka
 
Mwenyekiti ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo ametoa maoni yake kuhusu hotuba ya rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein iliyosisitiza kuhusu marudio ya uchaguzi visiwani humo.

Akiongea na kituo cha runinga cha ITV leo, Bulembo amewataka wananchi kutokuwa nawasiwasi na kujitokeza kushiriki uchaguzi wamarudio pindi tarehe ya uchaguzii takapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kwani utakuwa uchaguzi huru na haki kama ulivyopita.

“Cha kwanza amani. Rais ameonesha kwamba nchi itabaki kuwa kama vile vile ilivyo… Ndani ya miaka 52 tumeishi kwa amani. Hilo ndilo kubwa sana ambalo watu wanalitilia mashaka. Na kawahakikishia kwamba lazima uchaguzi utakaofanyika utakuwa huru na haki kama ule uchaguzi mwingine ulivyopita,” alisema Bulembo.

“Kwa hiyo hicho ndicho unaweza kukishika mkononi ni amani. Na uchaguzi unafanyika ili tupate uongozi halali ili tuendelee kuwa na amani,” aliongeza.

Aidha, Bulembo aliwataka watanzania kwa ujumla kufahamu kuwa uchaguzi wa Zanzibar utawahusu wote kwa kuwa utahusu Jamhuri ya Muungano. Lakini aliwataka wenye haki kikatiba na waliojiandisha kupiga kura visiwani humo kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe itakayotangazwa.

“Katiba yetu inaongelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wapo wenzetu wanadhani labda uchaguzi unahusiana na Zanzibar, hapana. Uchaguzi huu (wa marudio) unahusiana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

NB: Kama uchaguzi uliopita ulikuwa huru na wa haki kwanini ulifutwa hivi CCM wamekosa msemaji.
Jamaa kweli kasoma huyu angalau darasa LA saba anazungumza uharo mtupu sasa kama ilikuwa guru na haki mbona mshindi hakutangaza kweli hili jamaa akili za samaki
 
Mimi huwa nasema mtu akishakuwa na mtumbo na mbichwa mkubwa huwa hwana akili kabisa si mnumuona le mutuz kazi ni kupiga picha na wanaume na mademu kwa kijipendekeza sasa hivi kweli ccm wameishiwa watu mpka kumtuma huyo mjinga kwenda kuongea ktk média kabisa
 
Huyu jamaa anajitahidi sana kujitutumua ili aonekane anawajibika ndani ya chama, tatizo uwezo wake wa uelewa kila anapojitokeza anaharibu vibaya sana, bora angenyamaza kimya tu.
 
Huyu ndo kabisaaaa kaharibu,ina maana sasa wasemaji wa ZEK ni akina BULAMBO!!!!what a shame?????
mbuzi hawezi nenepa siku ya mnada,mwapisheni Maalim msizidi kuumbuka.
 
Oooh kumbe ulikuwa huru na wa haki lakini haukuipendeza CCM eeh! Nyang'au!
 
Huyo Bulembo asituletee hizo pumba zake.
Hivi huyo jamaa anafikiri watanzania tumesahau kauli yake aliyoitoa wakati anamfanyia kampeni Magufuli kuwa CCM ipo tayari wapinzani wapate madiwani na wabunge, lakini kamwe haitoweza kuruhusu mpinzani aingie Ikulu!
Sasa kwani hiko kinachotokea huko Zanzibar kina tofauti gani na kauli hiyo aliyowahi kuitoa Bulembo kwenye kampeni za uchaguzi mwaka jana?
Watanzania tunachojua ni kuwa Jecha wao alifuta matokeo ya uchaguzi baada ya kugundua kuwa Maalim Seif amembwaga Dr Shein.
Kwa maana hiyo Jecha alikuwa akitekeleza falsafa 2 za CCM
Falsafa no 1 ni ile iliyotolewa na mwanamama Asha Bakari kwenye Bunge Maalum la Katiba alipotamka mle bungeni bila kupepesa macho na huku akishangiliwa na wabunge wenzie wa CCM aliposema kuwa Zanzibar kamwe haitakuja kutolewa kwa vijikaratasi vya kupigia kura!
Falsafa no 2 ndiyo hiyo yake Bulembo kuwa CCM iko tayari wapinzani wapate nafasi za Udiwani na Ubunge, lakini kamwe hawatakuwa tayari kuiruhusu Ikulu aingie Rais kutoka Upinzani!
Sasa hao CCM wanalazimisha uchaguzi wa marudio ambao hata wao wenyewe wanajua kuwa hautaisha salama na hivyo wao CCM ndiyo wanataka kuiingiza nchi yetu kwenye machafuko makubwa.
 
With all people ndani ya ccm huyu ndio anaachiwa kuongea???


Kwa mtazamo wangu basi bulembo leo kasema jambo muhimu sana kupata kusemwa na CCM yoyote tangu kutokeo mtafaruku wa uchaguzi Visiwani wa okt. 2015.

Hapa nanukuu sehemu ya statement ya ITV "...Bulembo amewataka wananchi kutokuwa nawasiwasi na kujitokeza kushiriki uchaguzi wamarudio pindi tarehe ya uchaguzii takapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kwani utakuwa uchaguzi huru na haki kama ulivyopita. "

Suali muhimu la kujiuliza kama uchaguzi uliopita ulikuwa huru na haki jee kulikuwa na haja gani ya kurejea uchaguzi? Kwa nini Tume isimalizie kutangaza matokeo ya uchaguzi huru na haki kuliko kufanya uchaguzi mpya. hapo ndipo penye masuali magumu kwa akina Bulembo na CCM!
 
Back
Top Bottom