Buku la kuruba yangu

Sep 12, 2018
34
27
Nilikuwa narafiki, lake jina Chumu.
Hakuwa mnafiki, ni mtu wakukirimu.
Sahibu hawabanduki, shida zao kujikimu.
Kwenye buku la rafiki unaweza kukopia


Zilipompata dhiki, nduki kubwa wanadamu.
Kuielekea haki, mjomba alo muhimu.
Ikaanza taharuki, hawakumtilia tena timu.
Kwenye buku la rafiki unaweza kukopia


Hukoo Mashariki, jiji la Darusalamu.
Maskani ashiriki, mwili umekosa damu.
Afanyalo habariki, aktharu L kalamu.
Kwenye buku la rafiki unaweza kukopia


Leo hawamtaki, hana kitu mwandazimu
Wanamfanya shabiki, hana tena utimamu.
Hisani hawakumbuki, kumpigia hata simu.
Kwenye buku la rafiki unaweza kukopia


Ulitendalo mkuki, hilo waja tufahamu.
Mbelekatu haufiki, kwanza kwenda kuhujumu.
Unaanza nasitaki, kuja nyuma kusalimu.
Kwenye buku la rafiki unaweza kukopia

Shairi hili ni stori ya ukweli, iliyomswibu rafiki yangu wa karibu. Katika kuandika kwangu, nilimtaka ruhusa — akaniruhusu!


Nina furaha kubwa kushiriki nanyi rafiki zangu wa ukweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom