Habari zenu wakuu,
Nimeingiwa na wasiwasi sana, nina mpenzi wangu nampenda sana, lakini hivi karibuni ameanza kubadilika.
Kila muda nikionana naye ananipa stori za
mshana jr na
Bujibuji, anadai amewafahamia JF. Anataka eti wamfundishe kujikinga na wachawi, hivyo anawatafuta. Kumbuka hajui kama mimi nipo JF, wala hajui kama najua wanavyoleta thread za kichawi.
Anadai eti anamtafuta
Bujibuji ili ampe dawa ya kuona wachawi na kugundua nyoka wa Kichawi.
Mshana anataka ampe dawa na kujikinga na majini. Wiki mbili sasa akilala anaweweseka, anaota na kutamka maneno kwa Sauti. Kilichofanya niandike hapa, ni baada ya jana kuota na kusikia maneno akitamka kabisa BUJI, ikabidi nimuamshe, akasema nimemsikia vibaya alikua anaota akinywa Uji.
Mke wangu mwenyewe kila siku namuona kule MMU.
Naombeni msaada ili mpenzi wangu asichepuke kwani bado nampenda. Na hawa watu wanaomtongoza kwa dawa nawaogopa sana.