Bosi wa e-Government Dr. Jabiri Kuwe Bakari, kama umeshindwa kazi kaa pembeni

Kama yuko hivyo ninavyosoma hapo juu....anashindwa nini kutimiza malengo ya taasisi yake? Tunapimwa kwa vigezo sio maandishi na mikwala mingi mingi huku tunachofanya ni zero
wewe umeshindwa kuandika mukwara ukaandika mikwala . ungepewa hiyo kazi si ingekuwa balaa. Tuwe wepesi wa kuboresha kwa ushauri badala ya kukosoa kwa roho iliyojaa nyongo
 
Wewe pengine una chuki binafsi na Dr. Bakari. Haya sasa mambo ya kuvaa beji yanakujaje hapa. Jamaa anafanya kazi yake vizuri na kwa weledi. ICT ni zaidi ya tovuti jamani. Tovuti ziko chini ya vitengo vya Habari, mawasiliano na Elimu kwa umma. eGovernment ni zaidi ya tovuti. Acha chuki binafsi
Unachotetea ni nini?

Huyu mtu ndiye CEO wa e-Government Agency.

Hawa watu ni wazembe sana sana.

Inashangaza kuna baadhi ya watu kama wewe mnajitahidi kuwakingia kifua!
 
wewe umeshindwa kuandika mukwara ukaandika mikwala . ungepewa hiyo kazi si ingekuwa balaa. Tuwe wepesi wa kuboresha kwa ushauri badala ya kukosoa kwa roho iliyojaa nyongo

Ngoja jipu litumbuliwe kwanza
 
Kaka Idris, Yafanyie Kazi Haya Malalamiko Kama Kuna Ukweli,tuna Imani Na Ungozi Wako!
 
Tusimlaumu sana huyu jamaa kwani inawezekana hana vijana wa IT wa kutosha ambao ndio kazi yao kufanya updates na kazi zingine zilizo chini yake.

Kosa lake kubwa ni kutofuatilia kwa karibu kuona vijana wa IT katika idara zote wanafanya hizo updates na kadhalika.

Hivyo si kushindwa kazi maana anaiweza bali ni kujisahau ambako kwa Tanzania ni kawaida.

Mtu huwezi kuwa umesomeshwa hadi Ulaya halafu unajikalia tu kizembezembe.
 
Boss kabla ya ku-attack fanya kwanza utafiti.Ujue eGa wanafanya nn nini majukumu yao n.k.pia kazi ya tovuti ni ya nani kwa mipaka ipi (content/technology ).Hapo umekurupukaaaa mzee
 
CEO ana wasaidizi tena waliopewa hicho unachokiona sio. Hawezi kuondoka kwa un updated website !!
Hata ya Ikulu na wizara kibao zina mapungufu !!
Mfano ni majina mapya wa wizara na anwani zake nk.
Umekurupuka.
 
Wewe pengine una chuki binafsi na Dr. Bakari. Haya sasa mambo ya kuvaa beji yanakujaje hapa. Jamaa anafanya kazi yake vizuri na kwa weledi. ICT ni zaidi ya tovuti jamani. Tovuti ziko chini ya vitengo vya Habari, mawasiliano na Elimu kwa umma. eGovernment ni zaidi ya tovuti. Acha chuki binafsi
Ameshindwa kazi.. tovuti zinatia aibu
 
mtoa mada napenda kukupa ufahamu kidogo juu ya hii depertment ya e-goverment agency
ina majukumu makuu yafuatayo
1.huduma kwa simu
2.mtandao waserikali
3.mfumo wa barua pepe wa serikalini
4.rasilimali shirikishi za tehama
5.kuhifadhi mifumo ya tehama
6.kutoa ushauri na ufundi
7.usajili wa anuani na tovuti za serikali
8.usajili wa namba za SMS/USSD
9.Uthibitishaji wa miradi ya tehama
hayo ndio majukumu makuu ya e-goverment agency
dr. jabiri bakari ni proffesional na anajua nn anachokifanya ifike mahala siasa zikae pembeni na wanataaluma tuwaache wafanye kazi zao so tusilazimishe aonekane jipu wakati hakuna majukumu yake ya kimsingi ambayo hajayakamilisha,.
 
Wewe pengine una chuki binafsi na Dr. Bakari. Haya sasa mambo ya kuvaa beji yanakujaje hapa. Jamaa anafanya kazi yake vizuri na kwa weledi. ICT ni zaidi ya tovuti jamani. Tovuti ziko chini ya vitengo vya Habari, mawasiliano na Elimu kwa umma. eGovernment ni zaidi ya tovuti. Acha chuki binafsi
Hebu update info kwenye hiyo tovuti yenu

acha ubishi
 
Naomba kuweka kumbu kumbu sawa!

  1. Dr. Jabir sio Mkuu wa TEHEMA wa serikali, yeye ni Mtendaji Mkuu wa eGA! Mkuu wa TEHEMA wa serikali yupo kule PO-PSM! Hata yeye pia hana uwezo au mamlaka ya kukagua content za tovuti za taasisi zote za umma!
  2. eGA ni wakala ya serikali kama zilivyo wakala zingine mf: TMA, WDMI, TAeSA, kwa uchache!
  3. Katika utaratibu wa serikali, maudhui ya website au tovuti ya taasisi yapo chini ya PR Officer ama Marketing Officer, hii maanake ni kuwa, Taasisi zote za umma, watu wa TEHEMA wanahusika na technical issues tu za tovuti na sio content za tovuti!
kama hivo ndivyo basi, huwezi kumlaumu Dr Jabir moja kwa moja eti tovuti ya Taasisi fulani au ya eGA haina updated content, nadhani hapa kuna tafsiri hasi ya "hapa kazi tu!"

Ukweli ni kwamba hata hao ma PR wana wakurugenzi wao, wanawajibika kwao, tuachane na mambo ya kutumia nyundo kubwa kwa ajili ya kumuua sisimizi tu!

Yaani imefikia mahali content ya website, imuondoe CEO katika nafasi yake, lets be serious wajameni! Tuache huu utamaduni wa hovyo tunaotaka kuujenga, Dr Jabir kitaaluma ni Mtu wa TEHAMA mbobezi, hana taaluma ya PR au Marketing kama mnavotaka iwe! Kwa hiyo mnataka Dr. Jabir akilala akiamka aanze kukagua tovuti za mashirika yote ya umma, akimaliza akague tovuti zote za halmashauri zote, kisha akague tovuti zote za wizara na Taasisi mbali mbali!

Come on, hebu tujenge nchi kwa njia sahihi, sio hivi!

Analipwa kodi zetu kufanya kazi hiyo. Kama anaona ni kazi kubwa na nzito sana bas aache wapo watu wana Masters za MUM wanaweza kufanya hiyo kazi ambayo yeye anaona ni chini sana kwake
 
mtoa mada napenda kukupa ufahamu kidogo juu ya hii depertment ya e-goverment agency
ina majukumu makuu yafuatayo
1.huduma kwa simu
2.mtandao waserikali
3.mfumo wa barua pepe wa serikalini
4.rasilimali shirikishi za tehama
5.kuhifadhi mifumo ya tehama
6.kutoa ushauri na ufundi
7.usajili wa anuani na tovuti za serikali
8.usajili wa namba za SMS/USSD
9.Uthibitishaji wa miradi ya tehama
hayo ndio majukumu makuu ya e-goverment agency
dr. jabiri bakari ni proffesional na anajua nn anachokifanya ifike mahala siasa zikae pembeni na wanataaluma tuwaache wafanye kazi zao so tusilazimishe aonekane jipu wakati hakuna majukumu yake ya kimsingi ambayo hajayakamilisha,.

Unajichanganya mwenyewe

angekuwa anajua anachokifanya hii thread isingekuwepo hapa
 
Nashangaa mpaka leo bado wazara ya kilimo na ile ya uvuvi na mifugo zina website zao pamoja na kuunganishwa kwake
 
Dr idrisa jabiri anaitia aibu open university,kwani alikua boss wa IEMT hapa open university.
 
Unajichanganya mwenyewe

angekuwa anajua anachokifanya hii thread isingekuwepo hapa
hakuna anaejichanganya u have to know kuwa kuna utofauti wa mtandao wa serikali na tovuti za serikali e government hawahusiki na ku update hayo mawebsite
 
Kweli watz kama huu ndo uwezo wetu wa kuchambua mambo? Basi bado sana...! Isomeni ega kwanza...vizur uielewe ni nn hasa hyo ega...hoja zinazotolewa hapa ni sawa na kwenda kwenye atm ukute haijawaloaded cash...utoke mbio ukatake mkuu wa ict wa benki husika aachie ngazi...! Rubbish kabsa..! Nadhan aina hii ya uchambuzi ni very primitive!
 
Back
Top Bottom