Bora mfumo wa chama kimoja, haya ni mateso kwa Afrika

Mkuu Naanza kukubali maneno ya yule mgombea wa republican kuhusu Africa maana hawa wanaojifanya viongozi wanaongoza kutuua ndio maana hata mahakama ya ICC hawaitaki,lakini kila lenye mwanzo lina mwisho.
 
Sijui kwa nini ila nakubaliana mno na Trump.......anachosema ni sahihi kabisa......

Uko kama mimi,watawala ndiyo wabadhirifu wakubwa wa mali za umma,na Polisi na wanajeshi badala ya kulinda Mataifa yao wanalinda ulaji wa watawala.Hakika tunamuhitaji Trump
 
Kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini kuna haja ya kuithamini kama tuendelee na mfumo wa vyama vingi au turudi chama kimoja.
Hivi vyama vya siasa vimeleta mfarakano mkubwa katika jamii leo hii kuna yatima, walemavu, waliofungwa hata kuumizwa kwa sababu ya siasa za vyama.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema chama cha siasa ni jukwaani na barabarani huko ndipo wanaweza kufanya siasa zao na kutafuta uungwaji mkono pamoja na kupata wanachama wapya kwa kuuza sera zao lakini kwa sasa hali ni tofauti vyama vya siasa vimezuiwa kufanya mikutano hivyo huenda vikakosa wanachama wapya.

Je, kwa hali hii kuna haja gani ya kuendelea kuwa na vyama vya siasa ambavyo haviwezi hata kufanya mikutano ya kisiasa.
Dhahiri sasa kuliko kuendelea kujaza watu chuki, kutokana na kundi moja kuonewa turudi kwenye chama kimoja ili hata hizo pesa wanazopewa vyama vya siasa zitumike kwenye shughuli zingine za maendeleo.
 
Mkuu naunga mkono hoja kwa asilimia mia. Kihalisia sasa tulichonacho ni mfumo wa chama kimoja uliovishwa joho la vyama vingi. Sasa ni vizuri rais angetangaza tu kwamba tanzania ni nchi ya chama kimoja, tuache kutumia mabilioni mengi kwenye chaguzi kila baada ya miaka mitano. Wachaguane tu wenyewe kwenye mkutano wa chama dodoma iishie hapo tujue moja.
 
Back
Top Bottom