Bomoabomoa Kibamba yapigwa marufuku na Mahakama Kuu

gkutta

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
273
168
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imepiga marufuku bomoabomoa iliyopangwa kuanza katika jimbo la Kibamba, ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.

Amri ya usitishwaji wa bomoabomoa hiyo imetolewa leo (Jumaatu) na Jaji Leila Mgonya, kufuatia maombi ya zuo la muda yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wakazi wa jimbo hilo, kupitia kwa jopo la mawakili wao wanne, likiongozwa na Wakili Aidani Kitare.

Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na Abdallah Maliki kwa niaba ya wenzake 570, ambao ni wakazi wa maeneo ya Kimara, Mbezi na Kiluvya, dhidi ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika maombi hayo watoa maombi walikuwa wakiiomba mahakama itoe amri ya kuruhusu hali iendelee kuwa kama ilivyo, kwa maana ya kuwazuaia Tanroads kuendesha operesheni ya bomoabomoa, kusubiri kuisha kwa taarifa yao ya siku 99 kwa Serikali, ili kiufungua kesi ya kupinga bomoabomoa hiyo.

Chanzo: Muungwana Blog
 
Hawa jamaa nao ni wasumbufu sana kibaya zaidi kuna mida mingine huja bila taarifa hata usiku na kuanza kubomoa nyumba za watu, wazuieni tu hadi mwafaka upatikane.
 
Huyu jamaa anaweza kubomoa kinguvu hata kama mahakama imeamua.
 
Safi sana.

Kaka BAK hivi wanamjua Mgu kweli?, jamaa huwa hafati sheria hata kidogo, pale Mbezi Luis kulikuwa na zuio kama hilo na nyumba zikabomolewa, Magomeni Qtr kulikuwa na zuio kama hilo na nyumba zikavunjwa, watu wa maeneo ya Buguruni kandoni mwa reli walikuwa na zuio kama hilo na nyumba zikavunjwa, ile petrol station pale KAMATA ina hati ya tangu 1952 na walikuwa wanalilipia eneo lao lakini imevunjwa bila fidia yoyote,
Ningekuwa mimi nina nyumba hayo maeneo kwa kweli ningeanza kuangalia uwezekano wa kuamisha mali zangu, pamoja na hilo zuio watakuja kulia kilio kikuu kwa kupoteza mali zao
 
Nakumbuka ule wimbo wa M4V wa "presha inapanda inashuka...."
Poleni sana wana kibamba
 
Nafikiri ni vizuri zaidi serikali kuelewana na wananchi wake kwa mapana zaidi ktk mambo yanayoleta athari kubwa, kama hili kwa pande zote. Na haya pia yanasababishwa pengine na kutokuwa na mipango ya muda mrefu kama nchi, ama wananchi kutokupewa ufahamu wa kutosha.
 
Maendeleo ni muhimu lakini wafuate taratibu zote za kisheria, na kama watu wanatakiwa kulipwa fidia walipwe kwa wakati muafaka...
 
Nathan kuna shida mahali Kwani barabara ya zamani ilikuwa na hemaya yake ya mita 60! Ila kwa sasa imevamiwa hadi kwenye kingo! Je ina Maana serekali haikuwa na hati miliki ya hii barabara? Hawa wavamizi napendekeza wabomolewe bila huruma! Nani aliwaruhusu kujenga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…