Bodi ya Kimataifa ya Ushauri kwa Bodi ya Wakurugenzi na Watendaji ya Barrick Corporation Group...

Wamo mawaziri wa wizara ya ulinzi wawili wa marekani,mawaziri kutoka Canada,uingereza,spain

View attachment 523912

View attachment 524944
wanapaswa kujiuzulu maramoja hili kulinda heshima zao,kuliko kuendelea kuwa kwenye bodi ya kampuni ambayo imeshiriki kuibia nchi masikini kama Tanzania...wanajifedhehesha na nitawashangaa wasiasa makini wa Marekani na Ulaya kama watainyamazia hii kampuni ya Barick na Acacia...genge la wezi hili,na wana mawakala wao humu nchini wengi tu kama walivyotajwa katika taarifa ya Kamati ya pili!
 
Acha kuota wewe!! Wapi kuna Noah ya 2.16M? Hebu watz tuwe tunafanya tathmini ya kina jamani. Ndiyo maana tunashangilia mambo kabla hayajawa mambo. Hebu piga hesabu hii halafu uniambie hiyo Noah unaipataje. 108,000,000,000,000/50,000,000=2,160,000. Acheni kudanganywa.
ACha kukurupuka wewe!
Halafu kwanza Mi nimetania halafu uliambiwa ni watu wazima umri kuanzia miaka 18 na kuendelea!

Hiyo million 50 uliyogawanya ni sensa ya mwaka gani Ndio unasema watanzania watu wazima sasa hivi tuko million 50?
 
kila mchuma janga hula na nduguze kama ni ushauri toka kwa kagame na bashite basi najua huko kigali wanakula shampeni maana muda si mrefu tutaanguka kiuchumi na wao watazitumia rasilimali zetu kama zao kwa kigezo cha ushirikiano ili tuinuke tena.........
hahahahahah nani alikwambia kua kagame ana urafiki wa kweli? nani asiejua kua kagame alibadilishia gia angani kwakua chaguo lake lilikua lowasa? baada ya kuona hakuna namna na huyu jamaa ndio mkulu akamuingia na gia ya kuwa wowe ni wachu, kumbe danganya toto jinga then ulidhibiti.......
JK pole sana na ile operesheni kimbunga yako ambayo ilikua ya kizalendo na yenye lengo la kunusuru nchi yetu toka katika mikono ya watutsi wenye roho mbaya wenye kuitamani na kuihusudu nchi yetu....

sasas twaafwaaaa rasmi
Nonsense! Mzushi mkubwa wee!
Still thinking the same?
 
Bodi ya Kimataifa ya Ushauri kwa Bodi na Watendaji wa Barrick iliundwa kwa lengo la kutoa ushauri katika Nyanja za kisiasa, kijografia na masuala mbalimbali ya kimkakati yanayoweza kuathiri uendeshaji wa kampuni.

Ni wazi kwamba Barrick kama Mwanahisa Mkubwa (Majority shareholder ) wa Acacia, inayomiliki zaidi ya hisa asilimia 60 inaathirika zaidi na mgogoro unaoendelea kati ya Acacia na Serikali ya JPM.

Kwa mujibu wa malengo ya uanzishwaji wa Bodi, moja ya kazi zake kuu ni kuishauri Bodi ya Wakurugenzi na watendaji katika kutatua migogoro na hivyo kuhakikisha kampuni inajiendesha kwa faida na hivyo kulinda Imani ya wanahisa na wadau mbalimbali kwa kampuni.

Bila shaka katika hili la Zuio la Mchanga, Ripoti ya Prof. Mruma, kushuka kwa mapato ya Acacia, kuporomoka kwa thamani ya hisa zake katika masoko ya hisa ya dunia ni lazima litapelekea wajumbe hawa muhimu kukaa na kutoa maelekezo kwa Bodi ya Wakurugenzi au kufanya jambo kutokana na uzoefu na ushawishi wao.

Safu ya wajumbe hawa imesheheni watu maarufu, wanasiasa wenye ushawishi zaidi duniani na historia mbalimbali, mambo yanayofanya mgogoro huu kuwa na dhana ya umakini wa Tanzania katika kufikia malengo yake.

Wafuatao ni baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Ushauri na wasifu wao;

1. Mwenyekiti ni Hon. Brian Mulroney ambae amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Canada kati ya Mwaka Prime Minister 1984-1993

2. Mh.. José María Aznar ( Mjumbe) ambae amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Hispania kati ya Mwaka 1996-2004.

3. Hon. John R. Baird( Mjumbe) ambae amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada kati ya Mwaka 2011-2015

4. Gustavo A. Cisneros ( Mjumbe) , ambaye ni mfanyabiashara maarufu Nchini Dominica na Mwenyekiti wa Makampuni ya Cisneros Group of Companies

5. Secretary William S. Cohen( Mjumbe) ambae amewahi kuwa Seneta wa Marekani kati ya Mwaka 1979-1997 na pia Waziri wa Ulinzi wa Marekani kati ya Mwaka 1997-2001

6. Mhe. Newt Gingrich ( Mjumbe) , amewahi kuwa Spika wa 50 wa Bunge la Wawakilishi la Marekani (Speaker of the House of Representatives) kati ya Mwaka 1995-1999. Mwaka 2012, Gingrich alikuwa Mmoja wa watafuta uteuzi wa nafasi ya Urais ndani ya Chama cha Republican. (
https://en.wikipedia.org/wiki/Newt_Gingrich)

7. Mhe.Karl-Theodor zu Guttenberg ( Mjumbe), amewahi kuwa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani kati ya Mwaka 2009-2011.

8. Mhe. Lord Charles Powell of Bayswater KCMG( Mjumbe), ambae amewahi kuwa mshauri wa sera wa mambo ya nje wa Waziri Mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher 1983-1991.

9.
Mhe. Vernon E. Jordan, Jr. ( US) , ambae amewahi kuwa mshauri wa karibu wa masuala ya sheria wa Rais wa Marekani bwana Bill Clinton kati ya mwaka 1992-1993, mbali na hilo Vernon anatajwa kuwa Mfanyabiashara maarufu na Mtetezi wa haki za binadamu mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Marekani. Pia amehusika kwa kiwango kikubwa katika kashfa ya ngono maarufu kama Clinton–Lewinsky scandal.
10. Wengine ni Andrónico Luksic (Chile), Peter Munk
Canada (Founder and Chairman Emeritus, Barrick Gold Corporation) na John L. Thornton
United States (Executive Chairman, Barrick Gold Corporation).

NB: Andiko hili halina lengo la kuwakatisha tamaa, bali kufahamu vizuri adui yako, na pengine inaweza kuamua aina ya mbinu inayoweza kutumika kufikia ushindi.
Ni vigogo sana,dah!Kwa kuwa hawataki kuaibika watatulipa haraka.

Lakini Kikwete amekwenda kufanya nini Canada?Au amekwenda kuzunguuka mbuyu?Rais please take care. Huyu jamaa inawezekana amekwenda kuwapa mbinu pamoja na mengine.Si anajua system yetu?!
 
0fc1ad363f451c6b4daa73ad362a498b.jpg
a0670da4fc94144b10c5bfb1e5415b50.jpg
 
Punguza kujishushia heshima!
....Heshima tulishajishushia wenyewe long time ago, wenyewe tulienda kusaini mikataba mibovu,tena hotelini. Heshima pia mlijishushia wenyewe kupitia bunge kwa kupitisha sheria za hovyo.
 
....Heshima tulishajishushia wenyewe long time ago, wenyewe tulienda kusaini mikataba mibovu,tena hotelini. Heshima pia mlijishushia wenyewe kupitia bunge kwa kupitisha sheria za hovyo.
kwa hiyo tubaki hivyo hivyo tusiyasahihishe makosa?,...hata waliosaini hiyo mikataba wataendelea kutuita malofa tusiporekebisha
 
kwa hiyo tubaki hivyo hivyo tusiyasahihishe makosa?,...hata waliosaini hiyo mikataba wataendelea kutuita malofa tusiporekebisha
...Kusahihisha makosa kunafanywa kwa kukejeli wenzenu ambao all the time walikuwa wanawaonya on the same? Kusahihisha makosa kunafanywa kwa kuwa selective kwa waliohusika? Kwa nini bunge nalo halikuingizwa kwa ushiriki wake wa kupitisha sheria mbovu, tena kwa hati ya dharura? Tuanze na marekebisho ya katiba kwanza ...
 
...Kusahihisha makosa kunafanywa kwa kukejeli wenzenu ambao all the time walikuwa wanawaonya on the same? Kusahihisha makosa kunafanywa kwa kuwa selective kwa waliohusika? Kwa nini bunge nalo halikuingizwa kwa ushiriki wake wa kupitisha sheria mbovu, tena kwa hati ya dharura? Tuanze na marekebisho ya katiba kwanza ...
Mkuu unapokuwa na jaa anza na kilichopo kwanza ukisubiria ukipendacho,..we unafikirihao wanaweza badili katiba kirahisi rahisi...japo mwisho watakubali..kwa sasa tuanze na kilichopo tukisubiri kubadili katiba
 
Haijalishi hiyo Bodies ya Barrick imeundwa na wajumbe wa kaliba gani na ushawishi wa aina gani hayo ni ya kwao wao.

Sisi tunachoangalia na rasilimali zetu na mwekezaji anayetuibia mchanga jua linawaka kwa kutia taarifa ya uongo kuhusu kilichopo ndani ya makontena.

Huyo kwa Serikali hii ya Rais Magufuli hana nafasi Hata alie machozi ya damu hana nafasi huyo hafai kuendelea kuwa na sifa uwekezaji nchini.
Unajitoa akili,utaelewa tu,hii ngoma si ya kitoto musee
 
Back
Top Bottom