Bodaboda zinatudhalilisha sema basi tu hatuna jinsi

Full charge

JF-Expert Member
Mar 1, 2018
1,653
1,585
Hakuna kitu kinakera kama kupakiwa mshikaki,kwanza kuna hali fulani si ya kupendeza unakuta mke wa mtu kakaliwa nyuma na jamaa pale lazima jamaa liskie joto lake au shanga zake na kuvuta hisia.

Kero nyingine ni kile kitendo wanaume mnatangulizana halafu zote njemba hiyo kitu huwa siikubali hata kidogo yani bora nishuke kama sina nauli ya kupanda boda yangu.

Kosa ni pale umeogazako safi halafu mmepigwa mshikaki na mtu mchafu domo harufu chafu kikwapa cha maana wakati we umepuliza marashi yako.

Wadada wao wana kitabia fulani cha kusikilizia maumbile yako kama una tango au bamia pale unapomtanguliza mbele.

Upepo huwavua nguo wanawake tena zinapanda juu na kubaki uchi mbele za watu kibaya zaidi ikitokea ajali hapo ndiyo huwaburuza na kuwavua nguo zote uchi wa mnyama.

Boda ni usafiri wetu hususani sisi ambao hatuna uwezo wa kununua usafiri wetu binafsi ila isiwe kigezo cha sisi kunyanyaswa hata sheria sijui kama inautambua mshikaki
 
Back
Top Bottom