Wakubwa habari za huko kwetu!
Kuna binti wa kikenya niko nae huku kwa weupe! huyu binti nimekuwa nae karibu sana maana hapa tulipo ni mim na yeye ndiyo rangi yetu (black) na huwa namchukulia kama dada yangu. Ukaribu wangu kwake ni shule tosha jinsi wakenya walivyo na wanavyotuchukulia sisi watz.
Huyu binti kila tukiulizwa where are you from! (Nimen lai zi?) kabla hata sijavuta pumzi kujibu ameisha jibu KENYAAA! tena kwa msititizo mkubwa, napata hasra kweli kweli..
Hili swala linanikera sana, yaani hana subra yakusema ngoja mwenzangu leo ajibu au aseme natoka Kenya mwenzangu Tanzania ila jibu lake kila siku kutugeneralize..from Kenya! kwa ustarabu wa kitanzania huwa sitaki kumpinga kwa wakati ule.
Nilijaribu kushare nae siku moja lile swala la binti wa Odinga aliyesema oldvai gorge iko Kenya yaani ilikuwa mjadara mkubwa hakutaka kukubari kuwa hili eneo liko Tanzania..aligoogle na kugoogle, mwisho wa siku akasema walifundishwa hivyo kuwa eneo liko Kenya na pia wamefundishwa kutangaza nchi yao Kenya kwa nguvu zote.
Anawambia Kenya is very beutiful country than any other country in Africa!
Cha ajabu ananiambia mt Kilimanajaro iko boda ya Tanzania na Kenya so ni ya nchi zote!
Kama huyu binti anayasema haya kwa kujiamini inabidi serikali yetu na sisi watanzania tufanye kazi kubwa sana kubadiri hali hii.. huku duniani wakenya wanameisha wambia watu mt kilimanjaro na serengeti viko kenya.
Anasema kama hivyo vitu viko kwenu mbona hatuoni mkivitangaza! alafu wana wivu na sisi kwa kuwa na Magufuli! wanaona kwa siku chache zijazo twaweza kuwapita! kauli ya Magufuli kununua AIRBUS hili linamuumiza na kumnyima usingizi huyu mtoto wa kike.
Yaani wakenya na serikali yao wanatangaza kwa nguvu zote vivutio vyetu kuwa ni vyao!
Huyu binti wa kikenya atanisababishia kesi ya mauaji..