Bilioni 6 kupelekwa kwa Rais nini maana yake?

Dec 10, 2015
78
20
Waungwana na wapenda Maendeleo,

Awali ya yote nimpongeze Mh Rais kwa kazi ngumu ya kutumbua majipu ambayo yamekuwa ni matunda ya watangulizi wake.

Najua niwengi mmeona ama kusikia kitendo cha bunge kurudisha pesa kiasi cha bilioni 6 kwa Rais kimenipa kigugumizi, hivi ni kweli zile pesa zilistahili kurudi au ni makosa nikweli watanzania sasa hawana shida mbona tuna taka kutengeneza uzuri ambao ndai yake hauna uhalisia wowote.

Hizi ni changamoto za watanzania uhaba wa vituo vya Afya, Gari za wagonjwa, shule hazina madawati, Maji, Umeme barabara ndio usiseme ila fedha za kurudishwa kwa rais watanzania tufike mahala tufanye kazi kwa kujiamini nasio kwa woga nchi haijengwi kwa mashaka inajengwa na watu wanaojiamini na kazi wazifanyazo.

Mheshimiwa Rais nadhani anapata picha ya viongozi aliokuwa nao Rais anapambana ili watanzania waishi maisha bora wao wanamrudishia Fedha duuuu! Rais ukiona vyema hizo pesa ulizoletewa zirudi kwa wananchi kwakuboresha huduma muhimu ila zisipitie bungeni.
 



NIMETOKA KAPA SIJAAMBULIA KITU KTK UZI HUU.
 
Hujasikia JWTZ na Magereza ndio wamekabidhiwa hiyo hela kutengeneza madawati takribani laki na ishirini na yatasambazwa nchi nzima.?
 
Nitakuwa sijakosea kama nikisema kuwa mleta mada amekurupuka.....na inawezekana kukurupuka kwake kunaongozwa na mahaba juu ya jambo fulani....

Kila analipongeza bunge kwa kubana matumizi na hatimaye kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha ambacho moja kwa moja kimekabidhiwa kwa magereza kwa ajili kutengeza madawati kwa ajili ya kupambana na uhaba wa madawati kwenye mashule mbali nchi nzima....

Sasa sijui mtoa mada alitakaje labda....au alitaka hizo hela ziliwe ili aje kusheherekea kutumbuliwa kwa waliokula....??
 
s

siasa za kujipendekeza
 

Nasubiria matokeo ya hizi sarakasi
 
Bunge awakutakiwa kurudisha hizo pesa kwa Raisi.Wakitakiwa kuchangia hizo pesa kwenye huduma za kijamii kama elimu,maji,afya,kwa kuchagua mkoa mmoja au miwili na kuzielekeza hizo pesa uko.
 
Nafikiri ni swala lakuelewa mgawanyo wa majukumu kwenye mihimili ya serikali kwa maana ya sekali,bunge na mahakama.
Bunge haliwajibiki kwenye hayo unayoyasema hio ni kazi ya serikali,bunge liliomba pesa kwaajili ya mambo yakibunge,kama pesa walizoomba baada yakufanya majukumu yao zimebaki wako sahihi kuziridisha serikalini ili serikali izipangie kazi nyingine,ndio maana hata wao bunge hizo pesa wamepewa kutoka serikalini kwani ndio yenye kuwajibika na kutambua ni wananchi wapi wanahitaji nini na kwakiwango gani,ni serikali inafanya vitu kama sensa ili kukabiliana na haya na sio bunge,bunge wao wanawajibika kwenye posho za wabunge semina za bunge na gharama nyingine zinazohusu mambo yakibunge,hivyo kama wameshafanya hayo yote na pesa zimebaki wamefanya jambo lakizalendo kurudisha hizo pesa serikalini ili zipangiwe kazi nyingine
 
Don't you see this is what we call poor planning and budgeting?

Hivi inawezekanaje kusave 6bil kama sio kulikuwa na plan na budgeting mbovu.

Sina uhakika lakini ukifuatilia kiundani utagundua zimekuwa saved 6bil lakini zimepigwa more or less the same na 6bil.

Inawezekana hata hiyo bajeti inayosomeka 29tril ingekuwa pungufu ya hapo kukiwa na plan na budgeting nzuri
 
mwanzisha uzi ni hajaelewa pesa zinatoka kwa nani na zilitokana na nini katika upatikanaji wake, yeye kaona kukimbilia kuongelea matatizo ya wananchi ya kila siku tu. Hizo fedha zimeokolewa kwenye matumizi mabaya zimerudishwa kwa rais azipeleke kwa shughuli nyingine ya kijamii.
 
Bunge awakutakiwa kurudisha hizo pesa kwa Raisi.Wakitakiwa kuchangia hizo pesa kwenye huduma za kijamii kama elimu,maji,afya,kwa kuchagua mkoa mmoja au miwili na kuzielekeza hizo pesa uko.
Hivi wewe kichwa chako kiko sawa? Hivi madawati laki na ishirini yatakayo tengenezwa si huduma kwa wananchi?hivi uko sawa kichwani kweli?
 
Mkuu uko sawasawa kweli?
 
Nakubaliana na wewe inawezekana zimepigwa zaidi ya hizo ndio maana wakaona aibu na kurudisha kadhaa.....lakini hata hichi kilichopatikana basi tukifanyie mambo ya maana
 
Ubungo president bunge lilikua sahihi kurudisha hizo pesa otherwise xingeliwa na wabunge tu. Pia bunge halina uhalali wa kutatua shida za wananchi na pale wanapo fanya hivo wanatoa kama michango.pia kama pesa imetengwa kwa safar za nje.kama wameshindwa kwenda nje wana paswa kurudisha pesa na sio kuamua maamuzi mengine ndo maana raisi magu alipo kabidhiwa alielekeza ziende kutengeneza madawati kumaliza uhaba wa madawati.
I think hakuna kosa kwenye hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…