Bilioni 101.2 kujenga Barabara ya Kahama-Kakola KM 73 kwa kiwango cha lami

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,714
13,464
Serikali imesaini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama-Bulyanhulu Jct - Kakola (km 73) kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za kiuchumi za madini, Kilimo, Misitu na Utalii katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Tabora, Kagera na Kigoma.
WhatsApp Image 2024-03-16 at 18.11.08_3f3f49a3.jpg

WhatsApp Image 2024-03-16 at 18.11.04_ca0fc325.jpg
Mkataba huo umesainiwa kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa gharama ya Shilingi Bilioni 101.2 kwa ufadhili wa Kampuni ya Madini
ya Barrick Tanzania Mining Companies (BTMCs) na Serikali ya Tanzania.

Akishuhudia Utiaji Saini wa barabara hiyo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa barabara hii imekuwa ni kilio cha muda mrefu na sasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mzuri na wawekezaji wa ndani ya nchi ikiwemo kampuni ya Barick ametoa kibali barabara hiyo iweze kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.
WhatsApp Image 2024-03-16 at 18.11.06_2e71105a.jpg

WhatsApp Image 2024-03-16 at 18.11.04_2e27e94f.jpg

WhatsApp Image 2024-03-16 at 18.11.05_e2f5ff73.jpg

WhatsApp Image 2024-03-16 at 18.11.07_90088682.jpg
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Mhe. Rais pia ameelekeza Wizara ya Ujenzi kuanza hatua za kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Iloginhadi Mtakuja (km 57.4) ambayo ni barabara ya kiuchumi na inaunganisha Mkoa wa Shinyanga na Geita.

Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa mtandao wa barabara kwa zile za changarawe na zile za lami zilizopo Mkoani Shinyanga zitaendelea kusimamiwa na kuhudumiwa ili ziweze kupitika msimu wa kiangazi na vuli ikiwemo barabara ya Old Shinyanga - Solwa - Burige mpaka Kahama pamoja na ile Kolandoto-Lalago.

Bashungwa amemtaka Mkandarasi huyo kuona namna ya kuchangia huduma za kijamii kwa wananchi wanaouzunguka mradi huo pamoja na kushirikiana na wananchi wakati wa utekelezaji wa mradi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Mohamed Besta ameeleza kuwa Mkandarasi aliyeshinda zabuni ni Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa muda wa Miezi 27 na kusimamiwa na TANROADS Engineering Consulting Unit (TECU).

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa, ameomba ujenzi wa barabara uanzie katika mji wa Kakola ambapo wananchi wengi wamekiwa wakiteseka kwa ubovu wa barabara na kusisitiza mradi huo uweze kukamilishwa kabla ya muda uliopo kwenye mkataba kwa kuwa ana imani na kasi ya Serikali katika utekelezaji wa miradi.
 
Back
Top Bottom