Biashara ya Duka la vifaa vya ujenzi inauzwa( Hardware)

stanleyRuta

JF-Expert Member
Jul 19, 2014
851
519
Habari zenu wakuu,

Mimi ni mjasiriamali nayejishughulisha na biashara ya kuuza vifaa vya ujenzi hapa Dar es Salaam ambapo nimefanikiwa kuwa na maduka mawili katika sehemu mbili tofauti hadi sasa.Maeneo ya Kinzudi Salasala

Kiini cha kuandika Uzi huu ni kwamba nimeamua kuuza Duka mojawapo kati ya mawili baada ya kuwa mtu alokuwa ananifanyia kazi katika Duka mojawapo kuniibia kiasi kikubwa cha pesa ya mauzo na kukimbia,
Hivo nimekumbana na changamoto ya mtu Wa kuendesha hili Duka, hivo nimeamua nibaki na Duka moja.

Duka liko sehemu nzuri na tiyari lina wateja Wa kutosha hilo linajidhihirisha kwenye daftari la mauzo, mwenye kuhitaji kuona ataweza fika dukani na kujionea mwenyewe

Kuhusu location ya Duka liko njia ppanda ni center ilochangamka sana na watu bado wanajenga kwa kasi ( Dar, Salasala...Kinzudi)

Mwenye kuwa na uhitaji tafadhali tuwasiliane kwa 0754729751, 0716720444
 
Weka hata makisio ya bei basi, tulio wajuzi wa hardware tunaweza kutathmini ukubwa wa biashara iliyopo then tufanye biashara ikibidi
 
Weka bei Mkuu
 
Weka hata makisio ya bei basi, tulio wajuzi wa hardware tunaweza kutathmini ukubwa wa biashara iliyopo then tufanye biashara ikibidi
Mkuu naona kuweka bei nitashindwa ukizingatia Mimi nauza brand(Biashara ilokwisha kuanza na kuwa na wateja wake pamoja na bidhaa zilizomo)

Pia bei itategemea na jinsi wewe utaweza kuona location ya biashara iliko na pia ukishajionea trend ya mauzo.

Nakusihi tu ukipata muda tafadhali nitembelee dukani
 
Ungetaja bei unatupunguzia hata safar ya kuja kuona kama tukijua hatuwez kwa bei utayotaja
 
Ungetaja bei unatupunguzia hata safar ya kuja kuona kama tukijua hatuwez kwa bei utayotaja
Acha tu nitaje bei kulingana na matakwa ya wengi humu ndani ila ingefaa sana mtu kuja na kujionea.

Thamani ya biashara yenyewe ni MILIONI 11
 
Acha tu nitaje bei kulingana na matakwa ya wengi humu ndani ila ingefaa sana mtu kuja na kujionea.

Thamani ya biashara yenyewe ni MILIONI 11
Thamani hiyo ni kwa vitu viliyopo dukani na kodi ya jengo kwa muda gani? Toa mchanganuo nipange kuja kuona.
 
Acha tu nitaje bei kulingana na matakwa ya wengi humu ndani ila ingefaa sana mtu kuja na kujionea.

Thamani ya biashara yenyewe ni MILIONI 11
Kwa bidhaa za Hardware navyozifaham hiyo thaman ni ndogo, bilashaka una vitu vichache
 
Kwa bidhaa za Hardware navyozifaham hiyo thaman ni ndogo, bilashaka una vitu vichache
Mkuu kama umesoma Uzi wangu vizuri hapo juu , ni kwamba kijana alokuwa anafanyakazi dukani hapo kaniibia na kulifilisi Duka ikafika hatua akawa anachukua Mali anawauzia wenye maduka mengine ya hardware kwa bei ndogo hii ni kutokana sikuwepo nilisafiri......
Na hiyo bei nimefanya tu kukutajia sijafanya evaluation ila kimsingi siko tiyari kuiendesha tena hii biashara .
 
Kwa kutaja kwako bei sasa nipo tayar kuja kuona na kuzungumza mengne
 
Acha tu nitaje bei kulingana na matakwa ya wengi humu ndani ila ingefaa sana mtu kuja na kujionea.

Thamani ya biashara yenyewe ni MILIONI 11

Pole sana Mkuu, hii biashara bila kuisimamia mwenyewe ni ngumu sana.

Naomba ufafanuzi kidogo:
1. Chumba cha biashara pia kipo kwenye hiyo bei na kwa muda ganj?kama chako au ulipanga...
2. Je kuna bidhaa zilizopo ambazo mnunuzi atarithi kwa bei hiyo au ni duka tupu?na kama zipo ni bidhaa gani na kiasi gani?
 
A
Ahsante sana kiongozi kwa kunipa pole......changamoto ni nyingi ila kupigana siachi kamwe .
1 Frem ya biashara siyo yangu nimepanga.
2.Bei inajumuisha bidhaa tuu, kodi hiyo nimeamua ntafanya kama sehemu ya hasara.
Bidhaa zipo nyingi building materials na hardware.

Ukipata wasaa utakuja kujionea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…