Mtu ambaye hataki tuikosoe serikali ni wa kuogopa kama ukoma kwani moja ya faida ya kuikosoa serikali ni upatikanaji wa elimu bure mpaka kdt cha nne.Na sasa tunaona udhaifu mwingi kwenye sera ya uchumi hali iliyopelekea mizigo kupungua bandarini,watalii kupungua kwenye hifadhi zetu na,benki kufilisika,soko la hisa kuteteleka,na viwanda vilivyopo kuteteleka kiasi cha kupunguza wafanyakazi.Sasa ktk mazingira haya tunaambiwa mapato ya kila mwezi yameongezeka kiasi cha kuvuka lengo, kwanini tusiwe na mashaka kuwa huenda TRA wanapika takwimu kuogopa kutumbuliwa? Kwani kiuhalisia kama kweli mapato yameongezeka kwanini hatuongezewi mishahara yetu iliyositishwa kuongezeka,kwanini hatupandishwi madaraja yetu yaliyozuiwa, kwanini vijana hawaajiliwi hali kuna uhaba mkubwa wa walimu wa hesabu na sayansi,pamoja na wahudumu wa afya.Piakwanini kuna uhaba wa dawa hospitalini?Mwisho kwanini wastaafu wanamaliza mwaka sasa hawajalipwa stahili zao?