tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,307
- 4,585
Waungwana kuna mambo maishani huwa yanapotazamwa humuachia mtazamaji kila aina ya tafakuri kichwani mwake. Ndani ya miaka kadhaa ya hivi karibuni, kumezuka tabia ya watu kuitundika bendera ya Israel kwenye sehemu ya chini ya kioo cha ndani ya gari, kile ambacho dereva hukitumia kutazama magari yanayokuja kutokea nyuma ya gari.
Mwanzoni nilidhani ni mahaba binafsi ya mtu mmoja, lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo mashabiki wa bendera hiyo maarufu duniani, walivyozidisha tabia hiyo.
Huwa najiuliza kama Waisrael na wao wanayo tabia ya kuitundika bendera ya Tanzania, katika sehemu ile ile ambayo sisi tunaitundika bendera yao ndani ya magari yetu. Huwa najaribu kujiuliza iwapo Mtanzania anayekatiza katika mitaa ya Jerusalem au Tel Aviv anaweze kukutana na gari ambalo ndani yake kuna bendera ya Tanzania imetundikwa, na muisrael akiendesha gari huku akiufurahia uwepo wa bendera yetu.
Haya ni mawazo yangu, kwani tabia hii imenifanya nijiulize iwapo upendo unaotoka mioyoni mwetu kuelekea kwa Waisrael, unaweza na wenyewe kuwa unathaminiwa na Waisrael bila ya sisi Watanzania kujua ni jinsi gani tunavyothaminiwa.
Mkuu hilo jina Phillipo Bukililo ni lako?