Mwaka 2015 mwezi wa Oktoba kilo moja ya Sembe ilikuwa Tsh. 800/= hapa mtaani kwetu. Ilianza kupanda taratibu hadi majuzi kufikia Tsh.1600/= kwa kilo. Jana nimetuma mtoto wa jirani akaniletee nusu kilo nije kujipikia ka-ugali kangu nikampa Tsh.1000/= nikijua atanirudishia chenji Tsh.200/= maana kwa kuwa bei ilikuwa ni Tsh.1600/= kwa kilo.
Dogo alipoleta sembe nikamwambia "Asante sana mdogo wangu, hio chenji chukua tu utaenda kununua Aisikirimu", Dogo alinijibu "Mbona hela yote imeisha, kilo moja ya Sembe ni Tsh.2000/=".
Hapo niliishiwa pozi kwani kwa sasa Sembe mtaani kwetu limezidi bei ya mchele. Wale tuliokula tukila ugali hata usiku na kuonekana hatuna uwezo wa kula wali, sasa hivi tunaheshimika kwani mchele wa Ifakara kilo moja ni Tsh.2000/= mtaani kwetu.
Kwa mwendo nafikirisha akili yangu na kujiuliza hali hii itaendelea hadi lini kwani ukame huu na mavuno hayaeleweki. Natabiri kufikia Juni mwaka huu tutanunua kilo moja kwa Tsh. 5000/=