BASATA mnabeba lawama ya mmomonyoko wa maadili

kimaus

JF-Expert Member
May 10, 2011
582
707
Baraza la Sanaa la Taifa kwanini mmekuwa na kigugumizi kwenye muziki usio na maadili. Siku hizi nyimbo nyingi zina matusi, hazina maadili au zinachochea mmomonyoko wa maadili lkn cha kushangaza zinapigwa kwenye vituo vya redio na Televisheni.

Watoto wetu wanaimba nyimbo za ajabu kwa kuwa wanaziona zinapigwa. Nguvu inayotumika kushughulikia nyimbo zenye maudhui ya kisiasa itumike pia kushughulikia nyimbo zinazosifia ngono, pombe na mihadarati.

Mi ni mzazi na nikiangalia muziki wetu naogopa sana kizazi kijacho nchi hii kitakuwa cha aina gani!
Sihitaji kutaja nyimbo maana zipo nyingi sana, tafadhali BASATA okoeni maadili yetu kwa kuhakikisha kila wimbo kabla msanii hajautoa uwe umepita kwenu na umekuwa censored.

Kama hii kitu inafanyika sasa hv basi BASATA mjitathmini maana nyimbo nyingi zinatoka hazina maadili bado. Ni ngumu kuzuia wimbo kwa kutaka vituo vya redio na TV visiupige maana digital platforms na devices zipo nyingi, lkn mkiweka kanuni ya kutaka kila msanii ku submit wimbo wake kabla kusikika mtaani basi tunaweza kudhibiti nyimbo zisizo na maadili maana wimbo ukisikika popote na haujapita kwenu basi msaanii akamatwe.

Hatuwezi kuacha vijana wachache watuharibie vizazi vyetu kwa kisingizio cha sanaa!

Najua kuna vijana watapingana na mimi lkn ukiwa mzazi unayewaza future ya watoto wako mtaona hoja yangu.
 
Wenyewe wanakuambia sahv ukiamba matusi Ndiyo kuna soko

Ova
 
Wapo tayari kufungia nyimbo zinazoponda Ufisadi wa Viongozi Lakini siyo zenye maudhui ya Matusi.Mbona Alli kiba nyimbo zake zina Maadili na watu wanazipenda
Si ndiyo hapo,ila wanaoimba na kuhamasisha watu wazibuane mtr,kuzagamuana wanaachiwa
Wenyewe wanakuambia soko sahv ndiyo linataka
Mpaka kufika 2030 vitoto vitakuwa vimechakaaaa

Ova
 
Baraza la Sanaa la Taifa kwanini mmekuwa na kigugumizi kwenye muziki usio na maadili. Siku hizi nyimbo nyingi zina matusi, hazina maadili au zinachochea mmomonyoko wa maadili lkn cha kushangaza zinapigwa kwenye vituo vya redio na Televisheni.
  1. Kwenye daladala ambako wanafunzi wengi wanasafiria
  2. Kwenye sherehe mitaani ambako wanafunzi wengi wanaishi
  3. Kwenye school buses
  4. Kwenye mabasi yanayokodishwa kupeleka wanafunzi tour
  5. Kwenye mabasi ya abiria
  6. Kwenye mikutano ya siasa
  7. Kwenye maduka ya mahitaji muhimu
  8. Kwenye barber shops
Watoto wetu wanaimba nyimbo za ajabu kwa kuwa wanaziona zinapigwa. Nguvu inayotumika kushughulikia nyimbo zenye maudhui ya kisiasa itumike pia kushughulikia nyimbo zinazosifia ngono, pombe na mihadarati.
Mkuu hebu tutazame kwanza age ya walioko huko BASATA, huenda hawajui kabisa maana ya maadili, zamani alikuwepo Yustus Mkinga ambaye ni Mwalimu, college mate wa Jenista Mhagama na Jumanne Sagini pale Korogwe TTC, kwa umri wake na taaluma yake sidhani kama haya ya huo muziki angeyafumbia macho labda kuna nguvu inamdhibiti
 
Napenda nikilewa nipande juu ya meza, nipande juuu yyaaa mezaaaa...nipande juuu ya mezaaaa. Huku bonge la bibi na mitako hiooo kaiwacha wazi anaitingisha.....halafu tunaona sawa tuuuu.

Acha Tu Mungu Atuletee kila aina ya majanga...na bado
 
Suluhisho ni kuhakikisha msanii hatoi wimbo kabla ya kuupitisha Basata na wausikilize na kama kuna mashairi yasiyo na maadili basi msanii aambiwe akayaondoe. Maana wimbo ukishatoka huwezi kuuzuia!!
 
Tatizo limeanzia mbali,wapo waliopata umaarufu kupitia nyimbo chafu,na Sanaa chafu,hivyo wanakosa ujasiri wa kuwaandama wanaoibuka leo kwani wenye dhamana walifikiria na kuendekeza matumbo yao,hata kusahau wajibu wa msingi kwa jamii yao,taifa na hata nwajiri anayemlipa kwa jukumu aliloshindwa kutekeleza.
 
Wasanii wa zamani walikuwa wakiimba wapenzi na vimbwanga vyao.

Wasanii wa kati walikuwa wakiimba , wapenzi, mapenzi na vimbwanga vyake.

Wasanii wa sasa wanaimba kulombana na yanayofanana na hayo je wasanii wajao watatuimbia nini?

BASATA ni genge la wahuni wanaolipwa kodi za wananchi.
 
Suluhisho ni kuhakikisha msanii hatoi wimbo kabla ya kuupitisha Basata na wausikilize na kama kuna mashairi yasiyo na maadili basi msanii aambiwe akayaondoe. Maana wimbo ukishatoka huwezi kuuzuia!!
Kuna wasanii washenzi wanavujisha nyimbo kabla haijapewa ithibati
 
Wao wenyewe hawana maadili

Nchi sahv maadili sifuri

Nchi imekuwa kama sodoma na gomorrah tu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…