kimaus
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 582
- 707
Baraza la Sanaa la Taifa kwanini mmekuwa na kigugumizi kwenye muziki usio na maadili. Siku hizi nyimbo nyingi zina matusi, hazina maadili au zinachochea mmomonyoko wa maadili lkn cha kushangaza zinapigwa kwenye vituo vya redio na Televisheni.
Watoto wetu wanaimba nyimbo za ajabu kwa kuwa wanaziona zinapigwa. Nguvu inayotumika kushughulikia nyimbo zenye maudhui ya kisiasa itumike pia kushughulikia nyimbo zinazosifia ngono, pombe na mihadarati.
Mi ni mzazi na nikiangalia muziki wetu naogopa sana kizazi kijacho nchi hii kitakuwa cha aina gani!
Sihitaji kutaja nyimbo maana zipo nyingi sana, tafadhali BASATA okoeni maadili yetu kwa kuhakikisha kila wimbo kabla msanii hajautoa uwe umepita kwenu na umekuwa censored.
Kama hii kitu inafanyika sasa hv basi BASATA mjitathmini maana nyimbo nyingi zinatoka hazina maadili bado. Ni ngumu kuzuia wimbo kwa kutaka vituo vya redio na TV visiupige maana digital platforms na devices zipo nyingi, lkn mkiweka kanuni ya kutaka kila msanii ku submit wimbo wake kabla kusikika mtaani basi tunaweza kudhibiti nyimbo zisizo na maadili maana wimbo ukisikika popote na haujapita kwenu basi msaanii akamatwe.
Hatuwezi kuacha vijana wachache watuharibie vizazi vyetu kwa kisingizio cha sanaa!
Najua kuna vijana watapingana na mimi lkn ukiwa mzazi unayewaza future ya watoto wako mtaona hoja yangu.