BASATA kaeni mkao wa kula, Video ya Chura anarukaruka, ikitoka fungia kisha tia Kapuni

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Heshima kwenu wakuu,

Hii video ya Snura ya Wimbo wa Chura anarukaruka, ikitoka tu naomba ifungiwe. Mkishaifungia mumpige msanii marufuku ya kujihusisha na Muziki kwa Miaka mitatu. Hatuwezi endelea kulealea huu ujinga.

Kama mliweza kuufungia Wimbo wa Roma wa Viva Roma Viva ambao haukua na tatizo katika Swala la maadili, naamin huu wimbo ukitoka msanii atawekwa mbaroni hata siku mbili.

Imetosha sasa kwa hawa dada zetu kujifanya eti wamepinda, wao ndo wanajua kukata mauno, wao ndo wanajua kutembea uchi.

Naomba BASATA msiangalie Nyani usoni

==========

Updates;

Asanteni BASATA, hakika mumeonesha mlivyo makini na kazi yenu, Taasisi na Mashirika ya Serikali yote yangekuwa kama ninyi, Tanzania tungekua mbali sana katika hatua ya maendeleo.

Hii habari imenifariji=>Msanii Snura afungiwa kujihusisha na sanaa, TCRA waagizwa kuifuta video ya Chura mtandaoni

Pia Soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Mtoa mada mauno yake yanakuweka kwenye hal mbaya eenh!
Hivi ni mchaga wa wapi ana mauno hivi?
Nkiangalia najiskia aibu coz inakuwa too much!
 
Chura anarukaruka churaa in snura's voice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…