BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 497
- 1,200
Mtakwimu Mkuu wa Serikali,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
S. L. P. 2683,
DODOMA.
Ndugu,
Napenda kufikisha malalamiko ambayo pia nitafungua kesi Mahakamani kuishitaki NBS kwa kutozingatia vigezo vya Human Machine Interface (Usability and User Experience (UX)) katika mfumo wenu wa kuomba ajira za Sensa.
Nafanya hivi kama Mtaalamu wa TEHAMA ili kuwapa elimu (awareness) Watanzania, wazijue haki zao za msingi kama Watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA hasa ya huduma muhimu kama hii ya kuomba ajira.
Kuna mapungufu yafuatayo katika Mfumo wenu ambayo ni upande wa Developers na sio upande wa Internet Connectivity issues:
Kwa kanuni za Human Machine Interface hivi vitu sio sawa labda kama mmetumia Junior Developers, lakini ni aibu kwa Taifa letu kuwa na Mfumo kama huo kutoka Taasisi kubwa ya Serikali kama NBS. Mmeweka njia pekee ya msaada ni kupiga simu kwenu, simu ambazo muda wote hazipatikani au zipo busy.
Kama Google au Instagram au Facebook ambazo zinatumiwa na Watanzania karibia milioni 20 zingetumia mfumo wa kwenu, sidhani kama zingepata Watumiaji wengi Duniani. Kuna Mifumo mingi sana Tanzania ambayo ni bora sana na zina mfumo mzuri wa self-help na learnability kwa Watumiaji bila kuwa na haja ya kupiga simu huduma kwa wateja.
Kuna njia nyingi sana ambazo ni user friendly za kumuelekeza Mtumiaji wa Mfumo kujisaidia mwenyewe bila kuwa na haja ya kupiga simu. Na kwa maendeleo haya ya teknolojia hapa Tanzania sidhani kama kuna mtu ambae alikaa darasani akasoma Computer Science au Computer Engineering kwa miaka 3 au 4 anaweza kuwa hajui namna ya kumpa uhuru Mtumiaji wa Mfumo wa TEHAMA katika kufikia lengo anapoingia katika Mfumo fulani wa TEHAMA.
Kwenye mfumo wenu Watumiaji wanaweka taarifa kama namba zao za simu, namba za NIDA pamoja na e-mails zao, zingetosha kabisa kuwapa uhuru watumiaji kuweza kupata password mpya iwapo za mwanzo zinamsumbua bila kuwa na haja ya kuwapigia simu nyie.
Na bado usalama wa kimtandao ungekuwa haujaharibiwa kabisa, lakini pia Watumiaji walitakiwa kupewa uhuru wa kubadilisha password na kuweka password ambazo ni rafiki zaidi kwao kuweza kukumbuka.
Sasa na ndiyo maana naita huu ni utapeli umefanywa na Taasisi yako. Rekebisheni hizo kasoro na matangazo ya ajira yatolewe upya. Kama kweli mnataka kutenda haki mbele za Mungu.
Wako Katika Ujenzi wa Taifa,
Ni mimi Mtanzania mzalendo
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
S. L. P. 2683,
DODOMA.
Ndugu,
YAH: UTAPELI KATIKA MFUMO WENU WA TEHAMA WA KUOMBA AJIRA ZA MUDA ZA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Napenda kufikisha malalamiko ambayo pia nitafungua kesi Mahakamani kuishitaki NBS kwa kutozingatia vigezo vya Human Machine Interface (Usability and User Experience (UX)) katika mfumo wenu wa kuomba ajira za Sensa.
Nafanya hivi kama Mtaalamu wa TEHAMA ili kuwapa elimu (awareness) Watanzania, wazijue haki zao za msingi kama Watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA hasa ya huduma muhimu kama hii ya kuomba ajira.
Kuna mapungufu yafuatayo katika Mfumo wenu ambayo ni upande wa Developers na sio upande wa Internet Connectivity issues:
- Mtumiaji akishajaza Mkoa, Wilaya, Halmashauri, Jimbo, kuna Taarifa za Tarafa, Kata na Mtaa zinachelewa sana kuonekana na inachukua muda kama sekunde 30 kwa baadhi ya Mikoa (sio yote). Hiyo shida ipo kwenye Algorithms ambazo zimetumika hapo na sio Internet Connectivity. Maana ake Testing haikufanyika kisawa sawa inavyotakiwa.
- Link ambayo mtumiaji anatakiwa ku-click ili aweze ku-print application form kwa ajili ya kuweka saini pia ina shida ambayo ni upande wa Developers pia kutokuwa makini kuzingatia kanuni za Usability and UX.
- Ukishamaliza kujaza form unatumiwa password kwa njia ya e-mail, lakini kuna wakati hiyo password inakataa au username inakataa. Lakini katika Mfumo wenu hakuna option ambayo mtumiaji amepewa kuweza ku-recover password yake ikiwa ameisahau au anataka kuweka password ambayo ni rafiki kwake kuikumbuka, hilo ni jambo la ajabu sana na Developer gani anaweza kufanya designing ya aina hiyo (Na hili ndo tatizo kubwa Zaidi kwenye Mfumo wenu).