Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 59,506
- 103,168
Namtafuta sana diwani wa buyuni kama una namba yake nipatie, huyu nataka nimueleze waziwazi aendelee kula posho tu za udiwani kamwe asiwaze wala kujisumbuwa kuja kugombea tena.Tena kweli italian kwenda kigezi utazan hakuna viongozi hata umeme tu hakuna haraafu wanasema umeme vijijin wakati hapahapa bongo haujafika
Safi sana Matola, viongozi ni lazima wawajibike kwa mazuri na/au mabaya bila kujali itikadi.
Ndivyo mnavyopaswa kuishi ni viongozi wetu, kuwaambia ukweli peupe tena usoni.
Duh, poleni, huko hali itakuwa mbaya maana ni uzi wa pili huu toka mtu tofauti.Uvumilivu una kikomo, mimi nikiwa kama mdau wa jimbo la Ukonga kata ya buyuni wakazi tunaotumia barabara ya Italian kuingia Kigenzi ni kwamba tupo kisiwani, kuna two option za kuingia upande wa Kigenzi kwa Bafana Bafana either uingilie kwa Zoo au uingilie Italian.
Lakini jambo la kusikitisha kabisa njia hizi zote mbilihaziingiliki wala kutoka, hata ile ya kwenda kutokea kitunda haipitiki pia, ukiwa na gari yako binafsi ni mateso na ukiwa mtumiaji wa bodaboda ndio usiseme, maisha yamepanda bei, umbali wa kilometer moja tu kutoka barabara ya lami kuingia huko ndani bodaboda ni shilling 2000 that means kwa siku unahitajika kuwa na shilling 4000 za kupanda bodaboda tu kutoka nyumbani na muda wa kurudi hii ni nje nauli za daladala kwa route utakayokuwa unaenda kwenye shughuli zako na pia kutokana na ujenzi wa flyover Tazara watu karibu wote wa ukanda huu ushuka mwisho wa lami au gongo la mboto na kuunganisha treni kuwahi makazini.
Maisha yamekuwa ghali haisemekani watu wapo kimya lakini kimya chao msichukulie ni mazuzu, jambo la kusikitisha zaidi diwani wa kata ya buyuni na mbunge wa Ukonga wote ni Chadema, inasikitisha na inaudhi na haivumiliki kamwe.
Leo nimeamuwa rasmi kuihamisha familia yangu na ninaicha nyumba yangu ya Buyuni na nitarudi kuishi nilipotoka awali siwezi kuishi kwa mateso ya aina hii ndani ya capital city tena kwenye territory inayoongozwa na viongozi kutoka chama nilichokiamini Chadema.
Kitu kimoja tu ninachowaahidi katika waraka huu ni kwamba wote wawili mtang'oka na msije kujisumbuwa kugombea tena.
Sijawahi kuona juhudi zozote shirikishi za viongozi hawa, wangekuwa wanajitambuwa wakazi wa maeneo ya huku wako tayari kuunganishwa na kuchangia vifusi lakini wapi mbunge anawaza kula kichuri tu na Wakurya wenzake na diwani ndio maandazi kabisa.
Ole wenu Chadema msiseme Matola hakutowa onyo hapa JF, hawa viongozi nitahakikisha wanang'oka.
Cc: Tumaini Makene jiandaeni kuwatafutia vibaruwa vingine hii mizigo yenu, hawana msaada hawafai.
Mateso tunayoyapata hayavumiliki na hayakubaliki, hawa watu ni lazima tuwawajibishe warudi kijiweni waone maisha yalivyo magumu kama wao wana uwezo wa kukodi bodaboda kila siku kwa sehemu ambayo kimsingi ilipaswa kutolewa huduma na bajaji kwa shilling 500 tu.Waitara aendelee kulala hivi hivi, tunamshitua lakini wapi. Kwa akili zake anafikiri 2020 chadema itambeba, asitegemee ilo....
Juzi wameanzisha uzi kuhusu jimbo hili la ukonga, leo tena wewe.
Ni kwamba barabara ya kutoka njia panda ya kitunda hadi fremu kumi njia ni mbovu... Na kipindi hiki cha mvua makorongo ni ya kutisha. Wenye magari madogo wanapaki nyumbani... Daladala ni za shida asubuhi hadi jioni...
Kivule ni sehemu maarufu na yenye wakazi wengi lakini mbunge hapigani kwa ajili la ili jimbo, angetuhamasisha hata kuchonga barabara, hela za kifusi tungechangia. Barabara imekuwa mbovu kupita maelezo....
Akiendelea kujiziba mdomo na bandeji kumuiga mbowe, ikifika 2020 tutamrudisha mtaani naye aje asote...
Hali iliyopo haiwezi kuvumiliwa kwa namna yoyote ile, hizi mvuwa hazikuja kwa bahati mbaya na zitaisha na December zitanyesha tena, ni kitu ambacho kipo seasonal kabisa, sitaki kumsikia kiongozi wa kujitetea ati mvuwa, kwani mvuwa si zipo kila mwaka season mbili? Ni uzembe na kutokuwajibika tu, na ufumbuzi na dawa ya wasiowajibika dunia nzima ni kuwang'oa tu madarakani.Duh, poleni, huko hali itakuwa mbaya maana ni uzi wa pili huu toka mtu tofauti.
Hali iliyopo haiwezi kuvumiliwa kwa namna yoyote ile, hizi mvuwa hazikuja kwa bahati mbaya na zitaisha na December zitanyesha tena, ni kitu ambacho kipo seasonal kabisa, sitaki kumsikia kiongozi wa kujitetea ati mvuwa, kwani mvuwa si zipo kila mwaka season mbili? Ni uzembe na kutokuwajibika tu, na ufumbuzi na dawa ya wasiowajibika dunia nzima ni kuwang'oa tu madarakani.Duh, poleni, huko hali itakuwa mbaya maana ni uzi wa pili huu toka mtu tofauti.
Huyu jamaa aendelee kuleta mzaha, kuna siku nilipanda daladala jioni kuelekea fremu kumi, kila mtu alikuwa anaongea vibaya kuhusu mbunge....Mateso tunayoyapata hayavumiliki na hayakubaliki, hawa watu ni lazima tuwawajibishe warudi kijiweni waone maisha yalivyo magumu kama wao wana uwezo wa kukodi bodaboda kila siku kwa sehemu ambayo kimsingi ilipaswa kutolewa huduma na bajaji kwa shilling 500 tu.
Watu wengine wana magari yao njia zote hazipitiki ni nini hiki? Upuuzi mtupu hili halikubaliki kamwe na Chadema kama chama kijiandae kulipia gharama ya uzembe huu.
Watu wana pesa za kuchangia miundombinu inakuwaje kiongozi hata kumobilize watu ushindwe? Uligombea uongozi ili iweje?
Mwenyekiti wa mtaa atafanya nini wewe... Hapo ni mbunge akisaidiana na diwani..... Kwa sababu barabara imeunganisha mitaa mingi, sasa kila kiongozi wa mtaa atoke uko si itakuwa fujo na panya wengi hawachimbi shimo...Mwambieni mwenyekiti wenu wa mtaa aitishe kikao muongelee kuhusu kuchanga fedha kwa ajili ya kifusi mkikubaliana nendeni kwa mkurugenzi wa manispaa awape greda na mtaalamu wa halmashauri kama hata mwenyekiti hawezi kufanya hilo basi tatizo litakuwa kwa waliowachagua na siyo hao viongozi namaainisha mlichagua viongozi maboga kwa sababu tu walitoka chadema.