MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
Baada ya TFF kuona Mechi za Nusu Fainali ya ASFC zinahusisha Timu Kubwa na zenye Ushawishi nchini Simba, Yanga, Azam na hata Biashara United FC tayari Krav Maga nimeshtukia Jambo.
Barua kutoka TFF kwenda kwa Bodi ya Ligi ( TPLB ) jana kuwa ihakiki Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi ( Tabora ), Majimaji ( Ruvuma ) na Lake Tanganyika ( Kigoma ) kama vipo tayari Kuchezewa Mechi hizo ni kutaka tu Kutuzuga na Kutuandaa Kisaikolojia Wadau wa Soka nchini Tanzania.
Kinachoenda Kufanyika hapa ni kwamba Majibu ya TPLB yatasema Viwanja Tajwa hapo juu haviko tayari hivyo TFF ipange Viwanja vingine vizuri vya Kuchezea Mechi hizo Mbili kama si Tatu zenye Mvuto wa Kipekee nchini.
Kwakuwa tayari TFF wameshajua kuwa wana uwezo wa Kutengeneza Pesa Kubwa sana kuanzia ngazi hii ya Nusu Fainali na ile ya Fainali kama Simba na Yanga zitashinda Mechi zao Krav Maga nimehisi yafuatayo kutangazwa Siku si nyingi.
Kwakuwa inajulikana kuwa Ngome ya Simba SC ni Mkoa wa Arusha hivyo Mechi ya Azam na Simba ( Nusu Fainali ya ASFC ) itaamriwa icheze huko Sheikh Amri Abeid Kaluta ( Arusha ) ambako najua Nyomi litakuwa Kubwa na TFF kupata Mapato makubwa.
Kwakuwa inajulikana kuwa Ngome ya Yanga SC ni Mkoa wa Mwanza hivyo Mechi ya Biashara United na Yanga ( Nusu Fainali ya ASFC ) itaamriwa ikachezwe CCM Kirumba ( Mwanza ) ambako najua Nyomi lake litakuwa si la Kitoto na TFF kupata Mapato mengi tu.
Baada ya Mechi hizo za Nusu Fainali ya ASFC Kuchezwa na TFF najua tu watalazimisha Simba na Yanga zitinge Fainali tegemeni Fainali yake Kuamriwa ichezwe Uwanja mkubwa wa Benjamin Mkapa ambako hapo TFF ndiyo wanaenda Kupata Mapato ya Kufuru kwakuwa Mechi hiyo itakuwa na Mvuto baada ya Kuhairishwa Kwake Kipuuzi ( Kipumbavu ) tarehe 8 May, 2021.
Hivyo basi kwakuwa Uchaguzi Mkuu wa TFF unaenda Kufanyika tarehe 7 August, 2021 huenda Mkakati huu wa Siri ambao Krav Maga ( Mzee wa Nongwa na Fukua Fukua ) nimeuhisi ni kwamba Bajeti za Mkutano huo mkubwa wa TFF na Pesa za Kuhongea Wajumbe wa Mkutano Mkuu huo zitategemea Mapato ya kuanzia Mechi za Nusu Fainali ya ASFC, Fainali ya ASFC na ile Mechi ya Watani wa Jadi ( Simba na Yanga ) inayojulikana katika Ratiba ya tarehe 3 July, 2021.
Ukibarikiwa Akili nyingi ni raha sana tu.